Fahamu faida za kuwafundisha wengine kile unachokijua

Fahamu faida za kuwafundisha wengine kile unachokijua

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Hukuongezea Maarifa
Kufundisha wengine ni njia bora ya kuongeza Maarifa yako kwasababu utahitajika kujiandaa kwa kusoma na kujifunza mambo mbalimbali ili uweze kufundisha vyema

Huwezesha kujitathmini
Njia bora ya kujitathimini ni kwa kufundisha wengine kile unachokijua kisha uwaruhusu wakupe tathimini ya uwezo wako. Kwa njia hii utatambua ni jambo gani unalolifanya kwa ubora na ni wapi ufanye maboresho zaidi

Hukuwezesha kutatua matatizo ya Watu
Kuwafundisha Watu mambo mbalimbali ni njia bora na ya gharama nafuu ya kutatua matatizo yao. Fikiri ukimfundisha Mtu jinsi ya kujikinga na maradhi fulani, akifanyia kazi maarifa hayo na kuona matokeo tayari utakuwa umetatua tatizo lake.
 
Tatizo pale unapokutana na mtu mjuaji na mwenye dharau

Mtu unaona kabisa hajui,ila anakomaa na ukimuomba umfundishe anakudharau
 
Shukran kwa kushare Ms Zomboko, hakika hili ni jambo jema, binafsi hua napenda sana kuwapa wengine ule ujuzi nilionao

Shukran kwako pia leo umeleta uzi usiokua na huzuni wala majonzi
 
Back
Top Bottom