F.T: NBC Premier League | Simba SC 3 - 0 Biashara United | Uwanja wa Benjamin Mkapa

F.T: NBC Premier League | Simba SC 3 - 0 Biashara United | Uwanja wa Benjamin Mkapa

Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC) Premier League kuendelea kuvurumishwa leo March 4, 2022 ambapo kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera Sugar wanakipiga na Namungo FC, saa 10: 00 Jioni, huku wakali wa CAF, Mnyama Mkali Mwituni, Simba SC wakikipiga na Biashara United kutoka mkoani Mara katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo wa Simba SC dhidi ya Biashara United unatarajiwa kuwa mkali na kusisimua hasa ukizingatia timu zote mbili kihitaji alama tatu muhimu.

Kocha wa Simba SC Pablo Franco, amesema kuwa mchezo utakuwa mgumu, Biashara United ni nzuri na ina wachezaji wazuri mmoja mmoja hata hivyo tunahitaji kushinda ili kupunguza idadi ya alama na anayeongoza, hivyo tunategemea ushindi.

Kwa upande wa Kocha wa Biashara United Vivier Bahati, amesema Tunaimani kwamba Mchezo utakuwa nzuri, na tutapata matokeo mazuri, tukitazama maandalizi yetu yapo vizuri.

Mara ya mwisho kukutana, Simba SC waliibuka kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Biashara United. Je? Nani kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo, dakika 90 za mchezo kuamua. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00 Usiku. Usikose Ukaambiwa.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

....... Ghazwat.....


Naaam mpira umeanza uwanja wa Benjamin Mkapa.

00' Mpira umeanza kwa kasi huku Biashara United wakifanya jaribio la kwanza.

05' Umiliki wa Simba SC sasa huku lakini Biashara United wanazuia maridadi kabisa.

08' Sakho Goooooooooooooaaal gooal

Pape Sakho anaipatia Simba SC bao la kwanza kwa shuti kali akipokea pasi kutoka kwa Kapombe | Simba SC 1-0 Biashara United.

10' Biashara United alianza vizuri lakini sasa kasi yao inapungua sijui kwanini.

13' Mzamur Goooooooooooooaaal gooal
Mzamur Yasin akipokea pasi kutoka kwa Kapombe | Simba SC 2-0 Biashara United

Biashara United wanazidiwa hapa Uwanja wa Benjamin Mkapa. Haya wanakwenda Simba kutafuta bao la tatu, kwake Sahkooo anampasia chamaaaa

18' Chamaaaa Goooooooooooooaaal gooal

Chama anaipatia Simba SC bao la tatu kazi bomba kutoka kwa Sahko | Simba SC 3-0 Biashara United

Mpira unachezea katikati ya Uwanja huku Umeliki ukiwa kwa Simba, Biashara wanautafuta kwa tochi

25' Biashara wameamka wapeleka mashambulizi upande wa Simba SC walau sasa wanaamka.

30' Ametoka Kapombe baada kugongana mchezaji wa Biashara United hivyo kuumia na ameingia Patrick upande wa Simba SC.

35' Mkwaju wa mchezaji wa Biashara unatoka nje ya lango | Simba SC 3-0 Biashara United
Duka.
 
Siwezi amini jinsi Utopolo walivyotawanyika kwenye Uzi huu....!
Na Bado Utopolo mtaadimika Sana Kwenye nyuzi Kama hizi..!
 
Back
Top Bottom