Mkuu MSEZA-MKULU, Kwanza pole sana kwa juhudi kubwa unayoifanya ya kuelimisha na kutangaza kwa nguvu zote jinsi ya biblia inavoshabiana na Science kwa ujumla wake.
Katika watu waliojitahidi kitendea haki thread zao nawewe unaongoza. . Na kwa kweli umeiva kwenye mada uliyoiweka.
Mimi naomba nianze kwa kusema inaonekana unaijua sana historia ya mambo ya kale ki-Biblia na ki-Sayansi kwa uzuri kabisa hapa ninakisifu na kwa kweli umeiva. Ila kujua hizo historia kwa sana haikufanyi ukawa na ushawishi au nguvu ya hoja wa kuwateka the so called MATERIALIST , shida uliyonayo ni kuwa unaeleza historia nyingi ambazo at the end unajichanganya na kumpoteza mbwa kwa miluzi mingi-----na ndio maana pamoja na kujenga hoja nyingi sana hujaweza washawishi wengi humu kufuata unachokizungumza/kukiamini maana hoja zako hazina mashiko.
Kwanin nasema hazina mashiko:
Mosi; Unachanganya mambo sana, mfano wadau wengi wanakuasa kuwa biblia inazungumzia (imani) wakati sayansi inazungumzia (facts) hii ni sawa na maji na mafuta. Huu ni ukweli wa wazi kabisa unaotakiwa kuukubali.
Pili; Ni kweli kama unavosema kuwa biblia imejaa ilmu mbalimbali ila wewe umeamua ku-site areas zinazohusu masuala ya kisayansi, hatukatai upo sawa tu maana kiukweli Bible ni kapu lenye kila aina ya maarifa kinachotakiwa ni jinsi mtu anavyoitumia anachukua kipi na kipi anakiacha. Ila unapokosea ni pale unapotulazimisha tuamini kuwa bible in its general inasupport sayansi, kitu ambacho si kweli---maana yapo maeneo kibao bible ina criticise sayansi kabisa na kuna sehemu inaenda beyond sayansi hasa kwenye masuala ya miujiza. Sasa kitabu kama hichi huwezi ukatoa a general statement kuwa eti kinasupport sayansi 100% na kitumike ktk maswala ya kisayansi as a reference maana kitachanganya watu hasa pale watakapokutana na mistari inayopinga sayansi humohumo. WEWE ULITAKIWA USIONESHE MAPENZI MAKUBWA NA YA KU-GENERALIZE KUWA BIBLE NA SAYANSI VINAOANA KWA UJUMLA WAKE. Kwa maana ukisema hivo unaleta contradiction kama nilivoeleza hapo.
Tatu; Unatakiwa utambue kuwa si kwa sababu wewe unaamini jambo fulani bac ukaona we ndio mueleeewa kuliko wengine , nimefurahi ulivyonanwa na mdau mmoja hapo juu ukakiri kuwa wachina, wajapani na hata mataifa & makabila mengine yameweza kufanikiwa sana tena sana kwa maarifa na skills nje ya biblia unayoiamini wewe, hapa ndio unatakiwa ufahamu kuwa knowledge is beyond very far beyond what you believe as MSAZE MKULU . Ni hivi yapo maarifa mengi sana yanaelea hewani na yapo pande zote kinachotakiwa ni mtu kuwa na vision kali na kutuliza mind yako ili uya-capture . Hili linathibitishwa kupitia wanasayansi wengi ambao kama tulivoona hapo kabla kuwa walikuwa christian ila baada ya kuzidi ku-crack vichwa waliamua kuachana na ukristo na either kuwa wapagan au kuhamia pande nyingine ya imani, ila hiyo haikuwafanya kushindwa kifanikiwa , matokeo yake walifanikiwa sana tena sana. Hivyo maarifa yapo everywhere the matter is how to capture them. Hivyo unvyong'ang'ania biblia ndio kila kitu unakosea maana si kweli , bali biblia wengi wanaichukua kama reference ktk kakipengele flan tu na anaendelea na theory zake nyingine, sasa wewe ukiona amesite kamfano kamoja unawehuka kisema biblia yote ni kisima cha sayansi hapo unakosea, hamna kitu kama hicho. (hapa unadhihirisha unavoweka mapenzi mbele badala ya logic) usihubiri we weka fact zitajitetea zenyewe.
NOTE:
Biblia ni kweli unaweza itumia kama unavosema ikakupanua kiakili katika areas flan flan ila pia biblia hiyohyo unaweza itumia ikakupumbaza jumla ktk mambo flanflan.
(AKILI KUMKICHWA)
Wanasayansi pia mkuu ni kama kokoro(nyavu zilizobeba kila aina ya kiumbe maji/si-viumbe samaki watamu,nyoka,kaa,mawe,mayai, mamba watoto kenge na uchafu wa zaiwani). Kuna wanaomwamini Mungu, Kuna wasiojua chochote kuhusu Mungu, Kuna wanaujua ukweli kuhusu Mungu ila wanatafuta kuprove wrong mambo yake, Kuna wasiotaka kujua chochote nje ya Scientific evidence lkn wote wanakutana kwenye critical juncture ambayo ni kweli kwa Wanaimani vyote wanavyochunguza ni creative work of the lord.
Mosi:Bibilia imezungumzia imani ni kweli, Kuna ubaya gani kama kitu cha kwenye bibilia kilichopokelewa kwa imani, Akaja mwanasayansi kwa kujua au kutokujua akakidhibitisha ndivyo kilivyo. Mzizi na Msingi wa bibilia ni kuwa hakuna kitu kilichotokea by Chance. Vyote ni creative work of Biblical God.Sasa kama unamwamini au humwamili lakini unachunguza uhalisia wa kazi zake na majibu yakawa sambamba na kauli zake zilizoaminiwa kwa imani sioni shida hapo mkuu.
Pili;
Umeeleza vizuri mkuu na kiungwana pia. Maelezo yako ni kweli lkn pia wenda hujanielewa au mimi ndio sijaeleweka. Ninaweza kesho kuandika post kuwa bibilia ni SOURCE ya ECONOMICS maana Hata Founder wa modern economy Adam Smith aliwahi kuconvince bunge kukubaliana na Essay yake maana alicement hoja zake kwa kutumia Biblical principles za Kitabu cha Genesis. Haimaanishi bibilia nzima ni Economics. Nakubaliana na wewe kuwa bibilia ni Multknowledge source ila contradictions kwa Mwanasayansi anayeiamini haziwezi kutokea maana atakuwa na mental capacity kwanza ya kujua Mungu ana Infinity ability mwenye uwezo beyond scientific limitations. Atalewa Shoka ilipoelea,Yesu kupaa(Breaking g influence), Spiritual Dimension, Fimbo kuwa nyoka,Mtu kupotea Dar na kuibukia Mwanza in microsecond time,Yesu kutembea juu ya maji etc ni beyond sayansi. Kwa hawa ambao hawataki kumwamini Mungu wala Spiritual dimension bado wanaweza kuwa na fursa ya kuchimba kwnye hii Multimineral Mine, Mwanasayansi kama huyu ndiye mwenye uwezekano wa Kukutana na Contradictions. Ila anaweza kushauriwa ajikite kwenye investigation ya outputs of creation. Mfano what makes life possible on earth anauwezekano akagundua tens of forces and constants ambazo zinafanya maisha yawe possible duniani na sio jupiter and use the same principle to scientifically investigate mars. What force/power is behind cooperation of ants. Atagundua kuna special cooperative cognitive sensors ambazo zinawafanya wawe karibu, Pia atagundua kuna kiogozi wenda anaexcrete hormony inayowafanya wenzake wafuate anachoamuru japo haongei. Kumbe basi wanaweza kuja na prototype ya uwezekano wa wanadamu kufanya kazi kwenye kelele bila distraction. Kwa ufupi kuna tens of research titles around the creative work of God and his word BIBLE.
Tatu
Nakubaliana na wewe mkuu sijui kila kitu ila changAMoto ikitolewa lazima tuchakate hadi mtoa changamoto atoe basis zote za argument yake ikiwezekana kiini cha changamoto na supportive facts ili kuwa na mutual exchange of knowledge, Wenda akanishawishi kwa hoja au mimi nikamshawishi au tukakubaliana kutokukubaliana ila mwisho wa siku product ni Desire for more learning, Modification of faith,new knowledges, List of unanswered questions that needs deep research. Kwa mfano mimi vitabu nilivyopanga kusoma mwaka huu vingi sikuvisoma nikaishia kujikita kwenye majibu ya changamoto mpya ninazozipata katika mijadala na kusoma maMbo ya huko. Unapohoji na kukomaa kwenye kile unachokiamini huku ukiutaka upande wa pili ulete changamoto zaidi unaonekana mjuaji,mdini, mbishi, kichwa ngumu etc.
Mwisho
Nashukuru kwa changamoto ulizoteoa maana kwangu zinanifanya kuwa tofauti na yule wa jana maana ninarefine nilichojifunza na ninachoamini. Hata mimi ninaamini Kuna mamilioni ya maarifa nje ya bibilia ila kila ilmu iliyo nje ya bibilia lazima ikutana na elimu ya bibilia kwenye angle flani hata kama ni angle ndoogo sana vinginevyo elimu hiyo lazima iangaliwe kwa umakini zaidi nini kusudio nje ya elimu yenyewe Wenda ikawa ni upinzani wabibilia usio na mashiko kwa jina la sayansi au utafiti kama ilivyo evolution.
Asante sana, Nakosoleka na nakubali changamoto katika maelezo yangu wenda yakaongeza au kusawazisha ukakasi uliojitokeza