Tovuti ya Wizara ya Afya Tanzania
https://moh.go.tz/en/
Tovuti ya Shirika la Afya Duniani WHO
Home
Omba kwa Mungu wako unayemuamini akulinde wewe na uwapendao.
Punguza / acha kabisa tabia ya kujishika maeneo ya usoni (macho, pua, mdomo) maana virusi hivyo vya COVID-19 humuingia binadamu kupitia viungo hivyo. Kwa ulazima wa kujishika sehemu hizo, hakikisha umenawa mikono vizuri kwa maji na sabuni.
Punguza / acha kabisa tabia ya kusalimiana kwa kupeana mikono au kukumbatiana.
Epuka mikusanyiko isiyo ya lazima.
Ikitokea mikusanyiko ya ulazima, basi nunua face mask (zinauzwa katika hardwares, maduka ya dawa n.k) kisha kabla ya kuvaa, nawa mikono yako kwa sabuni na maji, kisha ivae ikifunika pua yako na mdomo.
Utokapo katika mikusanyiko au nje ya unapoishi, nawa mikono yako vizuri kwa maji yanayotiririka na sabuni.
Ripoti katika hospitali au ongozi wa unapoishi kama uonapo dalili za ugonjwa huo wa COVID-19 kwako, au kwa mtu unayemfahamu.
Dalili za COVID-19 na taarifa zingine kuhusu ugonjwa huu zinapatikana katika tovuti za Wizara ya Afya Tanzania pamoja na Shirika la Afya Duniani WHO.
Tovuti hizo nimeziambatanisha mwanzo wa comment hii.
Sent using
Jamii Forums mobile app