Fahamu kidogo kuhusu magari ya mizigo nchini Tanzania

Fahamu kidogo kuhusu magari ya mizigo nchini Tanzania

Kwa hiyo No Mbili. Hiyo Bei ni kwa aina yoyote ya gearbox auto na manual au zinatofautiana? Na kuna zinakua na double tyre je na hizo bei ni kama uliyoorodhesha hapo?
Hizo gharama sio fixed boss wangu, nimeweka kutokana na uzoefu wa vile tunavyoziagiza kwamba jumla ya gharama zake huanzia hiyo 14.5, bila kujali ni manual, auto au single au double tyre. Gharama hupanda au kushuka kidogo kulingana na uchache wa kilomita matunzo ya gari na maamuzi ya muuzaji wa Japan
 
Mkuu hiyo Mitsubishi Canter ambayo haibinui huwa zipo pia Automatic?
Zipo boss. Za series ya injini bora ya 4D ni za kutafuta boss, ila nyingi ni series ya injini ya 4M ambazo hazishauriwi sana na mafundi
 
hizi bei ni mpaka na usajili au ?
Ndio boss, hizo ni gharama zote kama vile manumuzi Japan, transfer fee ya kutuma pesa Japan, usafiri, bima ya kutoka Japan, na ukaguzi wa kabla ya kuipandisha gari kwenye meli.

Ikifika bandarini italipiwa vitu kama Ushuru, Wharphage, Shipping Line, Port Charge, Agent Fee, Registration na Plate Number. Baada ya hapo gari itasubiri kukatiwa bima tu ili ianze kutumia barabara zetu.

Hizi gharama hushuka na kupanda kutegemea na gari hadi gari na kwa upande wetu tunaziangalia kwa uwazi ili upate kujua nini unalipia
 
Hongera sana kwa uchambuzi mzuri sana. Vipi kuhusu Totoya Dyna? Hujaziongelea kabisa, zipoje?
Toyota Dyna sifa zake haswa kwenye uimara wa gari ni nzuri zaidi ya Townace au Toyoace, ugumu wa body mpaka injini. Sijaiongelea sababu ni ngumu kuongelea gari zote hapa jambini ntawachosha wasomaji.

Faida yake ya zaida ni kwamba zile za miaka sawa na Townace nyingi zina double cabin japo hii huganta saizi ya bodi la mizigo kupungua kidogo ukilinganisha na Townace
 
Hizo gharama sio fixed boss wangu, nimeweka kutokana na uzoefu wa vile tunavyoziagiza kwamba jumla ya gharama zake huanzia hiyo 14.5,bila kujali ni manual, auto au single au double tyre. Gharama hupanda au kushuka kidogo kulingana na uchache wa kilomita matunzo ya gari na maamuzi ya muuzaji wa Japan
Hivi haiwezekani kupata ambayo haikutumika kabisa(mpya)? Na bei zinakuwaje?
 
Salama naomba garama za townace 4wd na 1500cc
Hizo za Cc 1500 ni adim kidogo kwa miaka ya zamani ambazo ndio zenye unafuu wa bei. Kama hii hapa chini gharama zake zimefika 15.8m ambayo hii ni ya mwaka 1997, zipo za Cc 1500 kwa miaka 2006 na nyingi zaidi ni miaka ya 2012 ambzo kwa wastani manunuzi yake tu bila ushuru ni zaidi ya 20m.
7637C1E4-5F0D-4D05-B8D5-8F40FEB0A94E.jpeg
26722864-CFE4-4AF2-A880-6CC79FD7F834.jpeg
7C34D805-E57D-49BF-962B-3C3086121855.jpeg
44F65B6C-5958-40CC-812E-66476A036452.jpeg

Pata mda wa dk 20 ufike ofisini tuangalie nini cha kufanya ili upate unachotaka na kwa gharama nafuu
 
Hivi haiwezekani kupata ambayo haikutumika kabisa(mpya)? Na bei zinakuwaje?
Mpya unaweza pata boss ila gharama zinakua juu sana ndio sababu hizi gari za mizigo hua tunasubiri wenzetu watumie kwa kua pia zina maisha marefu kidogo

Ukiipata gharama zaweza kufika hata 45,000,000.
 
Toyota Dyna sifa zake haswa kwenye uimara wa gari ni nzuri zaidi ya Townace au Toyoace, ugumu wa body mpaka injini. Sijaiongelea sababu ni ngumu kuongelea gari zote hapa jambini ntawachosha wasomaji. Faida yake ya zaida ni kwamba zile za miaka sawa na Townace nyingi zina double cabin japo hii huganta saizi ya bodi la mizigo kupungua kidogo ukilinganisha na Townace
Zifananishe na Mitsubishi canter basi hizo Toyota Dyna
 
Back
Top Bottom