Habari zenu wandugu.
Samahani, leo nimeamua kuja kwenu baada ya muda mrefu kufanya mpango wa kuanzisha biashara.
Hivi karibuni nimefanikiwa kupata mtaji kiasi cha sh milioni tano (5,000,000) za kitanzania.
Hamu yangu kubwa ni kumiliki mgahawa.
Maeneo niliyopo ni dar es salaam.
Kabla sijaanza hii biashara ningependa kujua machache kutoka kwa wazoefu wa hii biashara.
Kati ya mambo ambayo ningependa kuyajua ni
1. Je, kwa mtaji huo nitaweza kuendesha biashara hiyo na kupata faida?
Jibu ni ndio kwa mtaji wa milioni tano unaweza kuendesha biashara na kupata faida
2. Ni changamoto zipi nitakutana nazo pindi tu nitakapoanza hii biashara.
Kwanza uwe tayari ku run biashara yako kwa siku kadhaa bila ya wateja, pili kama huna certificate ya FDA tegemea kusumbuliwa sana, tatu tegemea kukosa hiki na kile wakati wa kuanza (hii unaweza kununua vifaa kidogo kidogo kadri muda unavyoenda), tegemea malalamiko kwa hao wateja wachache watakao tumia huduma.
3. Ni vitu gani vya kuzingatia wakati wa kuendesha hii biashara.
Zingatia, sana sana usafi, usafi wamazingira na watoa huduma hii ni muhimu sana, huwezi kuendesha biashara ya mgahawa bila ya kuwa na mpishi ambae ni muelewa na ako na uzoefu wa kutosha, tatizo watu wa aina hio wengi tayari wana ajira zao kwa hio ni kitu cha kumtoa sehemu alipo na kumleta kwako itakugharimu kidogo, tahadhari hapa usichukue wapishi wa vichochoroni ama wale wanaopika pilau kwenye sherehe mitaani itakugharimu sana biashara nzuri kwa chakula ni ile inayo range kati na kati
4. Ni maeneo gani kwa mtaji huu yatafaa kuendeshea hii biashara nikapata faida ya kuridhisha.
Popote pale unaweza kuanzisha biashara ya mgahawa na ikaenda vizuri kutegemea na kundi gani unalilenga. Maeneo yenye movement kubwa ya watu kama mbangala, tandika, temeke mwisho na mengine kama hayo unaweza kuanzisha hio kitu. Zingatio, jikurupushe sokoni, feri na maeneo ya minada kwa kupata vitu bei nafuu alfajiri mapema
Ahsanteni sana