Fahamu kinachosababisha asali kuganda?

Fahamu kinachosababisha asali kuganda?

Fred Katulanda

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2011
Posts
380
Reaction score
550
Kumekuwa na maswali mengi kutoka kwa watumiaji asali ambao wengi wamekua wakiuliza kutaka kujua kama asali iliyoganda ni nzuri au imechakachuliwa. Wengine wamekua wakiamini asali iliyoganda imechanganywa na sukari guru.

Lakini hata baadhibya wafugaji na wauza asali pia wamekua wakiogopa kuiuza asali iliyoganda kwa Imani wateja wataikataa hivyo baadhi yao kujikuta wakipata hasara na wengine kuianikanjuani saa chache mteja anapokuja kuiona.

Kupitia Makala haya fupi Leo nakuja na sababu za asali kuganda, na kukufafanulia nini hasa husababisha Asali igande kitalaamu.

Sasa, ili uelewe vyema sababu ni lazima utambue kuwa nyuki anapoitengeneza asali dani yake huwa kuna sukari ambayo huipata kutokana na malighafi anazotumia kutengenezea asali hiyo.

Kitalaamu nyuki hutengeneza asali kwa kuchukua Pollen (Chavua) na Nectar (Mbochi), kutoka katika chanzo mbalimbali cha mimea. (Nectar ni majimani yenye utamu ya maua na Pollen ni unga wa maua).

Sasa malighafi hizi mbili hutengenezwa Kitalaamu na nyuki kwa pamoja na kuchanganywa (kusindikwa) na kuwa asali ambao kiasili huwa ni chakula cha ziada ambacho nyuki wao hukiandaa ili kukitumia kwa chakuka wakati ambao mvua zimekatika na mimea haitoi maua tena.

Kwa kawaida mchakato mzima wa nyuki unapokamilika na kuifanya asali kuiva ndani yake huwa na mchanganyiki wa sukari kuu za aina mbili ambazo ni;

(a). Fructose
(b). Glucose

Sasa wakati nyuki wakitembea na kuchukua Pollen ya maua kwa ajili a kutengenezea asali na wakapata Pollen nyingi ya maua yenye sukari nyingi aina ya Fructose zaidi ya Glucose basi asali hii haitokuwa na tabia ya kuganda.

Lakini ilitokea nyuki akachukua Pollen yenye kiasi kingi cha Glucose kuliko fructose basi asali itakayozalishwa na nyuki wa aina hii mara nyingi huwa na tabia kuganda.

Kwa maekezo yangu hayo, kuganda kwa asali siyo Jambo baya sababu inatokana na aina ya sukari iliyopatikana kwenye malighafi zake.

Jambo lingine muhimu ni kuwa; asali hiyo ikiganda hutengeneza chengachenga nyingi ziitwazo Crystallize. Asali hii kidogo husumbua watumiaji hivyo ukitakankuitumia ni lazima uiweke kwenye jua au majibya Moto ndiyo iyeyuke Kwa ajili ya kuitumia lakini siyo mbaya.

Zingatio: Asali ikiganda iangalie umepanda yote ndaniya chombo, lakini kama imeganda nusu tu, ndani chini na juu inaonekana haijaganda basi hiyo inauwezekano kuwa imechanganywa na kitu na siyo asali nzima.

Asanteni unaweza kuwasiliana nami kwa elimi zaidi. +255622 642620 au +255784 642620.

Pia unawaza kusoma Makala zangu nyingine za ufugaji nyuki hapahapa jamiiforums kama zifuatazo;

1.Utegaji nyuki waingie katika mizinga
2.Uvunaji wa Sumu ya Nyuki
3.Fahamu mbinu za kugawa makundi ya nyuki kwenye mizinga mpya

Screenshot_20210927-081852~2.png

Screenshot_20210927-081946~2.png
 
Shukran kwa elimu mujarrab, wengi wetu tusoijua vyema asali huwa tunawaza kupigwa tu.
Pia unawaza kusoma Makala zangu nyingine za ufugaji nyuki ili upate madini zaidi hapahapa jamiiforums kama zifuatazo;

1.Utegaji nyuki waingie katika mizinga
2.Uvunaji wa Sumu ya Nyuki
3.Fahamu mbinu za kugawa makundi ya nyuki kwenye mizinga mpya
 
Mkuu naomba kuuliza,
Asali hukaa muda gani wa matumizi kabla haijaharibika?
Pia ningependa kujua njia bora ya kuihifadhi home ni ipi?
 
Asali inaweza kukaa au kuhifadhiwa zaidi hata ya miaka 100, lakini lazima ihifadhiwe vizuri.

Hali kuu inayoathiri ubora wa asali ni joto kali hivyo wakati wa kuhifadhi asali lazima iwekwe kwenye chombo kisafi kisicho na maji na owe asali iliyovunwa ukiwa imekomaa, hii inaweza kuhifadhiwa hata miaka 100. Lakini ikivunwa haijakomaa haiwezi kukaa zaidi kwani inaweza hata kuchacha sababu inakuwa na kiwango kikubwa cha maji yaliyowekwa na nyuki wenyewe siyo ya kuongeza na binadamu.

Kipimo cha joto kinachofaa kuhifadhi asali kwa joto kati ya -5 ° C na + 20 ° C. Likizidi 40 ni hatati kwa Asali japo itabaki na utamu wake lakini haitokuwa na faida zake yaani baadhi ya Enzymes na vitamini.

Ushauri wangu;
Kwa mikoa yenye joto kipindi kirefu asali iwekwe kwenye dumu la plastiki na kufunikwa vyema lakini dumu liwekwe chini ya sakafu au vigae maana husaidia ubaridi ambao hubalance na hali ya hewa ya joto hivyo kuifanya kudumu muda mrefu zaidi.
 
Hali kuu inayoathiri ubora wa asali ni joto kali hivyo wakati wa kuhifadhi asali lazima iwekwe kwenye chombo kisafi kisicho na maji na owe asali iliyovunwa ukiwa imekomaa, hii inaweza kuhifadhiwa hata miaka 100. Lakini ikivunwa haijakomaa haiwezi kukaa zaidi kwani inaweza hata kuchacha sababu inakuwa nankiwanho kikubwa cha maji yaliyowekwa na nyuki wenyewe siyo ya kuongeza na binadamu.

Kilimo cha joto kinachofaa kuhifadhi asali kwa joto kati ya -5 ° C na + 20 ° C. Likizidi 40 ni hatati kwa Asali japo itabaki na utamu wake lakini haitokuwa na faida zake yaani baadhi ya Enzymes na vitamini.

Ushauri wangu;
Kwa mikoa yenye joto kipindi kirefu asali iwekwe kwenye dumu la plastiki na kufunikwa vyema lakini dumu liwekwe chini ya sakafu au vigae maana husaidia ubaridi ambao hubalance na hali ya hewa ya joto hivyo kuifanya kudumu muda mrefu zaidi.
Asante sana Mkuu.
 
Asali inaweza kukaa au kuhifadhiwa zaidi hata ya miaka 100, lakini lazima ihifadhiwe vizuri.

Hali kuu inayoathiri ubora wa asali ni joto kali hivyo wakati wa kuhifadhi asali lazima iwekwe kwenye chombo kisafi kisicho na maji na owe asali iliyovunwa ukiwa imekomaa, hii inaweza kuhifadhiwa hata miaka 100. Lakini ikivunwa haijakomaa haiwezi kukaa zaidi kwani inaweza hata kuchacha sababu inakuwa na kiwango kikubwa cha maji yaliyowekwa na nyuki wenyewe siyo ya kuongeza na binadamu.

Kipimo cha joto kinachofaa kuhifadhi asali kwa joto kati ya -5 ° C na + 20 ° C. Likizidi 40 ni hatati kwa Asali japo itabaki na utamu wake lakini haitokuwa na faida zake yaani baadhi ya Enzymes na vitamini.

Ushauri wangu;
Kwa mikoa yenye joto kipindi kirefu asali iwekwe kwenye dumu la plastiki na kufunikwa vyema lakini dumu liwekwe chini ya sakafu au vigae maana husaidia ubaridi ambao hubalance na hali ya hewa ya joto hivyo kuifanya kudumu muda mrefu zaidi.
Shukran kwa elimu mkuu juu ya asali swali langu asali ni nyeupe inatokana na nini ?
 
Rangi ya asali, kuwa nyekundu, nyeusi au yoyote hutokana na malighafi anayopata nyuki kutengeneza asali, akipata Pollen nyingi za njano asali itakuwa na mng'ao kama gold lakini akipata nyekundu asali itakuwa nyusi kiasi n.k.

Ila rangi haiathiri ubora hata ingekuwa nyusi, bado ubora wake ni uleule.

Bee-pollen-supplements.jpeg

Pollen nyekundu hii.

bee-pollan-250x250.jpg

Pollen ya njano.

Sasa unaweza kuona unapata asali gani Nyuki akipata Pollen ya kikaoni. Nakuwekea hapa picha za asali za rangi tofauti kutiana na pollen ya Maia wanayopata.

rtr38tuq.jpg

59940.jpg

mad-honey.jpg
 
Asantee mkuu kwa elimu vp kuhusiana kutofautiana kiwanga cha fructose na glucose akina effect kwenye rangi?
Rangi ya asali, kuwa nyekundu, nyeusi au yoyote hutokana na malighafi anayopata nyuki kutengeneza asali, akipata Pollen nyingi za njano asali itakuwa na mng'ao kama gold lakini akipata nyekundu asali itakuwa nyusi kiasi n.k.

Ila rangi haiathiri ubora hata ingekuwa nyusi, bado ubora wake ni uleule.

View attachment 1998535
Pollen nyekundu hii.

View attachment 1998539
Pollen ya njano.

Sasa unaweza kuona unapata asali gani Nyuki akipata Pollen ya kikaoni. Nakuwekea hapa picha za asali za rangi tofauti kutiana na pollen ya Maia wanayopata.

View attachment 1998543

View attachment 1998547

View attachment 1998553
 
Shukrani kwa ufafanuzi mzuri, ningependa kujua faida na utofauti wa asali inayotokana na nyuki wadogo na ile inayotokana na nyuki wakubwa. Asante.
 
Tofauti ya Asali ya Nyuki Wadogo na Nyuki Wakubwa:

Ubora:

Asali zote zinatayarishwa kwa namna moja na nyuki lakini kuna tofauti kidogo ya ubora ambayo hutokana na Maia ambayo Nyuki Wakubwa wanafika na nyuki Wadogo pia wanafika. Kimsingi hii ndiyo huleta tofauti ya Asali hizi na hata kusababisha kuwa na ladha tofauti.

Asali ya NYUKI WAKUBWA na WADOGO zinatofautiana katika mambo kadhaa ambayo nitakutajia.

NYUKI WADOGO
Tofauti na ilivyo kwa nyuki wakubwa, aina hii ya nyuki ni kundi dogo sana katika jamii ya wadudu wanaozalisha asali.

Nyuki hawa wana umbo dogo sana na rangi nyeusi, uzalishaji wao huwa ni mdogo ukilinganisha na aina nyinginezo za nyuki.

Aina hii ya nyuki tofauti na ilivyo kwa nyuki wakubwa, majike yote huzaa, huku madume yakifanya kazi kama nyuki wengine, ambapo nyuki jike huleta malighafi na madume hufanya kazi ya kujenga.

Kazi ya kuzalisha asali kwa nyuki hawa wadogo, hufanywa kwa ushirikiano wa wote bila kubaguana.

Asali inayotokana na nyuki hawa, ina aina nyingi zaidi za virutubisho kwa kuwa huweza kupata chavua kutoka katika aina nyingi zaidi za maua kwani hufikia hata kwenye maua madogo zaidi ambayo nyuki wakubwa hawawezi kuingia kwa ajili ya ukubwa wao kupata chavua (Pollen) ambayo hutumika kutengeneza asali.

1 – Ni nyepesi zaidi kwani ina kiwango cha maji kuanzia asilimia 24

2 – Ina ladha ya UCHACHU kama yenye limao ingawa ni tamu pia

3 – Mara nyingi ina rangi ya KAHAWIA ILIYOKOLEA iwakati mwingine huwa kahawia WEUSI

NYUKI WAKUBWA

1 – Asali yake ni nzito kuliko ya nyuki wadogo kwani ina kiwango cha maji kuanzia asilimia 17 hadi 20.

2 – Ni tamu moja kwa moja bila kua na ladha ya uchachu kama nyuki wadogo

3 – Ina rangi nyingi kuanzia NYEKUNDU, NJANO, KAHAWIA ILIYOPOA, KAHAWIA ILIYOKOZA kutegemeana na upatikanaji wa maua kama nilivyoeleza hapo juu kuhusu rangi.
 
Shukrani kwa maelezo yaliojitosheleza na hapa nimepata uelewa kwanini asali ya nyuki wadogo ni bei yake ni kubwa kutokana na ubora pia upatikanaji wake.
 
Kwanini huwa Wana pika(kuchemsha) Asali ?, na utaijuaje kama asali imepikwa. Shukrani Kwa ilimu mkuu
Kumekuwa na maswali mengi kutoka kwa watumiaji asali ambao wengi wamekua wakiuliza kutaka kujua kama asali iliyoganda ni nzuri au imechakachuliwa. Wengine wamekua wakiamini asali iliyoganda imechanganywa na sukari guru.

Lakini hata baadhibya wafugaji na wauza asali pia wamekua wakiogopa kuiuza asali iliyoganda kwa Imani wateja wataikataa hivyo baadhi yao kujikuta wakipata hasara na wengine kuianikanjuani saa chache mteja anapokuja kuiona.

Kupitia Makala haya fupi Leo nakuja na sababu za asali kuganda, na kukufafanulia nini hasa husababisha Asali igande kitalaamu.

Sasa, ili uelewe vyema sababu ni lazima utambue kuwa nyuki anapoitengeneza asali dani yake huwa kuna sukari ambayo huipata kutokana na malighafi anazotumia kutengenezea asali hiyo.

Kitalaamu nyuki hutengeneza asali kwa kuchukua Pollen (Chavua) na Nectar (Mbochi), kutoka katika chanzo mbalimbali cha mimea. (Nectar ni majimani yenye utamu ya maua na Pollen ni unga wa maua).

Sasa malighafi hizi mbili hutengenezwa Kitalaamu na nyuki kwa pamoja na kuchanganywa (kusindikwa) na kuwa asali ambao kiasili huwa ni chakula cha ziada ambacho nyuki wao hukiandaa ili kukitumia kwa chakuka wakati ambao mvua zimekatika na mimea haitoi maua tena.

Kwa kawaida mchakato mzima wa nyuki unapokamilika na kuifanya asali kuiva ndani yake huwa na mchanganyiki wa sukari kuu za aina mbili ambazo ni;

(a). Fructose
(b). Glucose

Sasa wakati nyuki wakitembea na kuchukua Pollen ya maua kwa ajili a kutengenezea asali na wakapata Pollen nyingi ya maua yenye sukari nyingi aina ya Fructose zaidi ya Glucose basi asali hii haitokuwa na tabia ya kuganda.

Lakini ilitokea nyuki akachukua Pollen yenye kiasi kingi cha Glucose kuliko fructose basi asali itakayozalishwa na nyuki wa aina hii mara nyingi huwa na tabia kuganda.

Kwa maekezo yangu hayo, kuganda kwa asali siyo Jambo baya sababu inatokana na aina ya sukari iliyopatikana kwenye malighafi zake.

Jambo lingine muhimu ni kuwa; asali hiyo ikiganda hutengeneza chengachenga nyingi ziitwazo Crystallize. Asali hii kidogo husumbua watumiaji hivyo ukitakankuitumia ni lazima uiweke kwenye jua au majibya Moto ndiyo iyeyuke Kwa ajili ya kuitumia lakini siyo mbaya.

Zingatio: Asali ikiganda iangalie umepanda yote ndaniya chombo, lakini kama imeganda nusu tu, ndani chini na juu inaonekana haijaganda basi hiyo inauwezekano kuwa imechanganywa na kitu na siyo asali nzima.

Asanteni unaweza kuwasiliana nami kwa elimi zaidi. +255622 642620 au +255784 642620.

Pia unawaza kusoma Makala zangu nyingine za ufugaji nyuki hapahapa jamiiforums kama zifuatazo;

1.Utegaji nyuki waingie katika mizinga
2.Uvunaji wa Sumu ya Nyuki
3.Fahamu mbinu za kugawa makundi ya nyuki kwenye mizinga mpya

View attachment 1954344

View attachment 1954345
 
Kwanini huwa Wana pika(kuchemsha) Asali ?, na utaijuaje kama asali imepikwa. Shukrani Kwa ilimu mkuu
Nakujibu kwa niaba na kwa uzoefu sio kitaalamu.

Ninavyojua njia hii ya kupika asali huwa ni njia rahisi sana ya kukamua asali na pia huwa wanaweka maji ili iwe nyingi.
Vilevile walikuwa wanaipika hawakujua kuwa asali ikipikwa inapoteza ubora wake wao daima walijali utamu t.

Ni njia ya muda kidogo ambayo hata sisi tumeitumia kipindi cha nyuma kwani asali ikipikwa huyeyuka haraka sana yaani ndani ya dk15 umeiyeyusha asali nyingi sana.

Zamani ukitaka asali mbichi tulikuwa tunakamua kwa mkono ama kuiweka juani inakuwa inatiririka kidogo kidogo
zoezi hili lilikuwa likichukuwa muda sana hata wiki nzima na zaidi kama asali ni nyingi.

kwa sasa kuna machine za kukamua asali mkuu dk0 kazi imeisha. Ahsante
 
Back
Top Bottom