OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Msikilize Easy E -Ezekiel Kamwaga akiongea kwa staha, weledi na umakini mkubwa. Anaongea kama msomi na mtu mwenye exposure. Hakuna porojo, povu wala mapovu.
Anaeleza issues na vipengele kwa kina katika mipaka yake ya usemaji. Hata kwenye page yake ya Insta mashabiki tunapata facts zilizonyoshwa na rula saaafi kabisa. Porojo tupa kule.
Kwa sababu Simba Sc imechagua kwenda kimataifa Level za Al Ahl, Mamelod nk. Huyu ndio msemaji sahihi katika safari hiyo.
Katika clip hiyo jamaa mmoja amewapa tahadhari Simba kwamba watu walioomba nafasi ya usemaji wanaonekana kuwa watu wa mapovu kama ya Mr.Buga (sio Bugatti, Bugatti hawezi kuishi kwa majungu, vijembe na umbea). Naushauri uongozi wa Simba umbakishe huyu mtu kwa mkataba wa kisoma.