Facebook ya sasa imejaa matapeli, madanga na waganga wa kienyeji tu

Facebook ya sasa imejaa matapeli, madanga na waganga wa kienyeji tu

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Facebook ya miaka ya 2015 rudi nyuma ilikua tofauti sana na ya sasa. Kwa sasa watumiaji wengi wa facebook ni

1. Matapeli wa mtandao (crypto & investments)
2. Waganga wa kienyeji wapo wengi lakini (west Afrika sana)
3. Wadangaji fake (Wabongo sana)
4. Watu wenye uelewa mdogo (hasa Wabongo)
Sioni faida ya Facebook tena, siku 7 tu toka niingie nimechati na waganga zaidi 200, matapeli zaidi ta 100 (wengi wa SA), madanga zaidi ya 50.

Yani mpaka sasa sioni mtu anaeongea cha maana tofauti na marafiki wachache ninaojuana nao au mashirika ya habari tu.

Unaipendea nini facebook?
 
Nadhani uzuri na ubaya wa kitu uanza na mtazamo, ushawishi na matumizi. Unajuaji kama matapeli, waganga na makahaba? Tuongozane.

Ukitumia Facebook for personal matter na integrity ya positivity hutokutana na hayo masuala na hata ukiyaona utadelay na kuyapoteza.

Uki-Request na Ku-Accept marafiki/profiles za watu usiowafahamu ni unattract kuingiliwa na hao. Yes unaweza request watu au accept lakini pitia profile kuhakiki ni watu chanya?

Unaweza kulalamika katika hili wakati mhusika anao marafiki 4782! Kweli kiuhalisia unao hao marafiki? Utaona mhusika ana group's za kila niche (Udalali, Ngono, Mahusiano, Bidhaa, Michezo nk). Unategemea mhusika asikutane na tapeli featuring malaya?

Binafsi Facebook nina marafiki 236 wote hawa nawafahamu, wananifahamu na tuna-associate katika masuala mbali mbali. Nina makundi mawili 1. Kampuni ninayo-associate nayo 2. Taasisi niliyowahi kuhisika nayo.

Same Instagram nimewafuata watu tunaofahamiana, niliowahi kuwafanyia shughuli au ninaowahusudu na ni wenye positivity.

Sijawahi kuona tapeli, kahaba, malaya wala mganga akikatisha.
 
Hizo ndo interest zako ndo maana unakutana na watu wa aina hiyo.

Kuna watu wanauza na kununua bidhaa fb kwenye FB Market.

Kuna watu wanatangaza biashara zao legit kabisa huko huko fb.

Kuna watu bado wanawasiliana na ndugu na jamaa kupitia fb na si Whatsapp au mitandano mingine.

USA, wamarekani wenyewe hawaijui au kutumia kabisa mitandao mengine zaidi ya fb.

Hapo ni dhahiri interest zako zipo kwa waganga, matapeli na madanga ndo maana umewafollow na kufanya mawasiliano nao kabisa.
 
We mganga au mdangaji?
Wewe huenda ukawa ni mmoja Kati ya Hao watu unao waita wenye uelewa mdogo Facebook unatakiwa ujue Facebook inabiashara nyingi kubwa kubwa kuliko mitandao yote Dunian
 
Hayo Mambo naona kila mtandao yapo..kidogo Twitter naona Kuna ahueni
 
Nadhani uzuri na ubaya wa kitu uanza na mtazamo, ushawishi na matumizi. Unajuaji kama matapeli, waganga na makahaba? Tuongozane....
Nilituma request nyingi ili nibadili acc juwa page sasa yamenikuta hayo
 
Kupitia Facebook naingiza Milion 3kwa mwezi Sasa wewe endelea kubeza
Mkuu lengo langu lilikuwa ni kuingiza pesa kupitia huo mtandao,sasa page yangu haikui nikashauriwa nitumie account ya kawaida (personal account) niwe na marafiki 5k kisha nibadili kuwa page,sasa naona mapicha picha tu. Nipe conection boss
 
Naingiza hela kwenye Facebook kwa groups na page pia naitaji watu smart hata kama ni wachache pia sio kwamba hela inaingia Facebook kwa sababu Nina page tu na group hapana Kuna jambo lingine unatakiwa ufanye nalo ni lazima ue na Biashara mkuu Facebook Kuna Biashara nyingi Sana Sema wewe ulipo jiunga Facebook ulianza kuwatafuta ndugu zako na Baadh ya master fake wa Facebook ndiomana unakumbana na io Hali

Mimi kwa mwezi nailipa Facebook shilingi 128000za kulipia Adds za matangazo yangu na kutafuta watu wa eneo husika ninalo li target
 
Tupe connection kaka
 
Back
Top Bottom