Nadhani uzuri na ubaya wa kitu uanza na mtazamo, ushawishi na matumizi. Unajuaji kama matapeli, waganga na makahaba? Tuongozane.
Ukitumia Facebook for personal matter na integrity ya positivity hutokutana na hayo masuala na hata ukiyaona utadelay na kuyapoteza.
Uki-Request na Ku-Accept marafiki/profiles za watu usiowafahamu ni unattract kuingiliwa na hao. Yes unaweza request watu au accept lakini pitia profile kuhakiki ni watu chanya?
Unaweza kulalamika katika hili wakati mhusika anao marafiki 4782! Kweli kiuhalisia unao hao marafiki? Utaona mhusika ana group's za kila niche (Udalali, Ngono, Mahusiano, Bidhaa, Michezo nk). Unategemea mhusika asikutane na tapeli featuring malaya?
Binafsi Facebook nina marafiki 236 wote hawa nawafahamu, wananifahamu na tuna-associate katika masuala mbali mbali. Nina makundi mawili 1. Kampuni ninayo-associate nayo 2. Taasisi niliyowahi kuhisika nayo.
Same Instagram nimewafuata watu tunaofahamiana, niliowahi kuwafanyia shughuli au ninaowahusudu na ni wenye positivity.
Sijawahi kuona tapeli, kahaba, malaya wala mganga akikatisha.