Fahamu Faida na Mbinu za Kupeleka Kampuni/ Biashara katika SOKO la HISA

Fahamu Faida na Mbinu za Kupeleka Kampuni/ Biashara katika SOKO la HISA

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,973
Reaction score
6,750
Habari za wakati;
Habari za wakati huu.Ni matumaini yangu kwamba unaendelea salama na Ujenzi wa Taifa na Uchumi binafsi.

Leo nataka nilete mada hii kwa ufupi ili nichokozi mjadala uanohusu soko La Hisa.Kabla ya kuanza kwa mjadla niweke wazi kwamba mimi sio mtaalamu wa fedha,wala biashara,wala uwekezaji na kwamba andiko hili sio ushauri wa kitaalama bali ni maoni na mtazamo wangu kulingana na uelewa wangu.Baadhi ya mambo nitakayoweka yanaweza yasiwe sahihi au yakawa na kasoro hivyo kabla ya kufanya uamuzi tafadhali tafuti ushauri wa kitaalam kwa kdiri ya mahitaji yako.Sasa Tuanze.

Soko la Hisa ni Nini?
Kimsingi soko la hisa au soko la mitaji ni moja kati ya masoko ya fedha ambapo watu wenye mitaji na watu wanaohitaji mitaji hukutana ili kufanya biashara.Katika Soko la Hisa,Hisa kama aina moja wapo ya vipimo vya umiliki na thamni huuzwa kutoka kwa mwekezaji moja kwenda kwa mwingine.Hivyo basi katika soko la hisa watu wanauziana umiliki wao katika biashara fulani.Ni kama mtu mwenye DUKA anapoamua kumuuzia mtu mwingine DUKA lake.Sasa katika soko la hisa uuzaji unafanyika kwa sehemu tu ya umiliki bila kuzingatia thamani halisi ya biashara husika.

Hivyo basi katika SOKO la hisa kuna wakati bei ya HISA inaweza kuwa Juu sana kuliko thamani halisi ya Biashara au inaweza pia kuwa chini sana kuliko thamni halisi ya biashara inayohusika.Kwa mfano kampuni ya SPACE X inaweza kuwa na Mali na Madeni.Sasa huenda Madeni yake ni Makubwa kiasi labda cha nusu ya thamani ya Mali zake ila sasa katika soko la HISA ukakuta Thamani yake ni Mara 2 ya Thamni halisi ya Mali zake(Huu ni Mfano).Kinachofanya hali iwe hivi ni kutokana na hali ya SOKO na shughuli za SOKO.Wawekezaji wengi hununua hisa kwa matarajio kwamba zitapanda thamani ndani ya muda fulani na UBASHIRI huo ndio ambao unafanya BEI ya HISA Ipande au ishuke kwani kila mwekezaji hufanya maamuzi kwa kutegemea na matarajio yake.Baada ya kueleza utangulizi huo sasa nieleze namna ya kupeleka Kampuni katika soko la Hisa.

Kwa Tanzania kwa sasa Tuna SOKO moja tu la HISA ambalo ni DSE hata hivyo sheria haikatazi kuundwa kwa masoko mwengine ya Mitaji.Mamlaka inayosimamia Uanzishwaji wa Masoko ya Mitaji inaitwa CMSA ambayo inahusuika na USIMAMIZI wa DSE,Inasimamia Pia Mchakato wa uingizaji wa kampuni katika SOKO la Hisa,Inawasimamia Madalali,washauri na wadau wengine wanaohusika na SOKO la HISA.Nisisitize hapa kwamba kwenye SOKO la hisa hata dhamana za serikali na za Makampuni makubwa zinaweza kuwekwa sokoni kama zilivyo HISA na zote zinasimamiwa na Taratibu za CMSA.Hata hivyo sina uhakiksa sana kma Treasury Bill zile zinazouzwa na BOT nazo zinasimamiwa na CMSA ila nafahamu kwamba za makmpuni binafsi zinasimamiwa zote na CMSA(Hii iwe kama homework kwako.Tafuta iwapo Dhamana na hatifungani za Serikali zinasimamiwa na CMSA na ni kwa kiwango gani.


Sasa unapotaka kupeleka kampuni yako DSE sehemu ya kwanza unatakiwa kwenda na CMSA maana wao ndio ambao watasimamia mchakato wa hatua za mwanzo za uuzaji ambao huitwa IPO(InitialPublic Offering).Hata hivyo kabla ya kufanya hivyo ni lazima kwanza UUNDEL Kampuni ambayo inatakiwa iitwe PUBLIC LIMITED COMPANY(PLC),Kampuni lazima iwe na wanahisa wasiopungua 50 na iwe na Wajumbe wa BODI wenye weledi na Utaalam.Kama kampuni yako ni ya Binafsi itakubidi kwanza uibadili iwe Public kisha ndio uweze kuanza mchakato mwingine.

Jambo lingine la kuzingatia ni kwamba lazima ufahamu unataka mtaji kiasi gani,Bei ya Hisa ni kiasi gani na Uoneshe Historia ya Utendaji ama Uoneshe Mwelekeo wa kampuni unaoshawishi.Katika Hili unatakiwa uwe na nyaraka ambayo inaitwa PROSPECTUS.Katika Hatua hii ni muhimu sana ukawa na mshauri ambaye amesajiliwa na CMSA ambaye ndiye atakayekuongoza katika hatua za kitaalamu na kisheria ili kuhakikisha kwamba unakidhi vigezo vyote.Madalali wengi wa SOKO la Hisa pia wana kibali cha kufanya hizi shughuli katika hatua za mwanzoni kama washauri.Zingatia kwamba kampuni yako lazima iwe na mwanasheria mbaye ndiye atakuwa katibu wa kampuni na Pia Mkurugenzi wa Fedha lazima awe na elimu ya Fedha na angalau CPA.Hii ni muhimu kwa sababu wewe unataka kukusanya hela za watu hivyo ni lazima ukidhi vigezo vyote vya kisheria na kitaalam.Unaweza ukachukua Hela za watu kisha wakishakupa Ukafikiri ni zako ukaanza kununulia magari.

Jambo lingine la kufahamu ni kwamba unapoamua kupeleka kampuni yako kwenye soko la hisa hasa iwapo kampunu inahsitoria ya utendaji na wewe ni mmiliki mkubwa ni muhimu sana ukaamua iwpo unataka kampuni yako baada ya kuwa ya umma mmiliki mkubwa awe ni nani.Hii ni kwa sababu wewe umeshaweka nguvu,muda na una maono fulani na iwpo utaachia watu wengine wawe na hisa nyingine zaidi kuliko wewe wanaweza kutofautiana na wewe na katika kampuni ya umma unaweza hata kuondolewa katika kampuni.


Ukikamilisha mchakato wa CMSA kulingana na mahitaji yako utatangaza tarehe ya kuanza kwa IPO ambapo utaonesha njia ya watu kununua HISA kwa sasa DSE wamerahisisah unaweza WEKA IPO yako kwenye DSE APP na huko watu wakanunua na kulipia moja kwa moja.Baa ya IPO kufungwa.Utaangalia iwapo HISA zimeuzika zote au la na iwapo kuna watu wameomba kununua hisa lakini zimezidi(Oversubsrciption)Iwapo wanunuzi wamezidi basi itabidi waliokosa warudishiwe mpunga wao.

Hapa nimeeleza kwa ufupi ili kuchokoza mjadala.Hata hivyo ninaamini kabisa kwamba wapo wadau ambao wanaweza kuweka hapa taarifa zaidi ili sote tuendelee kujifunza na kuhamasishana zaidi ili tuweze kuwa na kampuni nyingi ndogo na za kati ambazo zinataka kuingia katika SOKO la HISA.Karibuni tujadiliane
 
Bado tuna kampuni chache dse, usa karibia zote leading zipo nyse
 
Umeeleza vizuri lakini nahisi kama umesahau kiasi cha mtaji kampuni inatakiwa kuwa, lakini pia lazima iwe imepata faida kwa miaka mitatu iliyopita.
 
hivi mkuu Masokotz ,

Kwa uzoefu wako hapa bongo haya mambo ya hisa yanaweza kumtoa mtu?? maana kwa sasa wameibuka waalimu wengi mitandaoni wa maswala haya ya hisa wakitoa elimu namna ya uwekezaji ila wanataka kulipwa wao ili waweze kuitoa elimu hiyo.. Je, Unaweza kuwa na mifano au experiance yoyote kwa hapa bongo namna watu wamekuwa matajiri kwenye swala hili la hisa from humble beginnings? namaanisha kwamba mtu ameanza na kiasi cha uwekezaji kama wa shilingi millioni tano na mtaji ukakua kwa miaka kadhaa???

nina interest ya kuwekeza sana ila sijui niwekeze kwenye DSE and UTT au sijui mambo ya bonds.. sasa sina elimu na nikiwaza kuwalipa hawa online influencers naona kama ni yale yale mambo ya forex
 
hivi mkuu Masokotz ,

Kwa uzoefu wako hapa bongo haya mambo ya hisa yanaweza kumtoa mtu?? maana kwa sasa wameibuka waalimu wengi mitandaoni wa maswala haya ya hisa wakitoa elimu namna ya uwekezaji ila wanataka kulipwa wao ili waweze kuitoa elimu hiyo.. Je, Unaweza kuwa na mifano au experiance yoyote kwa hapa bongo namna watu wamekuwa matajiri kwenye swala hili la hisa from humble beginnings? namaanisha kwamba mtu ameanza na kiasi cha uwekezaji kama wa shilingi millioni tano na mtaji ukakua kwa miaka kadhaa???

nina interest ya kuwekeza sana ila sijui niwekeze kwenye DSE and UTT au sijui mambo ya bonds.. sasa sina elimu na nikiwaza kuwalipa hawa online influencers naona kama ni yale yale mambo ya forex
Kwa kuanza Pitia Huu uzi,Umegusia mambo mengi sana

Nitarudi hapa na majibu zaidi
 
Back
Top Bottom