Fahamu jinsi ya kutengeneza ndege ya kichawi, kwenda kokote Duniani

1.Mkoa wa Kigoma unasifika kwa uchawi sana Tanzania kuliko mikoa mingine je kuna ukweli gani juu ya hili? Na kwa nini Kigoma kuwe na wachawi wengi kuliko mikoa mingine?

2.Wazungu ni wachawi? Uchawi upi una nguvu kati ya uchawi wa kizungu na uchawi wa kiafrika? Uchawi wa kizungu unatumia tunguli na (makorokoro mengine) kama Afrika?
 
1-WanaKigoma kuzungumzia swala la uchawi (hatujidai nalo, na wala hatulipendi kulinganishwa nalo ispokuwa ni ile hali ya kua karibu nalo kimipaka, kwasababu nchi 4 zinazo ongoza kwa nguvu za giza Afrika ni pamoja na Sudan kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati, na Kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Sasa, sisi watu wa Kigoma tupo karibu nalo kimipika kutokea nchi ya Kongo. Kwa ujumla uchawi upo kila sehemu, na uchawi mkali zaidi unapatikana mijini kuliko vijijini.

2-Kiasili uchawi ulianzia nchi ya Haiti, mazoezi ya uchawi au ulozi yapo ulimwenguni pote kila nchi, na ulaya kuna uchawi mkali zaidi kuliko Africa, unaitwa 'Wicca' hao wenyewe wamejisajili kabisa kama imani ya kidini.
 
Mkuu kama umeokoka na unamwamini Yesu wachawi bado watakuwa wanaendelea kukusumbua?
 
Hivi ndugu zangu mnaamini kuna uchawi? Mmeingia darasani, mnama degree yakutosha, hivi inawezkana binadamu akasafiri angani kwa kutumia hivyo vyombo vya kichawi, ukifikiria kwa undani utapata jibu kuwa ni uongo, hakuna connection.
Wengi wetu tunasikia tu kuwa kuna uchawi lakini hatujawahi shuhudia live.
I stand to be corrected.
 
Sikuelewa kitu. 1 -0. Baadae ntarudi kusoma tena na tena, labda yataniingia.
 
Afadhali FaizaFoxy hajaiiona hii comment 🀦
Kwanini sijaiona?

Uchawi wenyewe nchi za nje nilizowahi kuishi wanauchukulia kuwa ni "dini na imani" pia.


Kiislam uchawi wa aina yeyote ile ni ushirikina, na kila mshirikina hana msamaha. Makao yake ni motoni tu na maulamaa wengi wanaamini mchawi anaanza kuuona moto kabla hajafa.

Mchawi Kiislam ni mfanya kufuru, kukufuru maana yake ni kuupinga Uislam (kujitoa katika Uislam). Ukimuona mtu anafanya uchawi au wanga anasema yeye ni Muislam huyo anacheza na akili za wajinga tu, siyo Muislam huyo.
 
WALE MASHEIKH WANGANGA WA KIENYEJI WAPIGA RAMLI CYO WACHAWI
 
UKIFIKIRI KWA KINA UTAWASHUKURU WAZUNGU NA WAARABU KWA KUJA NA KUTUTOA HUMO, ENDAPO WASINGEKUJA SIJUI MPAKA LEO HII HALI INGEKUWAJE?, SIPATI JAWABU.
 
Nadhani wewe ni miongoni mwa wachawi maana mchawi hata siku moja hapendi na hataki kujulikana kabisa maana uchawi ni uovu kama ulivyo uovu mwingine kwenye jamii. Hata jina lako tu hapa JF (Kikinga) limekaa/linathibitisha pasi na shaka kwamba yu mkini u-mchawi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…