Salamu kwenu wakuu, jana kwenye matembezi tembezi yangu hapa jijini arusha mida ya jioni mimi na ndungu yangu mmoja tulipita maeneo ya (eneo siwezi kulitaja ili kulinda biashara ya watu) tulikutana na mjasiliamali mmoja ana miaka kama 22-26 kwa kumuangalia. Pasi na shaka tukaona bora tukaribie eneo ilo. Eneo lenyewe lipo karibia na barabara (pembeni ya barabara upande wa kushoto) eneo analouzia popcorn kuna mashine ya popcorn na benchi la kukaa. Nikiwa nimekaa kwenye benchi nakula popcorn zangu nikaanza kumuuliza maswali madogo madogo tu.
Sw 1. Upo smart, una degree nn kaka?
Jb. (Akacheka) ninayo nimesoma accounting
Sw 2. Mbona umeacha uhasibu?
Jb. Sijaacha ila niliona ajira saivi ni ngumu bora nikiwa natafuta niendelee kujihusisha kwenye biashara ndogo ndogo
sw 3. Hahaa ok, mbona popcorn?, si ungefanya biashara nyingine labda kuuza mashati
jb. (Akacheka)mwaka jana nilivyo maliza chuo nilikua na kama 340000 cash mm nae nilikuta na muuza popcorn nikaipenda hii biashara
sw 4. Aise sasa biashara ulianzaje mkuu?
Jb. Nilipata hii mashine used kwa 270000 ilo benchi nilichukua nyumbani na ela iliyo baki nikanunua vifungashio, mahindi na mahitaji mengine. Siku ya kwanza niliuza popcorn za sukari mifuko 7 na za chumvi 12
MIMI: na saivi biashara inaendaje mzee bb?
jb. Yani hapa kwa siku naweza kuuza popcorn za chumvi mifuko 45 na sukari 20 minmum, maxmum popcorn za chumvi kama 55-60 na sukari 30-40
NOTE:
Popcorn za sukari mfuko mmoja 1000 na popcorn za chumvi 500
ukichukua minmum yake ya 45 X 500=22500 X 30= 675000,, 20 X 1000= 20000 X 30 =600000
TOTAL:1275000
(tuliongea mengi lakini ya muhimu ni hayo hata na ivyo popcorn zangu zilikua zimeisha)