Fahamu kidogo kuhusu magari ya mizigo nchini Tanzania

Fahamu kidogo kuhusu magari ya mizigo nchini Tanzania

KIMOMWEMOTORS

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2018
Posts
358
Reaction score
675
Salama wanajukwaa?

Leo tutagusia baadhi ya gari za mizigo ambazo hupendelewa zaidi hapa nchini kwetu Tanzania. Tutaziangalia kuanzia ndogo kabisa kuelekea zile kubwa.

1. Suzuki Carry
Hizi ni gari ndogo zaidi za kubebea mizigo yenye uzito usiozidi kilo 350 na bodi lake hua na urefu wa mita 3.4. Kuna baadhi zina 2 wheel drive, lakini nyingi zina 4 wheel drive. Kwa wastani gari hizi huweza kwenda kilomita 16 kwa lita moja ya petrol.

Ukubwa wa injini ni Cc 660 lakini zinaonekana kutumia mafuta sawa au zaidi kidogo ya gari zenye ukubwa wa Cc 1000- 1500, hii ni kwa sababu gari hizi za mizigo zina mfumo wa mafuta wa kizamani ikilinganishwa na huu wa kisasa wa Vvti ambao hupelekea mafuta kutumika kidogo zaidi.

Gari hizi zinahitaji matunzo na kupitishwa njia ambayo sio ngumu sana, na mara nyingi uzoefu unaonesha kua gia box yake na injini vinapoanza kusumbua hua havitengenezeki na kutulia hivyo mara nyingi inatakiwa ubadirishe injini yote au gia box yote.

Zikitunzwa ni gari zinazodumu kwa mda mrefu na zinasaidia sana katika kuhamisha mizigo midogo midogo. Mara nyingi gari hizi tunaziagiza kwa gharama zinazoanzia shilingi 10,000,000. Iwapo utaifanya kua gari ya biashara basi kwa siku inaweza kukuingizia hesabu ya shilingi 20,000.

Carry.jpg


2. Toyota Liteace/ Townace

Hii ni kubwa kidogo kwa hiyo ya hapo juu. Kwa hapa kwetu Tanzania, hizi zimekua gari ambazo hukimbiliwa zaidi na wafanyabiahsara kwa ajili ya kurahisisha kazi ya uhamishaji mizigo ya biashara na binafsi.

Hizi ni ngumu zaidi ukilinganisha na hizo za mwanzo, pia zinatengenezeka kwa urahisi, zina nguvu juu ya hizo Suzuki Carry na zinabeba ujazo mkubwa zaidi. Baadhi zina 4wheel drive na nyingine ni 2 wheel drive, bodi lake lina urefu wa mita 4.24, uzito wa hizi gari ni kilo 1290 na zina uwezo wa kubeba kilo 750.

Ki kawaida hutumia lita moja ya mafuta kwa kilomita 14, na mara nyingi bei zake tukiziagiza huanzia 14,500,000. Iwapo utaifanya kua gari ya biashara basi kwa siku inaweza kukuingizia hesabu ya shilingi 30,000.

Town Ace.jpg


3. Mitsubishi Canter
Hizi ni gari nyingine za kazi zeye ukubwa wa kati. Injini zinazoshauliwa sana na mafundi kwa sababu ya uvumilivu wa shida na ugumu ni series ya 4D ambapo maarufu zaidi ni 4D32, 4D33- 4D36. Kwa wastani gari hizi zina uzito wa kilo 2000- 3000.

Urefu wa bodi lake ni mita 4.7. Hizi hutumika zaidi katika shughuli za kilimo, ujenzi, uhamishaji mizigo ya kibiashara na binafsi n.k. Ni gari vumilivu sana na hazishuki thamani kwa haraka hivyo utakapohitaji kuiuza hutaiuza bei ya hasara sana.

Mara nyingi jumla ya gharama za uagizaji zinaanzia 22,000,000 kwa ambazo hazibinui (flat body) na zile zinazobinua yaani dump huanzia 27,000,000. Iwapo utaifanya kua gari ya biashara basi kwa siku inaweza kukuingizia hesabu ya shilingi 60,000.

Canter.jpg


4. Mitsubishi Fighter
Hizi mara nyingi uzito wake huanzia tani 3.5 mpaka 4.5. Wataalam hushauri zaidi injini series ya 6D kama vile 6D14, 6D15- 6D17. Hizi zinatajwa kama injini ngumu na stahimilivu katika magari haya.

Yapo ynayobinua ambayo hua na bodi fupi wakati zile zisizobinua mara nyingimzinakua na bodi refu zaidi. Hizi ni gara za kazi na ubeba wa mizigo ya safari ndefu na fupi pia. Urefu wa bodi lake huanzia kati ya mita 5- 7.7. Jumla ya gharam ya kuagiza gari za aiana hii huanzia 57,000,000.

Iwapo utaifanya kua gari ya biashara basi kwa siku inaweza kukuingizia hesabu ya shilingi 70,000.

Fighter.jpg


5. Mitsubishi Fuso
Hapa tunazungumzia gari za kubeba kokoto, mchanga na bidhaa nyinginezo za kubinuliwa. Kwa wastani huana uzito wa tani 5- 7 wakati urefu wa bodi ukiwa ni mita 6. Hizi ni gari ngumu na manunuzi yake ni nafuu ikilinganishwa na gari tutakayoiona hapa chini aina ya Scania.

Lakini ugumu wake sio sana kama wa hizi aina ya Scania. Hizi Fuso haswa zinazoingia kwenye mashimo ya mchana zimekua aikihitaji umakini zaidi zaidi ziingiapo mashimoni kwani difu yake hua na uwezekao wa kudhurika kutokana na namna ilivyoundwa, lakini pia chasis yake sio ngumu sana kama ilivyo kwa Scania ambazo zina chasis mbili ambazo ni ngumu. Kwa wastani gharam za kuagiza gari hizi huanzia 70,000,000.

Iwapo utaifanya kua gari ya biashara basi kwa siku inaweza kukuingizia hesabu ya shilingi 200,000 kutegemea ukubwa wa gari.
Fuso.jpg



6. Scania

Tunazizungumzia zote aina mbili za kuvuta Trailer (Tractor Unit) na zile za kubeba mchanga yaani Tipper. Manunuzi yake hua juu kidogo ya Fuso tulizoona hapo juu. Uzuri wa hizi ni kwamba zinadumu mda mrefu sana, zinahimili mazingira magumu na zinatengenezeka kwa urahisi zaidi.

Kwa wastani tipper lina urefu wa mita 8.7, wakati zile tractor unit hua na urefu wa mita 6.9. Mara nyingi kuagiza gari hizi huanzia 75,000,000.

Iwapo utaifanya kua gari ya biashara basi kwa siku inaweza kukuingizia hesabu ya shilingi 300,000 kutegemea ukubwa wa gari.
Scania222.jpg


Scania.jpg

Gari za mizigo ni muhimu sana kwa maisha yetu wanadamu kwani hurahisisha ubebaji wa vitu vizito kutoka sehem moja mpaka nyingine hivyo iwapo una uwezo wa kuwekeza katika usafirishaji wa mizigo ya kibiashara au binafsi ni Muhimu sana ukashauriana kuhusu aina ya gari kulingana na bajeti yako pamoja na aina ya kazi unazotaka kufanyia. Kila gari ina uzuri wake kulingana na aina ya matumizi.

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa sim namba 0746267740
 
Vipi kuhusu FAW tipper?
Nazo ni nzuri lakini mara nyingi tunaona ni kwa kazi za mda mfupi. Muda wake wa kuishi haufanani na hizi gari nyingine, kama Scania wala Mitsubishi Fuso.

Hizi uzuri wake ni kua utalipata likiwa jipya na kwa kua Horse Power yake ni ndogo kidogo kwa gari kama Scania hulifanya kutumia mafuta kidogo. Hili sisi haturuhusiwi kuliagiza kwa sababu lina wakala wao ambao n Sino Truck na kwa gharama zao za kila kitu inafika 173,000,0000.
 
Sikuwahi fikiri kama naweza kuagiza scania kwa 75M tu, maana mtaani watu wanakomaa kwa 70 hadi 50M
Kuagiza ni nafuu kidogo. Na pia hizo gari Scania hazishuki thamani kwa haraka kama magari mengine. Gari ambayo sisi tunakuagizia kwa hiyo 75m ukiikuta mtu kaileta ili auze apate faida atakuuzia kwa 90m. Sisi hatuweki faida na hesabu ziko wazi kila hatua, sisi tunalipwa na supllier huko nje
 
Reference Number:19201093249
Make:TOYOTA
Model:LITEACE PICK UP
Body Type:PICK UP
Year of Manufacture:2006
Country:JAPAN
Fuel Type:PETROL
Engine Capacity:1501 - 2000 CC
Customs Value CIF (USD):3,464.00
Import Duty (USD):866.00
Excise Duty (USD):0.00
Excise Duty due to Age (USD):1,299.00
VAT (USD):1,065.43
Custom Processing Fee (USD):20.78
Railway Dev Levy (USD):51.96
Total Import Taxes (USD):3,303.18
Total Import Taxes (TSHS):7,599,683.34
Vehicle Registration Fee (TSHS):500,000.00
TOTAL TAXES (TSHS):8,099,683.34
 
Kwa hiyo Namba Mbili. Hiyo Bei ni kwa aina yoyote ya gearbox auto na manual au zinatofautiana? Na kuna zinakua na double tyre je na hizo bei ni kama uliyoorodhesha hapo?
 
Back
Top Bottom