Fahamu kuhusu biashara ya kuuza chakula (Mgahawa)



Una jicho kama langu..!andika tu unaoba huyu hana commitment kbs
 
Kwahiyo wewe ni mwanamke usiyejua kufanya lolote jikoni zaidi ya kuchemsha chai na maji ya kuoga ama? Hujaolewa bado?
 
so ww huwez kushika usukani kbs umeamua kumuamini zaidi huyo
Huyu mshamba wa biashara, na hii business yenyewe kaamua kuianzisha kwa mhemko tu ila hana passion nayo thats why anategemea mwenzake amenyeke kumuendeshea biashara kwa faida kwa vile ni mtu experienced, anamuamini ama rafiki yake sana sijui blah blah. Hakunaga mtu anafanyaga biashara ya mtu baki kwa moyo, hata huko kazini watu wanapoenda kuna muda wanaspend kuchat na kupiga story bila kujali kwamba wanalipwa mshahara, badala ya kufanya kazi kwa bidii ili wamchangie CEO aongeze nyumba na magari zaidi hapa mjini!

Biashara ina stage 4 (introduction,growth,maturity na decline stage). Inatakiwa kusimamiwa kwa uchungu mpaka pale itakapofikia maturity stage. Kuanzia hapo una struggle kuhakikisha unafanya maboresho kila uchao ili graph isiporomoke kwenda decline, ukiskia matajiri hawalali vizuri hiko ndio kinawatesaga sana.

Sasa huyu mwenzetu yeye biashara hana uzoefu nayo ila ni mjuaji. Cha kufanya mwacheni hio 1m ikiteketea bila maelezo ya kueleweka atatia akili vizuri na huo ushoga wao ndipo utakapokufa.
 


😂😂😂Umeongea kwa machungu sana. Kifupi umewakilisha mawazo yangu. Tufanye mengine
 
Haimaanishi sitapatembelea kabisa ntakua naenda weekend tena jumamosi tu inatosha kbs comments nyingine atapokea yeye
Hu hu hu hu hu biashara ya usimamizi wa simu. Basi kuwa mfanyakazi wa sehemu km hii raha sana, hata ukiniambia utanilipa elfu 10 kwa mwezi.
 
Achana na maturity huko mbali, kwenye introduction penyewe ndio panapoamua uelekeo wa biashara. Ndio maana unaona kuna biashara zinakufa zikiwa na miezi michache tu. Sasa huyu introduction hataki kupasimamia maturity huko atafika.
 
Achana na maturity huko mbali, kwenye introduction penyewe ndio panapoamua uelekeo wa biashara.
Ndio maana unaona kuna biashara zinakufa zikiwa na miezi michache tu.
Sasa huyu introduction hataki kupasimamia, maturity huko atafika
Ndio maana nikasema ni katika hatua ambazo inabidi mtu akaze sana. Yani introduction, growth hadi kufikia maturity. Akichemka hapo tu hio biashara haita survive!
 
Baada ya miez sita yaani mwezi wa nane tutarudi hapa kupata mrejesho. Ila kwa uzoefu wangu hauwezi panda farasi wawil kwa wakati mmoja i.e hauwez kuajiriwa na kujiajiri na ukafanikiwa kote. Utatakiwa utoroke kazin uende kwenye ofisi yako kitu ambacho mwajiri hata kubali unaweza poteza huku. Na ukishindwa kutoroka basi jua kwenye biashara yako kutakuwa na uhuru wa manyani.

Kitu kingine ni kamba sio kila biashara inayofungwa au kufilisika basi wafanyakazi au mfanyakazi wako amekuibia. Mara nyingi wafanyakazi waaminifu huwa wanaingiza hasara kwa kutojua thaman halisi ya biashara kwa maana mtaji,faida na nini watumie na nn wasitumie. Kwa mfano mfanyakazi wako anaweza laza mauzo ya sh. 200,000/ kwa siku akaona ni hela nyingi sana nae anaamua kujiponheza kwa kazi nzuri atajiwekea bando la elfu tano kwenye smu, atanunua na kiatu cha 15,000/ akiamini anajipongeza lakin kumbe katika hayo mauzo ya laki mbili faida ni 30,000/ tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahah hii tabia ya Kanji kabisa. Anatengeneza urafiki wa siri na kila mmoja wenu ili kuwa spy. Kila mmoja atajikuta anamsnitch mwenzie hivyo mtaishia kuwa mnachukiana tu. Hamuwezi kushirikiana kumfilisi!
 
Mshua umetoa wazo la akili sana.
 
Bei cheap inategemea na eneo! Kama unauza kinondoni huwezi uza sahani ya wali 1,500/= mzee baba. Dar chakula watu wanauziana mpaka sh.10000 kwa sahani. The least niliowahi kuona ni 3,500 kwa maeneo ya mijini.
 
Mim simkatishi mtu tamaa ila hii biashara ni biashara ngumu sana, Utaianza vizuri haipiti miezi 6 ushaumia, labla usiwe na biashara moja, usiitengemee kama ndiyo biashara kuu inayo kuingizia hela
Sio hii tu, biashara yeyote usipokuwa strategic hutoboi!
 
Habari zenu wandugu,

Samahani, leo nimeamua kuja kwenu baada ya muda mrefu kufanya mpango wa kuanzisha biashara. Hivi karibuni nimefanikiwa kupata mtaji kiasi cha sh milioni tano (5,000,000) za Kitanzania. Hamu yangu kubwa ni kumiliki mgahawa.
Maeneo niliyopo ni Dar es Salaam.

Kabla sijaanza hii biashara ningependa kujua machache kutoka kwa wazoefu wa hii biashara.

Kati ya mambo ambayo ningependa kuyajua ni:

1. Je, kwa mtaji huo nitaweza kuendesha biashara hiyo na kupata faida?

2. Ni changamoto zipi nitakutana nazo pindi tu nitakapoanza hii biashara.

3. Ni vitu gani vya kuzingatia wakati wa kuendesha hii biashara.

4. Ni maeneo gani kwa mtaji huu yatafaa kuendeshea hii biashara nikapata faida ya kuridhisha.

Ahsanteni sana
 
 
Tatizo sio mtaji kuwa wa kutosha au kutotosha.

Kitu muhimu ni taarifa muhimu/sahihi kwa unachotaka kukifanya, na taarifa utazipata kwa kuzifanyia utafiti wa hicho unachotaka kufanya.

Nakushauri

1) Jua aina ya biashara unayotaka kufanya na kwa ubora gani,
2) Jua walengwa wako kina nani,
Na wanapatikana maeneo gani, na hapa ndio utajua ukafungue wapi biashara yako.
3) wafuate walengwa wako japo kwa uchache ujue wanahitaji nini
4) Pita kwenye biashara za wengine jua wanafanyaje
5) Pitia social media za biashara za wenzio pitia comments itakusaidia kujua pia nini kinalalamikiwa au kusifiwa nawe ukavifanyie kazi katika maandalizi yako ya kwanza hiyo biashara.
Nakutakia heri.
 
Ahsante sana
 
Tafuta location ambayo utaweza kuuza chakula kwa bei ya juu mfano wali nyama kuanzia 3000/=

Chini ya hapo usifanye biashara hii kabisa.
 
Mtaji unatosha kabisa, issue hapo location.

Kama utapata sehemu nzuri ambayo chakula unaweza kuuza Tsh 2000, ongeza na vinywaji baridi, pia weka na kijana wa chips maana wadada wengi ndo chakula chao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…