mbona nlkigoogle hiyo kampuni na huyo mmiliki wake napata taarifa tofauti,
Tanzania na hasa JK na Maige sijui kama wanaelewa lugha tunayo endelea kuitumia .Tumesha waeleza sana juu ua ujinga lakini wanasema tumesikia na yanaishia hapo hapo .Hawako serious na haya mambo na kweli kampuni nyingi ziko Ulaya na hawalipi kodi kabisa .Ndiyo tunavyo umizwa .TATO si huru kabisa .Wazungu wana honga mno kuwapata viongozi wanao wataka ili waendelee kula .Kuna uhalifu mwingi unafanywa kwenye utalii na serikali haiko pamoja nasi kabisa .Sijajua kigugumizi hiiki ni cha nini .
Sema uzuri chalii!mvumbuzi, you have nailed it................... unfortunately, what you said, may not be applicable in tiizii
Sasa mtu katoka majuu kuja tanzania kupata experince ya kitanzania kwa nini apewe tour guide wa kizungu.
But wahatver the case nadhani mtalii wa kweli anapenda akija apate tour gider wa sehemu asili hata kama anachapia lugha. Huo ndio utalii na ndio experince yenyewe ya utalii.
- Ina maana tour guide wetu hawana qualification au hawajafundishwa jinsi ya kuwahudumia watalii wa nje?
- Hospitality industry ya tanzania iko hoi ?
Siwezi kwenda kutalii UK nikafurahia kupewa tour guider mtanzania. Pamoja na kizungu changu cha kuunga unga nitataka nipate huyo huyo mzungu.
madini yashindikane kudhibiti ndio itakuwa utalii? na bado mtachonga sana mwaka huu
We unaongelea tour guide sasa hivi nyumba zingine Dar zina mahausigeli kutoka Ufilipino usiniulize wamepata wapi work permit.
Mvumbuzi,
Nashukuru sana kuwa umetoa angalizo kwa serikali juu ya kadhia hiyo, ili wafanye uchunguzi.
Kampuni hii naifahamu, maana kwa namna moja ama nyingine ofisi yangu ina udau na kampuni za Watalii.
Mara baada ya kusoma article ya Mvumbuzi nilifuatilia kwa jamaa wenye uhusika wa moja kwa moja na uendeshaji wake wakanipa maelezo yao.
Wanasema kwamba ni kweli wazungu wanafanya hiyo kazi ya tour-guide. Lakini wanasema kuwa kampuni hiyo ina namna tofauti ya operations kulinganisha na tour companies tulizozizowea hapa. Wazungu hao(tour-guides) wanatafuta watalii wenyewe katika nchi mbalimbali huko duniani na kuja nao huku, hivyo hawawezi kuwakabidhi kwa waswahili wawatembeze, wakati wao ndio wamebeba risk yote kuwasafirisha na kuwa 'care, na wanasema itakuwa si customer care nzuri, kitu ambacho kitawafanya wageni hao wasirudi tena kwa kampuni hiyo!
Kwa reasoning ya kawaida, sababu hiyo haitoshelezi kabisa kuwakosesha kazi tour guides wetu, zaidi sana ninachokiona mimi hapo ni aina ya ubaguzi wa rangi wa wazungu ambapo wanaona mswahili hataweza kutoa maelezo fasaha kwa mgeni!
Lakini hilo ni kosa la kiufundi. Tunafungua milango hadi ya vyumba vya siri kwa wageni.
Naungana na Mvumbuzi hizi ni kazi rahisi sana za waswahili wenzetu, hii ingekuwa sheria rahisi sana kuimplement dhidi yawatu hawa weupe, sielewi ugumu unatokea wapi.