Siku chache zilizopita mwanamuziki maarufu wa miondoko yakufokafoka almaarufu Roma mkatoliki aliripotiwa kutekwa na watu wasiojulikana katika studio za Tongwe record zinazomilikiwa na kijana jina maarufu (J mada),inasemekana ilikuwa ni majira ya usiku wavamisi walipowasili katika viunga vya ilipo studio hizo.
Kulingana na maelezo yaushaidi uliotolewa na shuhuda (the city) mwanadada aliyefika muda mchache kabla gari lawatekaji kuondoka alisema "ilikuja Noah nyeupe na wakashuka watu watatu,baada ya hapo wakatuamrisha mimi,bin Laden na wageni kutoka morogoro tuingie ndani ya geti,tulipoingia ndani ya geti walituuliza kwamba tumemkuta junior au tumemkuta Roma,tukasema junior hayupo ila Roma yupo ndani,wakatuamrisha Tukamuite Roma,tukamuita Roma,Roma akatoka akaulizwa wewe ndio ROMA na ilivyoonekana hawakumjua na pia walimuambia simu yake ipo wapi atokenayo Roma alitokanao sikuweza kujua nini kiliendelea kwa sababu waliongelea nnje ya gari,walirudi ndani wakamlazimisha binladen aingie studio akiwa amesindikizwa na mmoja wao na Wakarudi tena wakachukua TV zilizopo pale,wakatoka na imma walikuwepo wote ndani ya studio,studio ikabaki tupu,walivyotoka hapo wakaniambia mimi na wageni wengine waliotoka morogoro tusiende popote na nilichosikia baada ya hapo ni mshindo wa gari na gari kuondoka "
Fact:katika ushahidi wa shuhuda (the city) umejidadavua watekaji hawakuwa na haiba yautekaji kwani kiwango Chao cha ustaarabu kilikuwa juu sana ukilinganisha na watekaji wengine tunaowasikia na hata kuwashuhudia.
Hoja ya kwanza (1):watekaji waliuliza tumemkuta Roma na wakatuambia tukamuite?? Niajabu kwa mtekaji kuwa na nidhamu ya namna hii, mara nyingi hutumia nguvu kuhakikisha wanatimiza lengo Lao,mtekaji gani huyu anaogopa kuingia ndani anawaambia mashuhuda nendeni mkamuite Roma ??
Hoja ya pili (2):watekaji wakamuuliza Roma,wewe ndio Roma.sikawaida kwa msanii maarufu kama Roma ashindwe kujulikana tena na hawa watekaji ambao kwa asilimia kubwa huenda wakawa ni vijana,tena vijana hawa ndio wapenzi namba moja wa mziki huu wakufokafoka unaoimbwa na Roma ni wazi na sio rahisi kutokumfahamu Roma.
Hoja ya Tatu (3):watekaji wakaingia ndani na binladen,picha tunayoipata hapa bado watekaji walikuwa na ustaarabu napo hawakutaka kuingia studio wenyewe bado waliitaji mtu mwenyeji waingie nae ndani, wavamizi wengi hutumia nguvu na wakati mwingine huwa hawajali Mali ya waliodhamiria kumteka hawa waliomteka Roma watofauti sana.viashiria hivi vya ushahidi wa( the city)unatuonyesha wazi kunamaslahi binafsi yakisanà na wala siutekaji kama unavyoripotiwa..
Hoja ya 4.watekaji wakatuambia tusiondoke.watekaji baada yakuwachukua wahusika wakuu waliwaamuru the city na wenzake wasiondoke hii inamaana bado walitaka kuhakikisha usalama wa studio unakuwa salama hivyo walionyesha kujali na kudhamini Mali na vifaa vinginee vya studio. hali isiyo ya kawaida mtekaji kuhakikisha ulizi wa Mali za mtekwaji.
Upande wa mmiliki wa Tongwe record :nae mmiliki wa Tongwe record aliskika akiongea akisema "usiku wa jana likitokea tukio lakutisha sana,walikuja watu ambao hawakufaamika wametoka wapi au wametumwa na nani,bahati nzuri mimi si kuwepo studio,wakamuhoji ROMA baada ya kumuhoji Roma wakamuhoji na monie ambaye ni msanii wangu pia kutoka Tongwe record baada yakumaliza mahojiano yao wakaingia ndani studio wakachukua TV, computer pamoja na kamera"
Maelezo ya mmiliki wa studio na shuhuda namba moja hayatofautiani sana bado yote yanaukakasi wa kiwango cha ustaarabu wa hawa watekaji.
Hoja watekaji walimuhoji ROMA.ni tanzania pekee watekaji hupata muda wakuhoji mtekwaji,sidhani kama inaingia akilini kuskia mtekaji anaweza kufanya interview na mtekwaji,nguvu na ubabe huwa hawana muda wa kuwa wakarimu na kuchukua maelezo mara zote watekaji hawana huo muda,ili lililotokea kwa Roma ni maigizo yenye maslahi binafsi.
Kauli ya mkuu wa mkoa mh.Paul makonda.mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa mkoa ni haki na wajibu wake kuhakikisha mkoa unakuwa salama pamoja na Raia wake,ni haki na sahihi mkuu wa mkoa kuingilia kati upotevu wa watu wake.
Mh.Makonda aliskika akisema "bado tunayomamlaka yakudhibiti kila aina ya utekaji na kuhakikisha wanannchi wetu wanaendelea kuwa salama,sambamba na hilo nawapa imani tu haitafika jumapili tutakuwa tumeshawapata ndugu zetu wote wanne na mimi naomba kwa dini zetu kwa imani zetu kila mmoja kokote kule alipo aombe ili tuhakikishe ndugu zetu tunawarejesha wakiwa salama.
Kutokana na kauli ya mh Paul makonda imepelekea watanzania kijuiliza maswali kadhaa.
Hoja ya kwanza (1).kauli ya haitafika jumapili Roma na wenzake watakuwa wamepatikana.Niwazi kauli hii ni Tata na ilikuwa na viashiria vya huenda kuna Jambo muheshimiwa alikuwa analifahamu zaid, tena ukizingatia huwa anaukaribu na vijana hawa wanaofanya sanaa,nikweli jumapili hajafika na vijana wamepatikana,mh ni kijana anajua mbinu nyingi za vijana wenzake wanazotumia kujipatia umaarufu nadhani alishashtukia na akatoa kauli iliyojipambanua kuna kitu anafahamu.
Hoja ya pili (2).kauli yakuwarejesha Roma na wenzake wakiwa salama nayo ni moja ya kauli iliyotolewa na mh mkuu wa mkoa tutawarejesha wakiwa salama kauli hii nayo iliashiria mchezo mzima huenda mkuu wa mkoa alikuwa anajua mahali alipo mkatoliki.
Uchambuzi wa kauli ya mhusika mkuu (Roma).Roma mara baada yakupatikana alipelekwa kituo cha Polisi ambapo naamini aliacha maelezo yakutosha.
Roma aliskika akisema " kutokana na mazingira na situation nzima hatutakuwa na muda mrefu wakuzungumza, kwakifupi tu niwaakikishie mimi ni mzima mpaka Sa hivi kiafya na kiakili hata monie,bin LadenI wote tuwazima wa afya,niwaakikishie sisi wote ni wazima tunaendelea vizuri"
Hoja ya kwanza (1).nifuraha kuskia wapo salama ila yapo maswali ya kujiuliza nini hasa lengo la watekaji je ni kweli watu hawa walitekwa? ni kweli mtekaji anaweza kuwateka wasipigwe hata vibao kimoja kiasi cha kuachiwa wakiwa 100% sawa bila jeraha na hata mkwaruzo wowote?
Hoja namba mbili (2).mavazi ya Roma siku anatekwa na siku anaonekana,siku anatekwa Roma aliripotiwa kuwa alikuwa amevaa t shirt nyeupe suruali ya blue aina ya Jinsi, ila siku anapatikana alionekana akiwa na mavazi meusi .Niwazi uko alikokuwepo alipata fursa ya kupata huduma muhimu kama kuoga na hata kubadilisha nguo bado kuna ulakini wa aina hii ya utekaji,sio rahisi kwa watekaji kuwa na moyo wa namna hii vijana wasanaa inaonekana walikuwa bado katika mwendelezo wa sanaa yao,haingii akilini aina hii yautekwaji kwakweli.
My take.tusishangae na kuskia nyimbo mpya ya Roma katika kipindi cha mwezi mmoja kutoka sasa,attention aliyokusudia kuipata amefanikiwa kwa 100% otherwise kesho siku ya jumatatu atuambie wa Tanzania hoja nzito kutuakikishia ni kweli alitekwa na sio kutafuta umaarufu kisanaa.
Kamanda Sirro Azungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Sakata la Msanii Roma
MPEKUZI / 2 days ago
[
https://4]
Msanii wa hip hop Roma Mkatoliki alikamatwa April 5 usiku ambapo taarifa zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kuwa alikamatwa studio za Tongwe Records na watu wasiojulikana akiwa na wenzake na wakapelekwa kusikojulikana.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo asubuhi kuhusukutekwa kwa msanii huyo na wenzake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema kuwa hawezi kusema ni lini wasanii hao watapatikana kwani ni hadi pale upelelezi wanaouendesha utakapokamilika.
Sirro alikuwa akijibu swali la mwandishi wa habari aliyekuwa akiuliza kuhusu lini wasanii watapatikana kufuatia kauli ya Mkuu wa Mkoa aliyoitoa jana kuwa hadi Jumapili wasanii hao watakuwa wamepatikana.
==>Haya ni mambo machache aliyoyazungumza
“Matukio ya utekaji hayajaanza leo, yamekuwepo na tukafanyakazi tukapata majibu. Tukio hili la kutekwa wasanii ni la kawaida.
“Tukio hili la utekaji ni kama matukio mengine ya uhalifu ambayo tumeyashungulikia, hatuwezi kusema hali mbaya kwa tukio hili.
“Mimi ni Kamishna wa Polisi siwezi kusema wasanii watapatikana lini, kama kuna kiongozi alitaja siku watakayopatikana, muulizeni yeye.
“Upelelezi ndio utakao amua hawa watu watapatikana lini. Tunafanya kazi kufuata taaluma ni si kutoa maneno tu.
“Wanaosema simu ya Roma ilikuwa inapatikana na kuhoji kwanini hatukwenda TCRA, wasitufundishe kazi, wamejuaje hatukwenda TCRA?
“Wengine walalamika wasema leo ni siku ya tatu tumechelewa kutoa majibu walipo, wajue majibu ya polisi kuuawa tulipata baada ya mwezi mmoja.
“Hawa watu hawakuja kuniambia kuwa Kamishna Sirro sasa tunakwenda kuwateka, kwamba ninajua walipo lakini sitaki kuwakamata."
==>
FANANISHA NA HII PIA YA MAKONDA KISHA UTWAMBIE NANI KAKUTUMA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda Aahid Msanii Roma Atapatikana Kabla ya Jumapili Hii
MPEKUZI / 2 days ago
[
https://2]
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, ameahidi Roma Mkatoliki, Moni pamoja na wengine wawili watapatikana Jumapili hii baada ya wasanii hao kutekwa na watu wasiojulikana Jumatano hii wakiwa Tongwe Record.
Alisema hayo jana akiwa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam, muda mchache baada ya kutembelewa na wasanii ambao walimtaka mkuu huyo kuwasaidia kupatikana kwa wasanii hao.
Akiongea na waandishi mbele ya wasanii hao, RC Makonda alisema kila mtanzania ana nafasi ya kumtafuta Roma na wenzake kwa kuwa hakuna anayejua watu hao wako wapi.
“Natoa pole kwa ndugu pamoja na marafiki, hakuna mtu ambaye anaweza kupotelewa na mtu akawa na furaha na bahati mbaya tunahangaika kujua wapi waliko. Nitumie fursa hii kuwaambia wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kwamba tunapopotelewa na ndugu zetu katika mazingira ambayo hatuyafahamu sio wakati ya kuyarusha rusha maneno na kufika hatua tunapoteza ushahidi,” alisema RC Makonda.
Alisema tayari ameliagiza jeshi la polisi kufuatia suala hilo kwa ukaribu zaidi ili kupata ufumbuzi mapema huku akiahidi mpaka Jumapili hii watu wao watakuwa wamepatikana.