Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)

CORONA INAUSOGEZA ULIMWENGU KWENYE NADHARIA YA MWISHO WA DUNIA

VIRUSI vya Corona ni sehemu ya kundi la virusi ambavyo husababisha maradhi kwa mamalia na ndege. Virusi hivyo hushambulia njia ya upumuaji, hivyo kumsababisha mwathirika hali ya kikohozi, mafua, homa kali, upumuaji wa shida na hali ikizidi mgonjwa hupata nimonia.

Virusi vya Corona mara nyingi humsababishia mwathirika hali ya mafua ya kawaida (common cold), ila katika kesi chache, hufanya mashambulizi makali na hata kusababisha kifo.

Mpaka sasa virusi vya Corona ambavyo ni hatari sana na kusababisha kifo vipo katika aina nne; SARS, MERS, COVID-19 na NCOV.

SARS (Severe Acute Respiratory Syndrome), ni homa ya mafua makali kutokana na Virusi vya Corona. SARS ilipogundulika Novemba 2002, Kusini ya China, kesi zaidi ya 8,000 ziliripotiwa na watu 774 waliripotiwa kufariki dunia kutokana na SARS. Kati ya Novemba 2003 na Julai 2003, SARS iliripotiwa kufika katika 17 duniani. Tangu mwaka 2004 hakuna mgonjwa mwingine wa SARS aliyeripotiwa.

Hata hivyo, mwaka 2017, wanasayansi waligundua virusi vya Corona vyenye kusababisha SARS kwenye popo, jimbo la Yunnan, China.

MERS (Middle East Respiratory Syndrome), au kwa umaarufu ni Homa ya Camel. Ukiita Mafua ya Mashariki ya Kati sio vibaya. MERS ni ugonjwa wenye kusababishwa na Virusi vya Corona. Uligundulika kwa mara ya kwanza Saudi Arabia mwaka 2012 na mpaka mwaka 2017, kesi takriban 2000 zilisharipotiwa. Asilimia 36 ya watu walioripotiwa kupata maambuziki ya MERS walifariki dunia.

COVID-19 (Coronavirus Disease 2019). Hili ndilo janga jipya linaloitesa dunia kwa sasa. Ni mwendelezo uleule wa mashambulizi makali ya Virusi vya Corona.

COVID-19 kama ilivyo kwa virusi vingine vyote vya Corona, asili yake ni maambukizi kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

NCOV (Novel Corona Viruses), kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), Januari 21, mwaka huu, mgonjwa wa kwanza mwenye NCOV aligundulika Jamhuri ya Korea (Korea Kusini). Aliyegundulika ni mwanamke raia wa China mwenye umri wa miaka 35. Mkazi wa Wuhan, Hubei, China.

Kwa kifupi, Virusi vya Corona vipo kwenye kundi la Zoonotic, asili yake ni wanyama. Zoonotic au Zoonosis ni maambuzi ya kibakteria, virusi na pasarasaiti, kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

Kutoka kwa binadamu mmoja hadi mwingine, Virusi vya Corona hambukizwa kwa njia ya hewa. Mtu mwenye Corona akikohoa jirani na asiyekuwa na virusi hivyo, kisha asiyekuwa navyo akivuta hewa ndani, uwezekano wa kupata maambukizi ni mkubwa. Njia hiyo inaitwa respiratory droplets.

Njia ya pili ambayo inaelezwa na wataalamu mbalimbali duniani ni kugusana au kukaribiana kwa angalau futi sita na mwathirika wa Virusi vya Corona. Uwezekano wa maambukizi ni zaidi ya asilima 50.

CORONA INAVYOENEA

Mpaka jana (Machi 12), watu zaidi ya 125,000 walikuwa wameshaambukizwa COVID-19 katika nchi 80 duniani. Kati ya hao, watu 4,600 walishafariki dunia. Watu 68,000 wameripotiwa kupona COVID-19 duniani kote. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Kituo cha Sayansi cha Chuo Kikuu cha John Hopkins, kilichopo Baltimore, Maryland, Marekani.

Mpaka sasa hakuna kinga wala tiba ya COVID-19. Kwa mujibu wa madaktari wa China ambako maambukizi ni makubwa na vifo ni vingi, kupona kwa mgonjwa mwenye COVID-19, hutegemea uimara wa kinga za mwili wa mwathirika.

Kwamba idadi kubwa ya watu wanaopona COVID-19 wanabebwa na uimara wa kinga zao kuliko matibabu wanayopatiwa. Na hilo ni angalizo kuwa kwa mtu ambaye kinga za mwili wake zina shaka au anaumwa maradhi mengine, anapoambukizwa COVID-19, uwezekano wa kupona ni mdogo sana.

ATHARI YA KIUCHUMI

Taasisi ya utafiti ya Brookings ya Marekani, imetoa taarifa ya jinsi biashara ya mafuta ulimwenguni inavyopitia kwenye kipindi kigumu.

Jukwaa la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD), limetoa taarifa kuwa COVID-19, imesababisha anguko la kiuchumi ulimwenguni kwa dola trilioni moja (zaidi ya ya Sh2,300 trilioni) mpaka sasa. Hiyo ni hesabu ya mwaka huu, yaani kipimo cha kuanzia Januari 2020.

UNCTD wameongeza kuwa kasi ya kutanuka kwa maambukizi ya COVID-19 na tahadhari kubwa zinazochukuliwa kati ya nchi na nchi ili kujikinga na maambukizi mapya, inaelekea kuisababishia dunia anguko la kiuchumi la dola trilioni 2 (Sh4,600 trilioni).

Kwa mujibu wa UNCTAD, anguko la uchumi duniani linalosababishwa na kasi ya kusambaa kwa COVID-19, linaulekeza ulimwengu kwenye Nadharia ya Mwisho wa Dunia (Doomsday Theory), inayoeleza kuwa dunia itakuwa ukingoni pale ukuaji wa uchumi duniani utakapofikia asilimia 0.5.

Hadi sasa, ukiachana na athari kubwa ya biashara ya mafuta, kwa jumla, biashara za uagizaji na usafirishaji (importation and exportation), imeshuka kwa kiasi kikubwa ulimwenguni.

Hata hapa Tanzania, vilio ni vingi sana. Kariakoo wafanyabiashara wenye kutegemea bidhaa kutoka China wanaumia. Bidhaa zinakwisha lakini hawawezi kuagiza.

Kampuni za usafirishaji mizigo (logistics) kati ya Tanzania na China au nchi yoyote iliyowekwa kwenye karantini kwa sababu ya COVID-19, zipo kwenye sintofahamu, kazi zimesimama. Uchumi unasimama.

Kwa vile Kariakoo imekuwa ikitumika kama kituo kikuu cha manunuzi ya jumla hasa mavazi kwa nchi karibu zote za Maziwa Makuu, na kwa vile biashara za Kariakoo zinategemea China, na kwa kuwa China hakuendeki kwa sasa, mpaka hapo unaweza kupata picha kubwa ya namna uchumi wa dunia unavyopitia kupindi kigumu.

Hali ndio ipo hivyo karibu kila nchi ya Afrika, maana biashara nyingi za bidhaa Afrika zinategemea China kwa kiasi kikubwa. Hali inaendelea hivyo duniani kote, uagizaji na usafirishaji bidhaa nje ya nchi vimesitishwa katika mataifa mengi.

Uchumi wa michezo ni zahama. Mpaka sasa ligi kubwa tano kwenye nchi tano za Ulaya zimesimamishwa. Kutoka England mpaka Hispania. Ufaransa hadi Ujeruma. Italia pia.

Kabla ya hapo, ilishashuhudiwa baadhi ya michezo ikichezwa bila mashabiki. Lengo likiwa kuchukua tahadhari juu ya maambukizi ya COVID-19.

Baraza la Vyama vya Soka Ulaya (Uefa), limeahirisha mechi za mashindano yake ya Klabu Bingwa Ulaya na Europa League, lengo ni lilelile, tahadhari dhidi ya COVID-19. Wakati uamuzi huo ukitolewa, tayari baadhi ya wachezaji na makocha walikuwa wameshaambukizwa.

Chama cha Mpira wa Kikapu Marekani (NBA), kimeahirisha msimu wa mashindano ya NBA baada ya mchezaji Rudy Gobert, kukutwa na maambukizi. Gobert anachezea timu ya Utah Jazz ambayo ni memba wa Conference ya Magharibi.

Mapendekezo yametolewa kwa Ligi ya American Football (NFL) kusogezwa mbele, na wakati huohuo michezo ya vijana chini ya umri wa miaka 16, imefutwa na haitachezwa tena. Ni kwa sababu COVID-19 imekuwa tishio la dunia.

Nchi za Ulaya, inaelezwa maduka yanabaki tupu. Bidhaa zinakwisha, watu wananunua kwa wingi na kuhifadhi ndani kusudi wasitoke nje kukwepa COVID-19. Bahati mbaya zaidi, bidhaa hasa za chakula zimegeuka adimu. Hofu ya watu kukosa chakula ni kubwa.

Dunia inachapika mno kiuchumi. Taa nyekundu inawaka kuelekea kwenye poromoko la kiuchumi kwa thamani ya dola 2 trilioni. Tusiombee ufike wakati uchumi uwe unakua kwa kasi ya asilimia 0.5. Ikifika hapo ni kutimia kwa nadharia ya mwisho wa dunia, yaani Doomsday Theory.

Tuombe maambukizi yasiendelee kwa kasi iliyopo. Ni hatari mno kiuchumi. Tuombe udhibiti kwa wagonjwa wenye COVID-19, wapone bila kuambukiza wengine.

Ndimi
Luqman Maloto mwandishi
 
Nimetumiwa video na rafiki yangu alieko moshi .....je serikali inaficha kuhusu ugonjwa mbona hawasemi kama kuna cases kama hizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa taarifa nzuri ila sijaelewa hapa uchumi ukiwa 0.5 unawezaje kusababisha dunia kuwa mwisho yan naomba kujua ss uhusiano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ongera kwa kutujuza nikisikia tu umefika apo Kenya nitaenda kujichimbia kusiko julikana na familia yangu na vyakula vya miaka angalau 2!
Bila shaka ushaenda kujichimbia kusikojulikana mana ushapiga hodi Nairobi
 
UPDATE: Visa vipya 107 na vifo vipya vitano (5) nchini Korea Kusini.

Hadi hivi sasa nchini humo;
  • Visa 8,086 vimethibitishwa
  • Vifo 72 vimeripotiwa
  • Wagonjwa 36 wako mahututi
  • Wagonjwa 714 wamepata ahueni
 
Bila shaka ushaenda kujichimbia kusikojulikana mana ushapiga hodi Nairobi
Mkuu apa tuna waza kuna vyakula vingine vina kuwa vigum kuvi hifadhi kwa mda mrefu sehemu yenyewe umeme haujafika hakuna maakazi ya watu karibu solar ya Ku charg simu na mwanga ipo ila net shidah!!
Nipe mbinu mbadala mkuu ipo sehemu nyingine ila tiari ni maakazi ya muda mrefu watu ni wengi tuna hisi hapo hapata kuwa salama!!!
 
Just don't panic yet...wakati wa kuwa na wasiwasi uliopitiliza bado haujafika kwetu

Na kama ikitokea basi hifadhi nafaka na mboga yoyote iliyo jamii ya mikundekunde (mbaazi, choroko, maharage n.k)...

Vitu kam viazi, ndizi, mbogamboga,samaki unaweza hifadhi kwa kuzikausha na jua kwa muda mrefu au moshi...

Nyanya unaweza ukaziosha uzuri na ukazihifadhi ndani ya mafuta ya kupikia...

Mkuu shukran bila shaka mawazo yako yata wapa wengi mwanga sio mawazo madogo!!
 
UPDATE: Italia

Visa 17,660 vimethibitishwa nchi nzima hadi hivi sasa.

Vifo 1,266 hadi sasa vimehusishwa na COVID-19 nchini humo.

Wenye ahueni wafikia 1,439 huku 1,328 hakiwa katika hali mbaya zaidi.

Nchi nzima yawekwa kizuizini, shughuli mbalimbali za kijamii zasitishwa, maduka, migahawa n.k. yafungwa.
 
UPDATE: Iran

Visa 11,364 vimethibitishwa nchi nzima hadi hivi sasa.

Vifo 514 vimehusishwa na COVID-19 nchini humo hadi hivi sasa.

Waliopata ahueni wafikia 3,529 huku kukiwa na uwezekano wa visa vipya kuongezeka zaidi.
 
Kutoka kwa mdau humu #Jf habari inasema...Pia Habari zisizo rasmi zinasema kitu huenda tayari kimetinga Moshi kupitia KIA.
Ni suala la muda tu ili itifaki ya WHO ifuatwe ili kutoa taarifa rasmi. Binafsi bado ninaamini matokeo yatakuwa Negative.

Maajabu ni kwamba hospitali ya uangalizi kwa washukiwa wa ugonjwa huo ipo Moshi mjini, katikati ya mji. Na inadaiwa washukiwa wote wameletwa wakisindikizwa na ambulance tatu, gari ya polisi wenye bunduki kutokea KIA nk. Sasa sijui elimu ya kupambana na huo ugonjwa ni upuuzi mtupu kwa wahusika. Why such movement from KIA with dozen of people?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UPDATE: Uhispania

Mpaka kufikia sasa, jumla ya visa 5,232 pamoja na vifo vipatavyo 133 vimeripotiwa nchi nzima.

Idadi ya waliopata ahueni imefikia 193 huku wagonjwa wapatao 272 wakiwa katika hali mbaya zaidi.

Nchi hiyo imetangaza hali ya hatari kufuatia kuongezeka zaidi kwa maambukizi ya COVID-19 nchini humo.
 
Kutoka kwa mdau humu #Jf habari inasema...Pia Habari zisizo rasmi zinasema kitu huenda tayari kimetinga Moshi kupitia KIA.
Ni suala la muda tu ili itifaki ya WHO ifuatwe ili kutoa taarifa rasmi. Binafsi bado ninaamini matokeo yatakuwa Negative.

Maajabu ni kwamba hospitali ya uangalizi kwa washukiwa wa ugonjwa huo ipo Moshi mjini, katikati ya mji. Na inadaiwa washukiwa wote wameletwa wakisindikizwa na ambulance tatu, gari ya polisi wenye bunduki kutokea KIA nk. Sasa sijui elimu ya kupambana na huo ugonjwa ni upuuzi mtupu kwa wahusika. Why such movement from KIA with dozen of people?

Sent using Jamii Forums mobile app
Si unajua akili zetu zilivyo, ikitokea ajali wangapi wanasogelea mahali pa ajali? ni wengi tu, sasa kibongo bongo wakisikia kuna wagonjwa wa Corona watasogea wengi na maambukizi yatazidi ndo usalama unahitajika!
 
Nimetumiwa video na rafiki yangu alieko moshi .....je serikali inaficha kuhusu ugonjwa mbona hawasemi kama kuna cases kama hizi
View attachment 1387600

Sent using Jamii Forums mobile app
Kutoka kwa mdau humu #Jf habari inasema...Pia Habari zisizo rasmi zinasema kitu huenda tayari kimetinga Moshi kupitia KIA.
Ni suala la muda tu ili itifaki ya WHO ifuatwe ili kutoa taarifa rasmi. Binafsi bado ninaamini matokeo yatakuwa Negative.

Maajabu ni kwamba hospitali ya uangalizi kwa washukiwa wa ugonjwa huo ipo Moshi mjini, katikati ya mji. Na inadaiwa washukiwa wote wameletwa wakisindikizwa na ambulance tatu, gari ya polisi wenye bunduki kutokea KIA nk. Sasa sijui elimu ya kupambana na huo ugonjwa ni upuuzi mtupu kwa wahusika. Why such movement from KIA with dozen of people?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumekuwa na taarifa nyingi sana kuhusiana na hili janga; uwepo wa visa, watu kushukiwa, watu kufa n.k. lakini mara nyingi taarifa hizo zimekuwa zikikanushwa.

Uwezo wa kubaini uwepo wa visa hivyo nchi nzima ni changamoto kubwa kwa mataifa mengi katika hatua za kukabiliana na COVID-19.

Kuchukua tahadhari ndiyo njia pekee inayobaki lakini bado pia kuna changamoto kubwa kuhusiana na hilo.

Kuna uwezekano huo wa kuwepo kwa visa na pia kinyume chake ingawa ni ngumu sana kusema kinyume chake kutokana na muingiliano wa kimipaka kati ya nchi na nchi, watu na watu, bado ni mkubwa.
 
UPDATE: Ujerumani

Visa vyote nchini humo vimefikia 3,675 hadi sasa huku vifo nane (8) vikiripotiwa.

Wagonjwa 46 wameripotiwa kupata ahueni.

Ujerumani itaanza kuzifunga shule zake nyingi kuanzia siku ya Jumatatu ijayo baada ya jimbo la North Rhine Westphalia kuungana na jimbo la Bavaria, Baden-Wuttemberg na majimbo mengine kutangaza kuzifunga shule.

Majimbo kumi kati ya 16 tayari yametangaza kuzifunga shule kama sehemu ya mkakati wa kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona.
 
UPDATE: Marekani

Mpaka kufikia sasa, jumla ya visa 2,599 vimeripotiwa nchi nzima.

Vifo vipatavyo 47 vimeripotiwa hadi hivi sasa.

Rais Donald Trump ametangaza hali ya dharura kutokana na kuenea kwa virusi vya Corona, pamoja na upatikanaji wa karibu dola bilioni 50 kama msaada zaidi wa kupambana na ugonjwa huo.
 
Back
Top Bottom