Fadlu Davids - The Great Communicator

Fadlu Davids - The Great Communicator

Best Daddy

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2019
Posts
950
Reaction score
1,672
Simba wamepita makocha wengi bora katika mbinu, lakini wachache bora katika maelezo, either kuelezea programu zake, hali ya timu, mbinu zake au kuwasilisha jambo lolote.

Japo sio sifa ya lazima kama kocha, lakini endapo ukawa mzungumzaji mzuri basi inasaidia zaidi.

Fadlu Davids ni moja ya kocha ambao ni bora sana katika kuwasilisha mambo au katika mazungumzo. Kwa wale ambao walifanikiwa kusikiliza vile anavyozungumza kuhusu kambi na maendeleo yake wakati wa pre-season basi unaweza sema hapa umepata Kocha.

Ni kocha mwenye nadharia(theory) kubwa sana ya mpira. Kwa hii nadharia kubwa na uwezo mkubwa wa uwasilishaji basi ni kocha mzuri kwa vijana(kuwatoa ujinga, u-mtaaani) au kufundisha academy au kuwa Kocha msaidizi endapo akishindwa kufanya kazi kama Kocha Mkuu.

Hapa wamepita akina Robertinho, Mgunda, Benchika ni ngumu kuelewa anataka kusema nini? kuna wakati unakuta kocha anaamua kumeza maneno tu kama Mgunda, kila siku anarudia yale yale.

Huyu jamaa yupo vizuri sana. Nieleweke vizuri sijasema yeye ndio kocha bora, ila ni great communicator.

Kocha mwingine angalau una-enjoy kumsikiliza na ana nadharia kubwa ya mpira basi ni Dabo- Kocha wa Azam FC, pia Gareth Southgate-aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, japo katika vitendo performance ilikuwa ni zero.

Ila kuna hawa wazawa kama akina Julio ni Comedian tu, siwezi kuwaweka katika list ya great communicator.
 
Mzawa ambaye anajitahidi sana ni Denis Kitambi.

Jamaa anajua sana kuzungumza. Nimepata nafasi kama mara mbili tu ya kumsikiliza, anajua kueleza.

Guardiola mnene yeye utasikia kwanza tumshukuru Mwenyenzi Mungu, every now and then.
 
Mzawa ambaye anajitahidi sana ni Denis Kitambi.

Jamaa anajua sana kuzungumza. Nimepata nafasi kama mara mbili tu ya kumsikiliza, anajua kueleza.

Guardiola mnene yeye utasikia kwanza tumshukuru Mwenyenzi Mungu, every now and then.
Yes Yes. Denis Kitambi yupo vizuri pia.
 
Hivi wakuu huwa mnapata nafasi ya kusikiliza yale anayazungumza Fadlu?
 
Ukipata nafasi, hata kidogo basi jaribu kurejea kile anachokizungumza huyu bwana mdogo.

Ana madini sana, Kijana.
 
Hata kama itatokea ameshindwa kupata matakeo, au kufika malengo ya Klabu.

Simba tuna muhitaji hata mwaka mkoja mzima ili atusaidie kutoa toa ujinga wa wale watoto(wachezaji).
 
kwanu kuzungumza sana ndo nini ?? Mpira uwanjani mengine hadithi tuuu!
 
Back
Top Bottom