Angeelezea introvert na extrovert kwa makundi manne usingejikosa!! Binafsi naona hajawaelezea hawa Sanguine hili ni kundi linalotoka ktk extrovert,watu ambao hawana lile shipa la aibu! Hawa ndio wazee wa show off wanapenda kusikilizwa,Ni washawishi wazuri,waongeaji,wachekeshaji,wanashauku Sana,si wazuri ktk ratiba! Yani hawana ratiba maalum ye kitu kikimgusa tu tayari twende,ni very social na huwa na marafiki wengi, hupenda kujulikana(kuwa maarufu).
Hupendelea kufanya kazi za kuonekana ili apate sifa n.k na hawapendi kazi ngumuuu![emoji41]
Kazi wanazopendelea kufanya ni Kama kuwa mtangazaji(mshehereshaji),uanamuziki,uchekeshaji n.k si kila mwenye hizo kazi Ni kutoka kundi hili hapana ila wengi wao hutoka hapa.. Dully Sykes ni moja ya kiumbe niliemtazama na kugundua anatoka kundi hili..
Ukiifahamu saikolojia kiundani Kuna watu utajua wanafaa wapi na wapi na ukiwa unaakili kubwa utaweza kuwaendesha kwani kila mmoja unajua udhaifu wake na uimara wake!,na elimu hii ikitumika ktk kuendesha kampuni unaweza kupata wafanyakazi unaowataka na ukafika unapopataka ila muda ndo unaohitajika!! Kuwasoma watu si jambo jepesi ila moja kati ya kundi jepesi kuwasoma ni hawa niliokutajia hapa.. wapo wengi ktk jamii hata likitokea tukio hawa wanakuwa wakwanza kufika na kuanza kutoa msaada tofauti na makundi mengine kidogo mpk wajivute fulani hivi hasa introvert maana hawa mara nyingi ni watu wa mantiki!! Maswali ya kwanini..? Kivipi..? Muda gani..? Hutoka kwao ni kwamba hawafanyi kitu kihisia zaidi ila in logics.