Ezekiel Wenje ajibu mapigo ya Tundu Lissu na Godbless Lema, mazito yafichuliwa CHADEMA

Ezekiel Wenje ajibu mapigo ya Tundu Lissu na Godbless Lema, mazito yafichuliwa CHADEMA

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu

Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Victoria, ambaye pia ni Mtia Nia wa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Ezekiel Wenje, anazungumza muda huu na Waandishi wa Habari.

Aliyoyazungumza Ezekiel Wenje

"Marafiki zangu wote, Lissu, Lema, Heche, wote wamekiri kwa nyakati tofauti kwamba mimi nilikuwa timu Lissu. Hata leo nimemsikia Tundu Lissu akiwa Clouds akisema, 'Nilipoona watu wameanza kushughulikiwa, mimi nikapiga u-turn (360) nikakimbia.' Nimemsikia akisema, 'Sasa na uongo umekuwa mwingi sana."

"Nianze kwa kusema hivi, ni kweli mimi nilikuwa timu Tundu Lissu na kwanini nilitoka, mnakumbuka mimi nilikimbia nchi, Lema alikimbia nchi na hata Lissu alikimbia nchi, experience ya kukimbia nchi yako sio kitu kidogo kwamba unaenda kwenye nchi ambayo hujuia mila na destuli zao, una ancha ndugu na na marafiki zako, sio experience ndogo"

"Sasa tukiwa huko mambo yakaenda mengi mpaka Mwenyekiti Freeman Mbowe akakamatwa na kwenda gerezani, Mwenyekiti akiwa gerezani mwaka 2022, akiwa gerezani marafiki zangu hawa wakashauriana waanzishe kitu kinaitwa Join the Chain na Mwenyekiti aliyeasisi hiyo movement ni rafiki yangu Godbless Lema na Join the Chain lengo lake ilikuwa ikusanywe fedha liitishwe Baraza Kuu, na mwisho wake Mkutano Mkuu lengo kubwa la vikao tulivyofanya kwasababu waliamini kabisa kwamba Freeman Mbowe ana kesi ya Ugaidi, waliamini kabisa kwamba Mbowe hawezi kutoka gerezani"

"Ikaitishwa movement 'Join the Chain', ambayo Godbless Lema alikuwa Mwenyekiti ili waende wafanye mapinduzi kwenye chama, Tundu Lissu awe mwenyekiti wa Chama, Mchungaji Peter Msigwa awe Makamu. Miliposhirikishwa mambo kama haya mimi nilikataa uasi, na hiyo ndio chanzo cha mimi kujiondoa kwenye hiyo timu Lissu."

Soma, Pia:
 
Wakuu

Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Victoria, ambaye pia ni Mtia Nia wa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Ezekiel Wenje, anazungumza muda huu na Waandishi wa Habari.

Mwamba kaamua kupoteza muda tu. Sidhani kama anaweza kua na jambo la maana la kuongea. Na trust me hatavuta attention ya watu. Ni bad and wrong timing ya press... to prove that, tutaona humu humu kwa hii post, responses na reactions za watu..
 
CCM itatawala milele kama this is how “wapinzani” wanabehave. Watu wamekuwa duped kwa muda mrefu na sasa mambo yanawekwa hadharani

Lemma na yeye arudi tena kumaliza kumwaga mboga na kutoboa sufuria kabisa ili hii chama kipotee tu.
 
Back
Top Bottom