Fred Katulanda
JF-Expert Member
- Apr 1, 2011
- 380
- 550
Kumekuwa na maswali mengi kutoka kwa watumiaji asali ambao wengi wamekua wakiuliza kutaka kujua kama asali iliyoganda ni nzuri au imechakachuliwa. Wengine wamekua wakiamini asali iliyoganda imechanganywa na sukari guru.
Lakini hata baadhibya wafugaji na wauza asali pia wamekua wakiogopa kuiuza asali iliyoganda kwa Imani wateja wataikataa hivyo baadhi yao kujikuta wakipata hasara na wengine kuianikanjuani saa chache mteja anapokuja kuiona.
Kupitia Makala haya fupi Leo nakuja na sababu za asali kuganda, na kukufafanulia nini hasa husababisha Asali igande kitalaamu.
Sasa, ili uelewe vyema sababu ni lazima utambue kuwa nyuki anapoitengeneza asali dani yake huwa kuna sukari ambayo huipata kutokana na malighafi anazotumia kutengenezea asali hiyo.
Kitalaamu nyuki hutengeneza asali kwa kuchukua Pollen (Chavua) na Nectar (Mbochi), kutoka katika chanzo mbalimbali cha mimea. (Nectar ni majimani yenye utamu ya maua na Pollen ni unga wa maua).
Sasa malighafi hizi mbili hutengenezwa Kitalaamu na nyuki kwa pamoja na kuchanganywa (kusindikwa) na kuwa asali ambao kiasili huwa ni chakula cha ziada ambacho nyuki wao hukiandaa ili kukitumia kwa chakuka wakati ambao mvua zimekatika na mimea haitoi maua tena.
Kwa kawaida mchakato mzima wa nyuki unapokamilika na kuifanya asali kuiva ndani yake huwa na mchanganyiki wa sukari kuu za aina mbili ambazo ni;
(a). Fructose
(b). Glucose
Sasa wakati nyuki wakitembea na kuchukua Pollen ya maua kwa ajili a kutengenezea asali na wakapata Pollen nyingi ya maua yenye sukari nyingi aina ya Fructose zaidi ya Glucose basi asali hii haitokuwa na tabia ya kuganda.
Lakini ilitokea nyuki akachukua Pollen yenye kiasi kingi cha Glucose kuliko fructose basi asali itakayozalishwa na nyuki wa aina hii mara nyingi huwa na tabia kuganda.
Kwa maekezo yangu hayo, kuganda kwa asali siyo Jambo baya sababu inatokana na aina ya sukari iliyopatikana kwenye malighafi zake.
Jambo lingine muhimu ni kuwa; asali hiyo ikiganda hutengeneza chengachenga nyingi ziitwazo Crystallize. Asali hii kidogo husumbua watumiaji hivyo ukitakankuitumia ni lazima uiweke kwenye jua au majibya Moto ndiyo iyeyuke Kwa ajili ya kuitumia lakini siyo mbaya.
Zingatio: Asali ikiganda iangalie umepanda yote ndaniya chombo, lakini kama imeganda nusu tu, ndani chini na juu inaonekana haijaganda basi hiyo inauwezekano kuwa imechanganywa na kitu na siyo asali nzima.
Asanteni unaweza kuwasiliana nami kwa elimi zaidi. +255622 642620 au +255784 642620.
Pia unawaza kusoma Makala zangu nyingine za ufugaji nyuki hapahapa jamiiforums kama zifuatazo;
1.Utegaji nyuki waingie katika mizinga
2.Uvunaji wa Sumu ya Nyuki
3.Fahamu mbinu za kugawa makundi ya nyuki kwenye mizinga mpya