FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
Matumizi ya mifuko ya plastiki inaweza kusababisha madhara yafuatayo;
1.) Kansa za aina mbali mbali
- Uchomaji wa mifuko ya plastiki majumbani, mabarabarani, mahospitalini pamoja na kwenye madampo husababisha kemikali za sumu aina ya carcinogens kusambaa hovyo kwenye hewa unayovuta. Mfano wa kemikali hizo ni 'Dioxins' na 'Furans' ambazo tafiti zimeonyesha kuwa na uhusiano mkubwa sana na magonjwa ya cancer na hata matatizo ya mifumo ya upumuaji kwa binadamu. Tupime kodi tunayokusanya kwenye mifuko hii vs hasara na mateso tunayopata kutibu watu kule hospital ya cancer ya ocean road, mamlaka zinazohusika zichukue hatua sasa.
2.) Matatizo ya homoni za jinsia (Ushoga na usagaji)
- Kemikali ya 'Dioxin' ambayo hupatikana kwenye moshi wa taka za plastiki zilizochomwa, endapo itavutwa kwa njia ya hewa na mtoto mchanga, utafiti umeonyesha kwamba inaweza ikasababisha mfarakano katika mfumo wa homoni za jinsia kwa mtoto huyo. Mtoto wa kiume anaweza akaja kuanza kuonyesha tabia za mtoto wa kike, na mtoto wa kike anaweza akaanza kuonyesha tabia za mtoto wa kiume hapo baadae, hivyo kupelekea kuongezeka kwa mashoga na wasagaji katika jamii. Waziri anaehusika apime haya na afanye maamuzi sahihi.
3.) Matatizo ya mfumo wa uzazi kwa wanaume wasio mashoga (Uhanithi na 'low sperm count')
-Utafiti umeonyesha pia, katika maeneo ambayo wanaume wake wamekuwa 'exposed' na kemikali za 'Dioxins' na 'Furans' kwa muda mrefu, pamekuwa na ongezeko la kushindwa kusimamisha viungo vya uzazi (usenge) pamoja na kuongezeka kwa matatizo ya wanaume kushindwa kurutubisha mayai (Low sperm count/weak sperm cells). Hili linahitaji kitabu kizima kuanza kufafanua, nashauri kila mtu akafanye research zaidi kwenye makala za kitabibu ili kupata undani wake. Pia katika maeneo hayo, imeonekana kwamba wasichana wanavunja ungo mapema mno. Hii hali naiona sana Tanzania, waziri unaehusika, waokoe wananchi wako.
4.) Athari za kiafya kwa wanyama, ndege na samaki
- Wanyama kama n'gombe hufananisha mifuko ya plastiki na chakula, hivyo huweza kuimeza na kusababisha kuziba kwa utumbo na hatimae kifo.
5.) Mifuko ya plastiki huweza kukaa hadi miaka 500 bila kuoza.
- Mifuko hii huwa haiozi bali huvunjika vunjika na kuwa vipande vidogo vidogo sana ambavyo huweza kujichanganya katika mifumo yetu ya maji na chakula na kusababisha watu kula na kunywa plastiki kwa kiwango kikubwa sana bila kujijua. Vipande hivyo vya pastiki ni sumu inayoua taratibu.
6.) Mifuko ya plastiki hupeperuka kirahisi na kuchafua mandhari
- Kutokana na kuwa miepesi sana, mifuko hii hupeperuka kirahisi kutoka kwenye vyombo vya kubebea taka na kwenye madampo, hivyo kusambaa hovyo kwenye makazi ya watu na kuharibu mandhari, pia huziba njia za maji na kusababisha mafuriko, pia mifuko hii hutumika kama mazalio ya vilui lui vya mbu waenezao malaria.
======================================
UPDATE:
Kamati ya Bunge ya viwanda na biashara yaagiza Serikali kupiga marufuku mifuko ya plastiki kutoka nje ya nchi
================================
UPDATE: 09/04/2019
Hatimae serikali kupitia waziri mkuu wamepiga marufuku, uzalishaji, uagizaji na matumizi ya mifuko ya plastiki nchi nzima, Tanzania inaelekea kuwa kama Rwanda sasa kwa usafi.
=====================================
Update: 24/05/2019
www.jamiiforums.com
===============================
Update: 08/04/2021
www.jamiiforums.com
================================
Nashukuru mpaka sasa tumefanikiwa kupata like 42 katika kampeni hii

Fahamu Miongozo kwa Wakaguzi wa Mifuko ya Rambo
Imekua kawaida binadamu akipewa madaraka kutumia fursa hiyo kukandamiza wengine. Kufukia Juni 1 mifuko ya Rambo haitatakiwa kutumika tena. Kuna watu wamepewa dhamana ya kukagua mifuko ya rambo sehemu mbalimbali. Nimeona niwasogezee kanuni wanazopaswa kuzifuata Wakaguzi hawa ili kila mwananchi...
Update: 08/04/2021
Waziri Jafo: Msako wa vifungashio kuanza kesho
Waziri wa Muungano na Mazingira, Selemani Jafo amesema kesho wataanza msako wa kukamata vifungashio vya plastiki kupitia NEMC na TBS . Msako utakuwa kuanzia viwandani na mitaani