Fahamu kuhusu biashara ya kuuza chakula (Mgahawa)

Hii biz ipo hivi inataka commitment! uwepo mwenyewe ila ukiajili watu and ur not around my dear bora ukabet tu!
chakula kina hesabu kila kilo moja inatoa sahan kadhaa Sasa Kama unapika kilo zako u hv to make sure Imepatikana sahani zenye ratio na maandalizi yako! Kama unaajiri mtu Bora usifunge tuuu!

Hatukuvunji moyo me am in that biznes ktk cafe pia nasuply yaan no easy way u hv to be there!

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Naunga mkono hojA
 

Ila kumbuka tungekua wote wezi mbingu ingekua tupu mkuu ila amini hvyo hvyo mkuu uwachunge wafanyakazi wako uone kama watakaa, mwizi anajulikana kama huwezi kuwagundua mimi nawagundua na niko maakini kupita maelezo na sijawahi danganyika namshukuru Mungu kwa hilo. Halafu hapa tunaongelea fremu moja huwezi linganisha na CCTV camera cjui huko mbali.
 

Ni bora yeye awepo Mimi nisiwepo kuliko Mimi niwepo yeye asiwepo coz ana ujuzi na hyo biashara
 

Hapo ndo umeongea khs graph bt swala la wizi kama wanavyosema wengine weka kando, nashukuru ntamuelimisha khs hilo la graph
 

Haimaanishi sitapatembelea kabisa ntakua naenda weekend tena jumamosi tu inatosha kbs comments nyingine atapokea yeye
 
Sijaelewa, huyo dada ndie atakua anafata vitu sokoni, anapika na kuhudumia akiwa peke yake au una wafanyakazi wengine ila yeye unamfanya kama msimamizi wako?
 
Pia,umejiandaaje kuhusu viporo vinavyobaki?Hakuna mteja anayependa kupata supu ya jana,maandazi,chapati au chakula cha jana ingawa ni hasara;lazima uwalishe wateja wako vitu fresh ili waendelee kukuunga mkono.

Hapo ndo unipe mawazo
 

Sasa asiejua hesabu la sahani ni nani? A very light point. Usijali sivunjiki moyo kirahisi mpaka sasa sijaona point ya kunivunja moyo.
 
Aisee, biashara nzuri ukiifanya mwenyewe ujionee changamoto zake na namna ya kuzitatua, kwa ninavyoona umejipanga kurudi jioni na kukusanya mapato huku ukiwapangia cha kufanya jiandae kupoteza hiyo milioni yako.

Nakupa mfano miaka mi 4 iliyopita nilifanya hiki unachokifanya tena kwa ukubwa haswa nikitafuta wamama wapishi wazuri (akiwemo shangazi yangu), nikafungua cafeteria chuo kimoja kipo hapo mbezi jogoo, nilitengeneza mfumo mzuri wa uendeshaji huku nikiwuweka shangazi yangu kama manager, mimi mara moja moja mwisho wa wiki ndio ninaenda, kukagua na kuchukua mapato kutenga budget ya wiki i ayofuatia n.k

Walichonifanya baada ya kuona kuwa ninakuj kuchukua hela tuu na kuwapangia cha kufanya wakataka nyongeza ya mshahara, nikawapa. Hawakuridhika nilikuwa nimepanga wafanyakazi kila mtu kitengo chake kuna mtu wa kuosha vyombo, wa juice, chips, chai na vitafunwa na wa bites, kila mmoja kwa kitengo chake wakaanza kunipiga taratibu mfano mtu wa bites (karanga, ubuyu n.k)anatengeneza wa kwake anauza ukiisha ndio anauza vyangu.

Mapato yakaanza kuporomoka, nikachukua likizo, na kwenda kusimamia mwenyewe waliacha kazi watatu wenyewe na wengine nilifukuza taratibu akiwemo shangazi yangu ambaye nilimtimua mpaka leo hatuongei.

Kuwa makini, usije ukawa umempa mtu mtaji afanye yake.
 
Kasema huyo dada anajua yeye atamsimamia swali atamsimamiaje na yeye yuko kazini? mama ntilie tena mpya raha uwepo mwenyewe au da rebecca unaonaje?mimi naona kodi ya miezi 3 ikiisha wanafunga biashara hawa.

Mie naona angeomba likizo isiyo na malipo kazini,kisha ufungue biashara yake yeye na huyo dada,biashara ya mama tilie ni nzuri sana ila ukikosea mwanzo wateja hawaji ng'oo lol, akianza vizuri mwanzo basi tayari
 
Ntamwachia ntapitia hesabu coz mda mwingi ntakua kibaruani
Jaribu kuchukua ata likizo ya mwezi mmoja ndo uanze biashara ukiwepo ili kuhakikisha kila utakachomwelekeza ata kifanyia kazi kwa mfano usafi ,chakula kizuri kiwe full package,namna ya kuhudumia wateja,muda wa kufungua n.k
Usipende kuwaamini sana watu kwenye kuanzisha kitu kwa pesa yako ukiamini atasimamia vizuri kumbuka malengo yatatofautiana utaishia kupoteza pesa na mtu hawezi kujitoa kama utakavyofanya wewe mwenye pesa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…