Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

Ndio ujue Mungu yupo, anaruhusu mitihani na kuacha upenyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani ung'ang'anie kula popo halafu umsingizie Mungu?!Wachina waache kula kila kinachotembea!
pwp3jo2mbwhof5e29ac0d1727f-1.jpeg
 
UPDATE: Kasi ya maambukizi nchini Korea Kusini inazidi kuongezeka

Visa vipya 22 vimeripotiwa nchini humo ukiachana na vile visa 24 vilivyoripotiwa hapo awali. Mpaka sasa jumla ya visa 104 vimeripotiwa nchini humo.
 
UPDATE: Kifo cha kwanza nchini Korea Kusini

Mtu mmoja mwenye miaka ya 60, mwanamume, aliyekuwa amelazwa hospitalini kwa matibabu ya ugonjwa mwingine.

Wagonjwa wengine kadhaa katika hospitali pia wamethibitika kuwa na virusi vya COVID-19.
 
UPDATE: Meli ya Diamond Princess

Visa vipya 13 vimeripotiwa katika meli hiyo na kufikisha jumla ya visa 634 huku vifo vikiwa ni viwili (2) hadi hivi sasa.

image.jpg
 
Hivi bro ukisema takwimu na khali khalisi nashindwa kuelewa apo mkuu..

Sent using Jamii Forums mobile app
Takwimu ama ripoti rasmi ni kile kinachotangazwa na mamlaka za maeneo husika (mamlaka za afya/serikali za mikoa/taifa n.k.).

Hali halisi ni kile kilichopo katika mazingira halisi kwa ujumla wake katika maeneo husika.
 
NEWS ALERT: South Korea told 2.5M people in the city of Daegu to stay indoors because of the coronavirus. Almost 50 of the new cases there are linked to a single infected woman.
 
FAHAMU: "Super-spreaders" ni kina nani na wanafanya nini?

Neno hili ni maarufu hususani kipindi hiki na limekuwa likitumika pale ambapo watu kadhaa wanapopata maambukizi ya virusi vya Corona kupitia chanzo kimoja ama mtu mmoja.

Chanzo hicho hutajwa kama "Super-spreader".

Kutokana na utofauti wa kiafya na kibiolojia, Super-spreader anatajwa kuwa na uwezo wa kueneza zaidi ugonjwa ama virusi kuliko watu wengine, kwa watu wengi zaidi ingawa wataalamu wa masuala ya virusi wanadai kuwa bado hakuna uthibitisho wa kutosha kuhusiana na hilo.
 
FAHAMU: "Super-spreaders" (muendelezo)

Profesa Christl Donnelly wa masuala ya kitabibu (Epidemiology) wa Imperial College London anasema;

"Binadamu hatupo sawa. Tunatofautiana katika kinga zetu za mwili, tabia na mahali tulipo. Vitu hivi vyote vyaweza kuchochea idadi ya watu tunaoweza kuwaambukiza magonjwa. Hivyo basi, sababu za kitabia na kibiolojia zinaweza kuchochea lakini pia muda na mahali tulipo."
 
NEWS ALERT: Iraqi heath ministry recommends travel ban to and from Iran after coronavirus deaths. [MEE]
 
Kuna taarifa zisizo rasmi kwamba, visa vya COVID-19 nchini Iran vimefikia 60 huku baadhi ya vyanzo vikidai uwepo wa vifo vinane (8) mpaka tisa (9) nchini humo hadi hivi sasa.

Bado naendelea kuzifuatilia taarifa hizi.
 
Aiseee!
Kuna taarifa zisizo rasmi kwamba, visa vya COVID-19 nchini Iran vimefikia 60 huku baadhi ya vyanzo vikidai uwepo wa vifo vinane (8) mpaka tisa (9) nchini humo hadi hivi sasa.

Bado naendelea kuzifuatilia taarifa hizi.
 
UPDATE: South Korea

A soldier in the South Korean military has been confirmed to have the coronavirus. He visited his hometown Daegu from February 13 to 18. Daegu has had dozens of virus cases confirmed in the last two days.
 
Back
Top Bottom