mkuu sioni haja ya kubishana hapa. kikubwa acheni waathirika tutoe maelezo kadri ya uzoefu.
mimi nilistuka siku hiyo wakala akikariri namba yangu palepale maana ilikuwa rahisi sana kwa vile ina sufuri nyingi nyingi.
nilikuwa nasajili laini 3: mbili za mtandao mmoja na moja ya mwingine. nakumbuka aliniuliza kwa card ya kwanza tu. awamu mbili alikuwa akiniamuru kuweka vidole tu.
nilipo mdadisi namba unaimudu vipi kuikariri akacheka akawa anairudia hadi mara 4 toka kichwani.
hata baada ya zoezi kukamilika, aliwasajilia wadada 4 nikasubiri kujifunza kitu, lkn akawa anajisemea nyie (wale wadada) kuwa namba zenu ni ngumu lkn ya jamaa huyu ni rahisi 198*051*3570*0001*1 niliondoka na mashaka kwamba huenda namba ilibaki inafanya biashara haramu
Sent using
Jamii Forums mobile app