Dr Luu
JF-Expert Member
- Nov 24, 2016
- 489
- 386
Napal cactus ni mmea wenye asili ya jangwani hasa unapatikana maeneo ya Afrika, Amerika na Asia. Kutokana faida zake na muingiliano wa watu imefanya kusamba maeneo mbalimbali duniani kote. Nopal imekuwa chakula pendwa zaidi Mexico, Asia na baadhi ya maeneo ya Afrika magharibi. hutumika zaidi majani mchanga kwani yakikomaa sana Huwa magumu kutafuna. Zipo faida nyingi za huu mmea kwa afya ya mwanadamu.
FAIDA
1. Inapunguza cholesterol mwilini
2. Inapunguza madhara ya hangovers (utakapokunywa juisi yake + tango)
3. Inapunguza uvimbe wa prostate
4. Hupunguza sumusumu mwilini hasa kwenye damu.
5. Hulinda mishipa ya fahamu
6. Hupunguza uwezekano wakupata presha ya macho (glaucoma)
7. Hutibu vidonda vya tumbo na pia nyuzi zake hutumika kutengezwa plaster za vidonda
8. Hutoa uchovu
9. Hutibu magonjwa ya ngozi
10. Hutibu magonjwa ya mifupa hasa kupunguza uwezekano wakusagika kwa viungo (joints) kwa kuongeza Ute kwenye joints.
11. Husaidia kutibu gout.
NAMNA YAKUTUMIA
1. Dawa
Chukua nopal bàada yakuiosha na ikatekate kama chips( vipande vidogo huwezavyo) kiasi kisha weka kwenye chombo safi kisha changanya na maji ujazo mara mbili ya ujazo wa vipande hivyo. Kisha acha kwa dk 30 Hadi saa 1, kisha chuja kwa kumimina kwenye chombo kingine. Sasa waweza kunywa hayo maji kama dawa. Waweza kunywa nusu Lita ya hayo maji mara 3 kwa siku.
Ladha: sio chungu ni kama unakunywa maji.
2. CHAKULA
Waweza kutumia kama kiungo Cha mboga, sehemu ya salad au juisi.
Link za upishi link1 link2 link3
Asante