Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

UPDATE: Maafisa wawili wa ngazi za juu wa tume ya afya ya mkoa wa Hubei nchini China wamefutwa kazi.

Sababu za wawili hao kufutwa kazi bado hazijawekwa wazi.

====

2 top officials of Hubei Province Health Commission removed from office, according to CCTV. Reason unknown.
 
FAHAMU: Idadi ya vifo vipya 108 mpaka sasa viliyoripotiwa hii leo ni idadi kubwa zaidi kuwahi kuripotiwa ndani ya siku moja tangu mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona ulipoanza.
 
Idadi ya vifo vya virusi vya corona yapindukia 1,000 nchini China

Idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa virusi vipya vya corona imeongezeka leo na kupindukia 1,000, wakati Shirika la Afya Ulimwenguni - WHO likionya kuwa watu walioambukizwa na hawajasafiri kwenda China huenda wakawasha moto mkubwa katika janga hilo.

Ongezeko la vifo limekuja baada ya Rais Xi Jinping kufanya ziara isiyo ya kawaida katika hospitali moja ya Beijing, akiwa amevaa vifaa vya kujikinga, na kushauriana na wahudumu wa afya na wagonjwa.

Timu ya mwanzo ya ujumbe wa kimataifa unaoongozwa na WHO imewasili China, wakati nchi hiyo ikipambana kudhibiti virusi hivyo vilivyoambukiza zaidi ya watu 42,000 na kusambaa hadi nchi 25.

Vifo vingine 108 vimeripotiwa leo. Serikali ya China imewazuwia mamilioni ya watu katika miji kadhaa. Serikali kadhaa za kigeni zimepiga marufuku watu kuwasili kutoka China na mashirika makubwa ya ndege yamesitisha safari ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo. [DW]
 
Tofauti na takwimu rasmi nchini China, baadhi ya wanasayansi wamekisia kuwa idadi ya waathirika inaweza kuwa mara 10 zaidi, kwa kuwa wengi wao huonesha dalili polepole, na hawapati matibabu, na hivyo kuwaambukiza wengine.
 
Ripoti zinasema kuwa kuna watu ambao walifariki wakati wa mlipuko wa ugonjwa huo ulipoanza tu, jarida la afya la Lancet linasema kuwa wagonjwa wengi walikufa bila kufahamika kile kilichowauwa.
 
Sasa ni rasmi kuwa ugonjwa wa Corona ni janga la kimataifa, kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.
 
BREAKING: Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuupatia jina jipya ugonjwa mpya unaotokana na virusi vya Corona.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, ugonjwa huo sasa utaitwa COVID-19.
 
UPDATE: The new coronavirus has been named COVID-19 by the Director General of the World Health Organisation, Tedros Adhanom Ghebreyesus.
 


Wazungu wanakiri hawajui kuhusu iko kirusi


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
BREAKING: Mkoa wa Hubei umeripoti vifo vipya 94 pamoja na visa vipya 1,638.
 
UPDATE: Kutokana na ongezeko la vifo 94, jumla ya vifo vyote mpaka sasa kutokana na virusi vya Corona ni 1,112.
 
UPDATE: Katika mkoa wa Hubei pekee, idadi ya vifo imeongezeka mpaka kufikia 1,068.
 
China: Hubei province reporting Feb 11:
  • 1,638 new cases of Covid19 (Total: 33,366)
  • 94 new fatalities (1,068)
  • 417 new discharged (2,639)
  • 26,121 cases remain hospitalized.
 
NEW: Updated coronavirus numbers worldwide;
  • 44,754 confirmed cases
  • 1,112 fatalities
 
Taarifa zaidi kutoka nchini Japan kuhusu meli iliyowekwa karantini (Diamond Princess);

Takribani watu 39 wengine wamebainika kuwa na maambukizi.

Mpaka sasa jumla ya watu 174 katika meli hiyo wamebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

UPDATE: 39 more people diagnosed with coronavirus on cruise ship in Japan, total now to 174.
 
Back
Top Bottom