Gerad2008
JF-Expert Member
- Jun 9, 2009
- 583
- 287
Heshima kwako Mvumbuzi.
Mkuu ni kweli tour guide wageni wamevamia kazi za wazawa.Bahati mbaya serekali ya magamba haina habari na masuala kama haya UWT iko kwaajili ya kuidhibiti CHADEMA na chama chochote kitakachotishia maslahi ya CCM.Miezi kadhaa iliyopita nilikuwa nafanyakazi fulani na kampuni ya SOKWE ASILIA nilishangaa kuanzia muhasibu,Inventory,manager wa camps,IT manager na key posts zote zimekamatwa na wageni [Kenya,Zimbabwe na S/Africa wazungu].Mishahara ya wafanyakazi wa wageni ulipwa kwa US Dollar[$ 5,000 - 12,000] pia haikatwi SDL,PAYE na NSSF.Hesabu za SOKWE ASILIA zinafungwa Kenya na South Africa.Hii ni kampuni moja yenye wafanyakazi wazawa zaidi ya 300 lakini wenye kulipwa kiwango kidogo cha mishahara Tsh 100,000 - 500,000/=.
Ukienda SERENA utashangaa nafasi zote kubwa zimeshikwa aidha na wahindi au wakenya.Ukwepaji wa kodi za serekali SDL,PAYE na Corporate Tax ni mkubwa kupita maelezo.Maafisa wa TRA mkoa wa Arusha wengi wana maisha ya juu kwasababu ya kushirikiana na haya makampuni kuinyima serekali mapato.wengi wanamiliki majumba na magari ya kifahari yasiyolingana na vipato halali.
Nasikia kutokwa na machozi; wako wapi viongozi wazawa na wazalendo kwa nchi yao au tuseme walikuwepo tu wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.Watanzania tumebaki kama yatima tunanyanyaswa, tunadhulumiwa, tunaibiwa tukiona na tunapiga kelele na hakuna wa kutusaidia. Mawaziri na viongozi wetu wa sasa wamebaki watu wa kutaka sifa mbele ya wahisani, watu wa kujionyesha na wanaohisi lugha ya uzalendo aidha imepitwa na wakati na ni aibu kuitaja au inatakiwa itajwe katika mrengo wa kukipigania CCM ili waendelee kula nchi.
Nchi inatelekezwa na imekuwa mahame ya wageni na hata tunapoongea hivi wanatuona kama machizi. Lakini nakumbuka Baba wa taifa hakuwa tayari kuona nchi yake ikichezewa kama mdoli namna hii na alitetea kwa kiasi kikubwa heshima ya Tanzania na matokeo yake WAHISANI HAWA HAWA walimbatiza na kumwita DIKITETA. Bora dikteta anayependa watu wake na kuchukia wageni kuliko viongozi wanaojidai wema kwa wageni huku wakiwatoa kafara wananchi wao ili tu wageni wafurahi.