Baada ya hayo maelezo yako nimelazimika kuiangalia hiyo video ya mahojiano! Refresh your memory... ni lini Clouds TV ilikuwa hewani? Ni lini Nenda Kamwambie ilitoka? Kwenye dakika ya 16:25 Sporah anamuuliza Rommy "Hapo Diamond alikuwa sio mtu yeyote?"
Kumbuka amemuuliza hili swali baada ya Rommy kutoa maelezo kwamba, baada ya kufanyiwa interview hapo hapo akalamba kazi Clouds TV lakini baada ya muda mambo yaakanza kuwa si mambo baada ya kuanza kuja wafanyakazi ambao walipitia audition, mara kinatokea hiki mara kile.... n.k! Remember, Clouds TV ilianza mwishoni mwa November 2009 na kuwa active ilikuwa 2010... kwahiyo hapo unaweza ku-approximate hayo inaweza kuwa yalitokea wakati gani! Na haishangazi, Rommy mwenyewe anaeleza kwamba, alianza hiyo kazi mwaka 2010 au 2009 mwishoni! Akili ya kawaida haishawishi kwamba ilikuwa 2009 coz' haiwezekani, kuanza na kuanza mara matatizo yanatokea kwahiyo kauli yake kwamba ilikuwa 2010 inaweza kuwa ndiyo sahii!
Baada ya hilo swali ("Hapo Diamond alikuwa sio mtu yeyote?"),
Rommy anajibu: "Anh... Diamond, no!"
Sporah: "Diamond hapo ndo anakuona kwenye TV, mwanangu nitoe na mimi"
Rommy: "Diamond hapo ndo ana-struggle, mimi roho inaniuma mdogo wangu....... kipindi hiko mimi nakaa Kinondoni, yeye anakaa Tandale, nikenda kule, dah, hana mia... hana lolote!"
Now the question: Hivi kweli mtu ambae hadi 2010 inaingia hana lolote, hata mia hana na ndo kwanza ana-struggle halafu mara: Does it make any sense mtu ambae hadi 2010 inaingia hajulikani, hata 100 mfukoni hana na ndo kwanza ana-struggle lakini March 25, the very same year anakuwa nominated KTMA na kushinda tunzo tatu na kuweka historia???!!! And don't forget, Mbagala ilianza kuonekana on TV April 2010 wakati huo Kamwambie imesha-hit tayari na ndio maana nikasema, kama alifanya promo labda hiyo Mbagala lakini sio Kamwambie!