MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,763
- 5,607
- Thread starter
- #281
maadam nampata yuko weak sana kusimama yeye na kuwa tayari kusimamia vitu vyake. Ndio maana nimemwambia yeye anawezekana kuwa yule jamaa jukwaa la dini anajiita gavana attribute zao zinafanana kabisa Bilia links,copypaste,fulani kasema, nilisikia flani anasema, hawana cha kujadili.Madam anataka sisi tumtajie anachokifikiria yeye,hii ni ajabu sana..
Yaani analeta madai halafu anataka wengine wamuoneshe madai yake yalipo utadhani tunakubaliana na hadithi zake...
Lakini huyu nishajadili naye mambo mengi najua namna yake ya kujadili mambo,hana uwezo wa kusoma kitu halafu akaleta maelezo alivyoelewa bali anakuwekea link uende huko ukasome halafu anataka uelewe kama alivyoelewa yeye ili uone anachokisema ni kweli wakati hajui unaweza ukasoma halafu ukatofautiana naye....
Kile anachopaswa kukisema hapa hawezi manaa kitamfunga....
Kitu ambacho anapaswa kujua ni kwamba Mnaweza kuwa wakristo wote lakini mkapishana kwenye imani baadhi ya vitu sio ugomvi wala dhambi jadili na mtu kwa kadili ya mlengo na uelewa au mada iliyopo mezani. Kunaweza kuwa na wakristo mia kila mtu analake. Sio unajadili hiki mtu anaruka papa mbona anasema hivi na hivi.
Kama bado anatabia hizo za kuandikiwa vitini na kuja kupaste humu bila kutumia akili yake hiyo nitamuachia afanye mwenyewe. Kuna waislamu wasomi wanajua kujadili vitu kwa hoja point baada ya point ukikosea anakukosoa akikifeli anakubali lakini hapa mama yeye anakomaa bila hata kufikiri kidogo, Sijui hiyo elimu yake ambayo aliielezea siku moja anaitumia wapi maana ikifika huku huwa anakuwa mtupu sana.
Binafsi huwa sioni tabu hata kutofautiana na dunia nzima, au wakristo wote au watu ambao wanaamini ninachoamini na ili twende sawa tushawishiane kwa hoja na kama zinamashiko nakubali ndio maana leo tunaweza kupatana katika hili kesho tukatofautiana na lingine. Lazima tutendee haki uhuru tuliopewa na Mungu kiakili katika kupambanua mambo.