Mvumbuzi,
Nashukuru sana kuwa umetoa angalizo kwa serikali juu ya kadhia hiyo, ili wafanye uchunguzi.
Kampuni hii naifahamu, maana kwa namna moja ama nyingine ofisi yangu ina udau na kampuni za Watalii.
Mara baada ya kusoma article ya Mvumbuzi nilifuatilia kwa jamaa wenye uhusika wa moja kwa moja na uendeshaji wake wakanipa maelezo yao.
Wanasema kwamba ni kweli wazungu wanafanya hiyo kazi ya tour-guide. Lakini wanasema kuwa kampuni hiyo ina namna tofauti ya operations kulinganisha na tour companies tulizozizowea hapa. Wazungu hao(tour-guides) wanatafuta watalii wenyewe katika nchi mbalimbali huko duniani na kuja nao huku, hivyo hawawezi kuwakabidhi kwa waswahili wawatembeze, wakati wao ndio wamebeba risk yote kuwasafirisha na kuwa 'care, na wanasema itakuwa si customer care nzuri, kitu ambacho kitawafanya wageni hao wasirudi tena kwa kampuni hiyo!
Kwa reasoning ya kawaida, sababu hiyo haitoshelezi kabisa kuwakosesha kazi tour guides wetu, zaidi sana ninachokiona mimi hapo ni aina ya ubaguzi wa rangi wa wazungu ambapo wanaona mswahili hataweza kutoa maelezo fasaha kwa mgeni!
Lakini hilo ni kosa la kiufundi. Tunafungua milango hadi ya vyumba vya siri kwa wageni.
Naungana na Mvumbuzi hizi ni kazi rahisi sana za waswahili wenzetu, hii ingekuwa sheria rahisi sana kuimplement dhidi yawatu hawa weupe, sielewi ugumu unatokea wapi.