Facts za kushangaza kuhusu satellites zinazozunguka dunia hivi sasa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Watu wengi wakisikia satellite wanafikiria ni vifaa vichache tu vinavyozunguka dunia, lakini ukweli ni kwamba anga la karibu na dunia limejaa vitu vingi sana kuliko watu wanavyodhani. Kuna maelfu ya satellites zilizotumwa na nchi mbalimbali, makampuni binafsi, jeshi, vyuo vikuu na taasisi za utafiti. Lakini si zote bado zinafanya kazi.

Kwa makadirio ya sasa ya mwaka 2026, kuna zaidi ya satellites 14,000 hadi 15,000 zinazofanya kazi angani zinazozunguka dunia. Ukijumlisha satellites zilizokufa, mabaki ya rocket, na space debris, jumla ya vitu vinavyofuatiliwa angani vinafika zaidi ya 33,000.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba miaka michache iliyopita idadi ilikuwa ndogo sana. Mwaka 2019 kulikuwa na karibu satellites 2,000 tu zinazofanya kazi, lakini sasa zimeongezeka mara kadhaa kutokana na kampuni binafsi kuingia kwenye space race.

Baadhi ya satellites zimeharibika, zimepoteza mafuta, au teknolojia yake imepitwa na wakati. Tatizo ni kwamba hata zikifa hazidondoki moja kwa moja duniani. Zinaendelea kuzunguka angani kwa miaka mingi sana zikiwa kama “magari yaliyoharibika barabarani” lakini kwenye space. Hizi ndizo huitwa “space junk” au uchafu wa angani.

Kinachofanya jambo hili kuwa la kutisha ni kasi yake. Hata satellite iliyokufa inaweza kusafiri kwa zaidi ya kilomita 27,000 kwa saa. Hiyo ni kasi kubwa mno kiasi kwamba kipande kidogo tu cha chuma kinaweza kuharibu satellite nyingine kabisa kikigongana nayo. Kwenye space hakuna breki wala hewa ya kupunguza mwendo, hivyo vitu vinaendelea kukimbia kwa kasi kali sana.

Mfano wa kutisha ni pale satellite au rocket ikilipuka au kugongana. Vipande vyake vinaweza kuwa maelfu ya vipande vidogo vinavyoendelea kuruka kila upande. Kila kipande kinakuwa hatari kwa satellite nyingine, ISS, au hata mission za kwenda mwezi na Mars.
International Space Station

Wanasayansi wana hofu ya kitu kinachoitwa “Kessler Syndrome.” Hii ni scenario ambapo collisions zinaongezeka mfululizo mpaka space ya karibu na dunia inaanza kujazwa na vipande vya uchafu kiasi kwamba kutuma satellite mpya kunakuwa hatari sana. Collision moja inaweza kusababisha nyingine, halafu nyingine tena kama chain reaction.

Kwa sasa kuna mifumo maalum ya kufuatilia space junk masaa 24. Marekani, China, Urusi na mashirika binafsi yana radar na telescope zinazofuatilia maelfu ya vitu vinavyozunguka dunia ili kuzuia migongano.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba hata bolt ndogo au kipande kidogo cha rangi kinachosafiri kwa kasi hiyo kinaweza kutoboa satellite au kuharibu kioo cha spacecraft. Ndiyo maana ISS wakati mwingine hulazimika kubadilisha njia yake ikiwa kuna uchafu wa angani unakaribia kupita karibu nayo.

Kadri internet satellites kama za SpaceX Starlink zinavyozidi kuongezeka, mjadala kuhusu msongamano wa satellites angani nao unazidi kuwa mkubwa zaidi duniani.
 
Nchi ya Tanzania ina Satelite yake?.

Kwanini salelite hazitoroki kwenye mfumo wake.

kwanini hizo satelite zilizokufa hazidondok duniani?. Wakat zinakuwa hazina kasi kuhimili gravity ya dunia
 
unajua juu huko kwenye space sio kama atmosphere yetu..msuguano ni mdogo..zinaendelea kuzunguka dunia kwa miaka mingi mpaka polepole gravity izishushe zikiingia kwenye anga letu zinaungua kama kimondo
 
Umesema kasi ndio inasaidia isidondoke, kwahiyo zinapoharibika na kufa (hazina kasi tena) nategemea kwa haraka zivutwe na gravity na kuanguka dunuani.

Na zikifika atmosphere kwnn zinaungua wakat ndio zilitakiwa kupeperushwa na hewa na kuvutwa dunian kwa haraka?.
 
Umesema kasi ndio inasaidia isidondoke, kwahiyo zinapokufa nategemea kwa haraka zivutwe na gravity na kuanguka.
kufa haimaanish speed imepungua bali namaanisha imepoteza mawasiliano au imeharibika tu kifaa...kas inaendelea ileile kwa sababu hakuna brerki ya ghaflaangani kuisimamisha
 
hio ni kwa sababu ya gravity ya dunia inaendelea kuzivuta muda wote kumbuka na zenyewe ziko kibati muda wote. Hivyo zinakuwa kwenye balance kati ya mvuto wa dunia na speed yake
anway sijui mambo ya satelite.

Kwahiyo satelite inasetiwa kuzunguka eneo hilo hilo moja la dunia parallel?.

Na maanisha kama inamulika TZ bas inakimbia huku inaangaliaa TZ na pia dunia inajizungusha huku inaendelea kuivuta satelite kuendelea kuimulika Tanzania?
 
Na zikifika atmosphere kwnn zinaungua wakat ndio zilitakiwa kupeperushwa na hewa na kuvutwa dunian kwa haraka?.
kinachofanya ziungue ni kwamba ikiwa inashuka kwa speed kali hewa mbele yake inabanwa na kupata joto kali sana. Msuguano na compression ya hewa ndo hutengeneza joto kubwa hata kuyeyusha chuma.so inshort ni kinetic energy inayozalishwa na speed yake ndo inayogeuka na kuwa joto kali
 
Kwahiyo satelite inasetiwa kuzunguka eneo hilo hilo moja la dunia parallel?.

Na maanisha kama inamulika TZ bas inakimbia huku inaangaliaa TZ na pia dunia inajizungusha huku inaendelea kuivuta satelite kuendelea kuimulika Tanzania?
hizo huitwa geostationary satellites zinarushwa juu sana so zinakuwa zinazunguka same speed na dunia jinsi inavyojizungusha.direction moja.so kama satellite imeelekezwa kuangalia Tanzania, itaendelea kuonekana kama ipo hapo hapo ikiimulika eneo hilo muda wote. Ndiyo maana TV satellite dishes huwa yanaelekezwa upande mmoja tu hayafuatilii satellite kila sekunde.ila za internet, GPS zenyewe sio geostationary na orbit zao ni za chini zinapita chini chini tu hapa..
 
Watu wengi wakisikia satellite wanafikiria ni vifaa vichache tu vinavyozunguka dunia, lakini ukweli ni kwamba anga la karibu na dunia limejaa vitu vingi sana kuliko watu wanavyodhani. Kuna maelfu ya satellites zilizotumwa na nchi mbalimbali, makampuni binafsi, jeshi, vyuo vikuu na taasisi za utafiti. Lakini si zote bado zinafanya kazi.

Kwa makadirio ya sasa ya mwaka 2026, kuna zaidi ya satellites 14,000 hadi 15,000 zinazofanya kazi angani zinazozunguka dunia. Ukijumlisha satellites zilizokufa, mabaki ya rocket, na space debris, jumla ya vitu vinavyofuatiliwa angani vinafika zaidi ya 33,000.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba miaka michache iliyopita idadi ilikuwa ndogo sana. Mwaka 2019 kulikuwa na karibu satellites 2,000 tu zinazofanya kazi, lakini sasa zimeongezeka mara kadhaa kutokana na kampuni binafsi kuingia kwenye space race.

Baadhi ya satellites zimeharibika, zimepoteza mafuta, au teknolojia yake imepitwa na wakati. Tatizo ni kwamba hata zikifa hazidondoki moja kwa moja duniani. Zinaendelea kuzunguka angani kwa miaka mingi sana zikiwa kama “magari yaliyoharibika barabarani” lakini kwenye space. Hizi ndizo huitwa “space junk” au uchafu wa angani.

Kinachofanya jambo hili kuwa la kutisha ni kasi yake. Hata satellite iliyokufa inaweza kusafiri kwa zaidi ya kilomita 27,000 kwa saa. Hiyo ni kasi kubwa mno kiasi kwamba kipande kidogo tu cha chuma kinaweza kuharibu satellite nyingine kabisa kikigongana nayo. Kwenye space hakuna breki wala hewa ya kupunguza mwendo, hivyo vitu vinaendelea kukimbia kwa kasi kali sana.

Mfano wa kutisha ni pale satellite au rocket ikilipuka au kugongana. Vipande vyake vinaweza kuwa maelfu ya vipande vidogo vinavyoendelea kuruka kila upande. Kila kipande kinakuwa hatari kwa satellite nyingine, ISS, au hata mission za kwenda mwezi na Mars.
International Space Station

Wanasayansi wana hofu ya kitu kinachoitwa “Kessler Syndrome.” Hii ni scenario ambapo collisions zinaongezeka mfululizo mpaka space ya karibu na dunia inaanza kujazwa na vipande vya uchafu kiasi kwamba kutuma satellite mpya kunakuwa hatari sana. Collision moja inaweza kusababisha nyingine, halafu nyingine tena kama chain reaction.

Kwa sasa kuna mifumo maalum ya kufuatilia space junk masaa 24. Marekani, China, Urusi na mashirika binafsi yana radar na telescope zinazofuatilia maelfu ya vitu vinavyozunguka dunia ili kuzuia migongano.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba hata bolt ndogo au kipande kidogo cha rangi kinachosafiri kwa kasi hiyo kinaweza kutoboa satellite au kuharibu kioo cha spacecraft. Ndiyo maana ISS wakati mwingine hulazimika kubadilisha njia yake ikiwa kuna uchafu wa angani unakaribia kupita karibu nayo.

Kadri internet satellites kama za SpaceX Starlink zinavyozidi kuongezeka, mjadala kuhusu msongamano wa satellites angani nao unazidi kuwa mkubwa zaidi duniani.
Nasikia jeshi la mgambo la CCM lilirusha satellite 🛰️ 📡 yake kuelekea kizimu. Na siku sio nyingi chama kizima kitahamia huko
 
bado ila washapewa orbit yao nadhani haitafika 2030 tutarusha tu kama rwanda na kenya wameweza nasi pia tutaweza
 
Umembiwa free space huo mvutano wa dunia unatoka wapi
aliyekwambia kwenye space hakuna gravity nani..hata kama hakuna hewa huko bado gravity ya dunia ipo ndo maana ISS ipokaribia km 400 toka duniani ila bado kuna gravity inaiendesha japo sio sawa na ya kwenye atmosphere yenyewe imepungua kidogo
 
Umembiwa free space huo mvutano wa dunia unatoka wapi
Uvutano upo ndio mana hazichezi mbali na dunia, uvutano wa dunia ndio unazifanya zisitoke nje ya anga la dunia. Ila voyager ilipo voyager 1 ndio hakuna uvutano wowote inaenda tu na imeshatoka nje ya solar system tokea ilivyotumwa mwaka 70.
 
Back
Top Bottom