Ben Zen Tarot
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,298
- 7,612
1. Usimpigie mtu simu zaidi ya mara mbili mfululizo. Ikiwa hapokea simu yako, chukulia kuwa ana jambo muhimu yuko analifanya.
2. Rudisha pesa ulizokopa hata kabla mtu aliyekukopa hajakukumbusha au kukuomba. Kufanya hivi kunaonyesha ni jinsi gani ulivyo mwaminifu, na kutakufanya uaminike zaidi.
3. Usiagize chakula kingi usichoweza kukimaliza unapokuwa mgahawani au hotel. Agiza chakula kinachokutosha na utakachokimaliza, hii itakufanya uonekane ni jinsi gani unavyothamini chakula na kuheshimu juhudi za wakulima.
4. Usimuulize mtu maswali ya aibu mbele ya watu kama ‘Oh kwa hiyo bado hujaolewa?’ .au ‘Je, huna watoto’ au ‘Kwa nini hujanunua nyumba?’ Au kwa nini hununui gari?. Hilo sio jukumu lako, ni jukumu lake mhusika pamoja na MUNGU wake.
5. Ikiwa unapawe ofa na rafiki yako katika kulipia mambo tofauti tofauti wakati wa matembezi, Jitahidi na wewe umlipie wakati ujao, ili asikuchoke au kukudharau maana binadamu hawana dogo.
6. Heshimu maoni au mawazo ya mtu kwa kumsikiliza wakati anapoongea. Kumbuka kile ambacho ni 6 kwako kitaonekana 9 kwa mtu mwingine, usidharau maoni au mawazo ya mtu hata kama unajua kaongea pumba.
7. Usimkatishe mtu katika kipindi ambacho anazungumza, sikiliza kwanza akimaliza kuongea na wewe ongea, hii itasaidia kuepuka ugomvi au mabishano wakati wa mazungumzo yenu.
8. Usimseme mtu vibaya au kuongea mabaya yake mbele ya watu wengine, ikiwa una mabaya yake mtafute na zungumza nae kwa upendo ili ayatambue madhaifu yake na ajisahihishe. kumbuka hakuna binadamu mkamilifu.
9..Usisahau kusema asante katika kipindi ambacho unapokea kitu chochote kutoka kwa mtu au kusaidiwa jambo fulani. Hii itaonyesha ni jinsi gani unavyothamini.
10. Jifunze kumsifia mtu hadharani.na mkosoe mtu faraghani, hii itaonyshesha ni jinsi gani ulivyo muungwana. Usimkosoe mtu hadharani.
11.Mtu anapokuonyesha picha kwenye simu yake, usitelezeshe kidole chako kushoto au kulia. Huwezi kujua nini kinafuata, Jenga tabia ya kufanya kile ulichoelekezwa kufanya, tena kifanye kwa uaminifu.
12. Mwenzako akikuambia anajisikia vibaya kuwa mwelewa, usitake kujua sababu za kwanini anajisikia vibaya ikiwa hajakuambia.
13. Mtende na kumfanyia mfanyakazi wako wa ndani mambo unayowafanyia watoto wako, ikiwa ni upendo muonyeshe upendo kwa kumtimizia mahitaji yake yote. Kumbuka wewe umezaa tuu, ila yeye anakulelea watoto wako.
14. Ikiwa mtu anazungumza moja kwa moja na wewe, huku ukitazama simu yako au unacharti ni kukosa adabu. Jifunze kuweka umakini wako katika jambo moja.
15. Usitoe ushauri kamwe hadi uombwe; ili usije onekana umejipendekeza kwa kutoa ushauri usiohitajika.
16. Ondoa miwani yako ya jua ikiwa unazungumza na mtu yeyote barabarani. Ni ishara ya heshima.
17. Usizungumze kamwe kuhusu utajiri wako katikati ya watu maskini. Vivyo hivyo, usizungumze juu ya watoto wako katikati ya mtu tasa. Usizungumze kuhusu wazazi wako katikati ya mayatima.
Natumai umenielewa.