Fahamu adhabu ya Uhaini

Fahamu adhabu ya Uhaini

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Kwa mujibu wa sheria ya Tanzania, mtu akifanya yafuatayo huhesabiwa kama amefanya kosa la jinai la uhaini hivyo huadhibiwa kulingana na ukubwa wa kosa hilo.

Kifungu cha 39 (1) cha kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, kujaribu kumuua Rais, kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano, kusababisha, kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kuhusu kifo, kumwondolea Rais heshima na jina la Mkuu wa nchi, Amiri jeshi mkuu, au kiongozi wa Serikali, kupindua serikiali iliyo madarakani, kutishia Serikali, Bunge au Mahakama kwa makosa haya na yale yaliyotajwa hapo juu mtu wa namna hiyo atakuwa ametenda kosa la jinai ambalo ni kosa la uhaini

Mtu atakayekutwa na hatia ya kosa la uhaini adhabu yake ni kifo na sheria hiyo ya kifo imeelezwa katika kifungu cha sheria namba 39 na 40 cha kanuni za adhabu.
 
Vipi tena mbona tunaanza kutishiana na vifungu vya sheria....!!?
 
Na kuna wengi mtandaoni wanaweza kuangukia katika kuchochea na kushawishi.. hili ni hatari sana.
 
Kwa mujibu wa sheria hii kunauwezekano raisi akawa anafanya uhaini akiwa angali kwa office?
 
Hukumu ya adhabu ya ugaidi ni kunyongwa hadi kufa, je, baada ya hawa "magaidi" watatu kunyongwa hadi kufa tutarajie wawekezaji wengi toka uarabuni? Kwanini uarabuni, kwa sababu wenzetu hao hukumu za vifo ni za kawaida sana kutokana na miongozo ya dini yao, pia hatutakuwa na upinzani kwenye mikataba ya uwekezaji.
 
Adhabu ya mhaini siyo kunyongwa.
Mtu akishaitwa mhaini,anahojiwa,kama hataki kujibu,sigara inazimwa kwenye ngozi yake.
 
Hukumu ya adhabu ya ugaidi ni kunyongwa hadi kufa, je, baada ya hawa "magaidi" watatu kunyongwa hadi kufa tutarajie wawekezaji wengi toka uarabuni? Kwanini uarabuni, kwa sababu wenzetu hao hukumu za vifo ni za kawaida sana kutokana na miongozo ya dini yao, pia hatutakuwa na upinzani kwenye mikataba ya uwekezaji.
Kwamba nchi inaanza kutoa adhabu zinazopendwa na Waarabu?
 
Nchi zisizojali haki za wananchi wake hutumia ugaidi kama fimbo ya kuwanyamazisha wananchi wake bila kujua kuwa madhara yanairudia nchi kuliko mlengwa.
 
Kwa mujibu wa sheria ya Tanzania, mtu akifanya yafuatayo huhesabiwa kama amefanya kosa la jinai la uhaini hivyo huadhibiwa kulingana na ukubwa wa kosa hilo.

Kifungu cha 39 (1) cha kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, kujaribu kumuua Rais, kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano, kusababisha, kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kuhusu kifo, kumwondolea Rais heshima na jina la Mkuu wa nchi, Amiri jeshi mkuu, au kiongozi wa Serikali, kupindua serikiali iliyo madarakani, kutishia Serikali, Bunge au Mahakama kwa makosa haya na yale yaliyotajwa hapo juu mtu wa namna hiyo atakuwa ametenda kosa la jinai ambalo ni kosa la uhaini

Mtu atakayekutwa na hatia ya kosa la uhaini adhabu yake ni kifo na sheria hiyo ya kifo imeelezwa katika kifungu cha sheria namba 39 na 40 cha kanuni za adhabu.
Hii post ni ya mwaka 2020 inawezekana ulikua unawaonya watu lakini ndo hivo tena sikio la kufa
 
Back
Top Bottom