Ezekiel Wenje ajibu mapigo ya Tundu Lissu na Godbless Lema, mazito yafichuliwa CHADEMA

Ezekiel Wenje ajibu mapigo ya Tundu Lissu na Godbless Lema, mazito yafichuliwa CHADEMA

Napenda namna CDM wanavyopasuana, its good for democracy. CCM hawawezi hivi hata kidogo, labda kuwekeana šūmû na kumalizana kimya kimya.
Demokrasia sio kupasuana na kupakana matope yasiyo na ushahidi hakikika wowote

hiyo siasa na wala sio demokrasia ni uhumi wa mitaani

CCM hatuwezi iga huo ujinga wenu
 
Wakuu

Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Victoria, ambaye pia ni Mtia Nia wa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Ezekiel Wenje, anazungumza muda huu na Waandishi wa Habari.

Aliyoyazungumza Ezekiel Wenje

"Marafiki zangu wote, Lissu, Lema, Heche, wote wamekiri kwa nyakati tofauti kwamba mimi nilikuwa timu Lissu. Hata leo nimemsikia Tundu Lissu akiwa Clouds akisema, 'Nilipoona watu wameanza kushughulikiwa, mimi nikapiga u-turn (360) nikakimbia.' Nimemsikia akisema, 'Sasa na uongo umekuwa mwingi sana."

"Nianze kwa kusema hivi, ni kweli mimi nilikuwa timu Tundu Lissu na kwanini nilitoka, mnakumbuka mimi nilikimbia nchi, Lema alikimbia nchi na hata Lissu alikimbia nchi, experience ya kukimbia nchi yako sio kitu kidogo kwamba unaenda kwenye nchi ambayo hujuia mila na destuli zao, una ancha ndugu na na marafiki zako, sio experience ndogo"

"Sasa tukiwa huko mambo yakaenda mengi mpaka Mwenyekiti Freeman Mbowe akakamatwa na kwenda gerezani, Mwenyekiti akiwa gerezani mwaka 2022, akiwa gerezani marafiki zangu hawa wakashauriana waanzishe kitu kinaitwa Join the Chain na Mwenyekiti aliyeasisi hiyo movement ni rafiki yangu Godbless Lema na Join the Chain lengo lake ilikuwa ikusanywe fedha liitishwe Baraza Kuu, na mwisho wake Mkutano Mkuu lengo kubwa la vikao tulivyofanya kwasababu waliamini kabisa kwamba Freeman Mbowe ana kesi ya Ugaidi, waliamini kabisa kwamba Mbowe hawezi kutoka gerezani"

"Ikaitishwa movement 'Join the Chain', ambayo Godbless Lema alikuwa Mwenyekiti ili waende wafanye mapinduzi kwenye chama, Tundu Lissu awe mwenyekiti wa Chama, Mchungaji Peter Msigwa awe Makamu. Miliposhirikishwa mambo kama haya mimi nilikataa uasi, na hiyo ndio chanzo cha mimi kujiondoa kwenye hiyo timu Lissu."

Soma, Pia:

Kwa vile ilibidi aongee na yeye, basi tu ameongea, lakini hakuna hoja ya msingi inayoweza kumshawishi mtu kuamini maneno yake. Nadhani moyoni anajuta kwanini alijichanganya kwa Mwamba.
 
Sasa kama mtu (mwenyekiti) yupo gerezani, si lazima ateuliwe mwingine ashike nafasi ya UENYEKITI?

Chama kingebaki bila mwenyekiti hadi lini?

Kwani katiba yao inasemaje??
 
Heri uitishwe mdahalo "wachambane" kuliko hii kuita Press kila dakika!
 
Safi sana ,waroho wa madaraka lazima wachanwe ,mapinduzi ndani ya chama hayakubaliki...Lema/Lissu/Msigwa wangefuata utaratibu wa kugombea na si mikakati kama ya Zitto na Kitila.
Mapinduzi au utaratibu.
Kwa upa nde wangu hata kama ingekuwa kweli, ulikuwa uamuzi sahihi ili chama kisonge mbele.
 
Hata anavyoongea unaona kabisa ni mtunga maneno.
Katunga na kitabu cha Dr Slaa?Ambacho Dr Slaa anamuona Lissu kama mtu baki,mwongo,mnafiki,kiserela?Kasome kitabu hicho kwanza ndio mlete upupu hapa.

Vikarogosi havikuanza leo,Wenje kaonyesha mbichi na mbivu.
Mimi nilikuwa najiuliza kwanini timu Bush man haitaki sanduku la kura bali Mbowe ajiondoe yaani ajiuzulu kumbe wanataka kula bata bila kunawa!Wanafiki wakubwa akina pangu pakavu tia mchuzi.
Vita takatifu imewadia kuwaondoa na kuwaangamiza mapandikizi,ALLUTA continua.
Lissu is a looser.
 
Kuna siku moja hapo zamani za kale, Mwenyekiti wa CUF alisema hatagombea tena. Ghafla akaamua kugombea na kuleta taflani.
Maalimu na ujanja wake wote akasalimu amri. Mengine yabaki kwenye historia.
Naona kama yanatokea tena CDM. Muda utathibitisha, anyway, kama nimejidanganya mwenyewe au ndio mambo yalivyo
 
Chadema wameamua kuteka media na wameweza.
Chadema true color identity exposed.
Wapo cream wanaojua hesabu za viboma kwamba upinzani unahitaji maarifa na sio kelele tu.

Wapo wanaona kila kitu ni sawa ikiwa kuna kinachoingia kinywani.

Wapo wanafiki,wanajiita Chadema damu kume wanapanga mapinduzi ndani ya chama.
 
Huyu project ya serikali anazidi kumuingiza Mbowe matatani kwa vile ameyataka mwenyewe basi sisi tunamalizia,hapa chini Mbowe anaonekana akikusanya hela ya join the chain ili ajipindue
 

Attachments

  • FB_IMG_1737030202896.jpg
    FB_IMG_1737030202896.jpg
    57.1 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1737030098799.jpg
    FB_IMG_1737030098799.jpg
    54.2 KB · Views: 2
Wenje anatapa tapa, Join the chain ni kampeni ambayo Mbowe ameshiriki kikamilifu, kwahiyo kama anasema kampeni hiyo ililenga kumpindua Mbowe , je, Mbowe inawezekana vipi alitaka kujipindua mwenyewe !?
 
Back
Top Bottom