Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

UPDATE: Ujerumani

Visa vipya 404 pamoja na kifo kipya kimoja (1) vimeripotiwa hii leo nchini humo.

Visa vyote nchini humo vimefikia 4,585 hadi sasa huku vifo tisa (9) vikiripotiwa.

Wagonjwa 46 hadi sasa wameripotiwa kupata ahueni.

Mamlaka za mji mkuu, Berlin na ya jiji la Cologne katika jimbo la North Rhine Westfalia zimetangaza kufungwa baa, vilabu vya starehe, majumba ya sinema na kumbi za matamasha.

Kuanzia sasa hafla yoyote inayohusisha watu 50 au zaidi katika mji wa Berlin imepigwa marufuku.
 
UPDATE: Indonesia

Visa vipya 21 vimeripotiwa hii leo na kufikisha jumla ya visa 117 nchi nzima hadi sasa.

Waliopoteza maisha wafikia watano (5). Waliotibiwa na kupata ahueni wafikia watano (5).

Shule zafungwa kwa muda wa wiki mbili katika mji mkuu Jakarta kutokana na kuhofiwa kuzuka kwa maambukizi zaidi.
 
UPDATE: Ufaransa

Idadi ya visa vyote imefikia 4,499 hadi sasa nchi nzima.

Wagonjwa wapatao 12 hadi hivi sasa wameripotiwa kupata nafuu huku wengine 300 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona (COVID-19) nchini Ufaransa ni 91 hadi hivi sasa.

Ikiwa ni siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa leo hii Jumapili nchini Ufaransa, kuongezeka kwa kasi ya kusambaa kwa virusi vya Corona nchini humo kunaweza kusababisha wapiga kura kuhofia kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Maduka, migahawa na sehemu za burudani kufungwa kuanzia leo Jumapili. Watu takribani milioni 67 wanaoishi nchini humo wametakiwa kubaki katika nyumba zao kama hatua mojawapo ya kusaidia kupambana na virusi vya Corona nchini humo.
 
UPDATE: Marekani

Hadi hivi sasa, visa vipatavyo 2,866 vikiwemo vifo 57 vimeripotiwa nchini Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump ambaye siku chache zilizopita ilitangaza marufuku ya wasafiri kutoka nchi kadhaa za Ulaya kuingia Marekani, sasa marufuku hiyo itazihusu pia Uingereza na Ireland ambazo hapo awali hazikuwemo.

Pia, Rais Trump amefanyiwa vipimo vya COVID-19 na kugundulika kuwa hana maambukizi, ikulu ya Marekani White House imethibitisha kupitia kwa daktari wake.

Trump alifanyiwa vipimo siku ya Ijumaa kama tahadhari baada ya kukaribiana na afisa wa Brazil aliyegundulika hapo baadaye kuwa na maambukizi ya COVID-19.
 
UPDATE: Uhispania

Idadi ya visa vyote nchini humo ni 6,391 hadi hivi sasa.

Waliopoteza maisha nchini humo kutokana na COVID-19 wafikia 196 hadi sasa.

Mpaka sasa, wagonjwa wapatao 517 wametibiwa dalili za COVID-19 na kupata ahueni huku wengine 272 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Begona Gomez, ambaye ni mke wa Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez, amebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Hatua za dharura zimechukuliwa ili kuzuia kuenea zaidi kwa virusi vya Corona. Uhispania inapanga kuweka kizuizi kwa raia wake karibu milioni 46 kuanzia kesho Jumatatu kama sehemu ya mpango wa hali ya dharura wa siku 15 kukabiliana na virusi vya Corona nchini humo.
 
UPDATE: Thailand

Visa vipya 32 vimeripotiwa hii leo nchini humo.

Idadi ya visa vyote nchi nzima ni 114 kikiwemo kifo kimoja (1).

Hadi hivi sasa, wagonjwa wapatao 35 wamekwisha tibiwa dalili za COVID-19 na kupata ahueni.
 
UPDATE: Austria

Visa vipya 145 vimeripotiwa hii leo.

Idadi kamili ya visa vyote nchini Austria ni 800 kikiwemo kifo kimoja (1) pekee.

Waliopata ahueni wafikia sita (6) mpaka sasa.
 
PRESIDENT Uhuru Kenyatta announces two new Covid-19 cases. Declares following measures

1. Restrict travel to Kenya from all countries with reported Corona cases

2. Only Kenyan citizens to be allowed into Kenya provided they go to self quarantine or govt facility. In force for 30 days

3. All persons who’ve come to Kenya in last 14 days must self quarantine

4. Schools suspended with immediate effect. Day schools closed from tomorrow, boarding schools by Wednesday. Universities and colleges by Friday

5. Govt and companies to allow employees to work from home except essential services

6. Use cashless transactions like Mpesa and cards. Appeals for reduced transaction costs from the providers

7. Avoid congregations, weddings, funerals

8. Avoid shopping places and minimize congestion in public transport

9. Limit visitors to hospitals

10. Hospitals and malls encouraged to provide water, soap, sanitizers and ensure regular cleaning and disinfecting places

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom