The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 4,249
- 11,592
Mwanahabari mwandamizi na mchambuzi wa siasa za bara la Afrika, Ezekiel Kamwaga, amesema Watanzania mara nyingi husahau matukio muhimu yanayojiri nchini mwao kiasi cha kushindwa kuthamini na kuheshimu matendo mema ya baadhi ya viongozi na wananchi wenzao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mdahalo wa kiuchumi ulioandaliwa na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC) na kuhudhuriwa na wachambuzi wa masuala ya uchumi, Kamwaga amesema tabia hiyo imekuwa ikidhihirika hata katika matukio makubwa ya kitaifa.
Akitoa mfano, Kamwaga alirejelea tukio la mwaka 2017 ambapo mwanasiasa Tundu Lissu alipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya. Amesema wakati huo kulikuwa na viongozi waliokwenda Nairobi kumjulia hali Lissu alipokuwa akipokea matibabu, akiwemo aliyekuwa Makamu wa Rais wa Tanzania ambaye sasa ndiye Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye aliruhusu picha ichukuliwe licha ya kuwepo mashaka kutoka kwa baadhi ya watu. Hata hivyo amedai pamoja na yote aliyofanya Dkt. Samia kwa Lissu bado kuna watu wanasema kwamba hampendi Lissu. Si kweli, Rais Samia anampenda sana Tundu Lissu🤔🤔🤔
Amesisitiza kuwa ili taifa lisonge mbele, ni muhimu Watanzania wakajenga tabia ya kuheshimu na kukumbuka mambo mazuri yaliyofanywa na viongozi na wananchi, badala ya kusahau au kuyapuuza.
Huyu ndiye Ezekiel Kamwaga. Bila shaka anaitafuta nafasi ya Gerson Msigwa pale magogoni. Ataliweza timbwili lake kweli huyu..?