Fahamu kuhusu biashara ya kuuza chakula (Mgahawa)

Fahamu kuhusu biashara ya kuuza chakula (Mgahawa)

dada mimi nimekulia kwenye biashara.. wazazi wangu hawajawai kuajiriwa wote. na hata nilipo nafanya biashara ndogo ndogo nyingi sana...
nina dry cleaner zaidi ya 5, nina tshirt workshop, photo studio, uber tax, na vingine.. najua changamoto nyingi sana

mimi sio mwanasiasa.. nakueleza nayoyaona na kuyaona...

biashara nafanya na wafanyakazi.. ila nawasimamia kwa technology... hata hao kina mengi wameweka mabosi wahindi vichwa.. na pia wanawasimamia kwa technology..

haya mambo ya kusaini kwa vidole, cctv, kpi, etc etc. ni usimamizi wa kisasa

Narudia tena hakuna mtu duniani anaependa kumtafutia mwenzake hela.. huku hata yeye ana shida ya hela...

what you think, what we print (@tshirt_garage_mabibo_hostel) • Instagram photos and videos
Aiseee niliwahi print t-shirt kwako.

Mkuu hiyo mashine ya kuprint inauzwaje?

I'm the girl from nowhere, he one no one will miss. That's why they choose me.[emoji97]
 
Kufeli kupo iwapo ataondoka
Kwa iyo unaamini bila yeye hauwezi fika popote?

Watu wengi humu wamekupa ushauri mzuri sana na wengi wanaonekana wanaongea kupitia experience.

Wengi hatujui MTU unaeenda kumuachia biashara yako anauzoefu gani wa kuendesha hiyo biashara.

Kujua kupika au kuwa mpishi mzuri na kuendesha biashara ya mgahawa ni vitu viwili tofauti.

Kwa biashara ya chakula hiyo formula unayotaka kutumia inafanya kazi ukiwa mzoefu wa iyo biashara lakini kama ni mgeni kuna mianya mingi sana ya pesa kupotea.

Trust but verify.
 
Itakushinda kama utaanza hiv dada angu,nikwambie ukwel tuu.

Sabab management ndo kila kitu,huyo msichana si maono yake hyo biashara so yeye anafanya tuu alipwe..wew ndie mwenye maono kwamba unataka chakula kiwe hiv,quality i mean..usaf,hospitality,uwepo uvumiliv,acountability etc .so huyo dada hatoweza.

Atauza wik 1 ataona hamna wateja atavunjika moyo ataanza lipua kaz na ndo mwanzo wa kuharibika, sababu trend ya biashara yoyote enewea, graph huanza kidogo then hushuka kwa kas ya ajab, badaee ndo huanza kupanda,je huyo unaemwachia ataweza haya yote.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu Napoleone umeonge points za maana sana
 
Mammbo ya kuzingatia unapoanzisha biashara ya chakula:-

1. Usafi wa watu/mtu na mahala pa kufanyia kazi (hili ni muhimu mnooo)
2. Kujua bei za bidhaa, kujihimu kudamka sokoni (masoko makuu) Nazi ya kawaida unaweza kuinunua kwa shilingi 1,500 mda wa kawaida, lakini ukidamka sokoni unaipata kwa mia saba ama elfu moja.
3. Kujua aina ya wateja waliokuzunguka na wanataka nini. Huwezi kupiga mchele kwenye eneo la wasukuma wengi.
4. Kujali maslahi ya wafanyakazi wako na kuwa na ukaribu nao
5. Kuwa na tabia ya kudamkia Feri siku za weekend, kusanya stock ya wiki nzima badala ya kununua rejareja (feri utajifunza meng)
6. Ubunifu na ucheshi kwa wateja
Mkuu kwani Ngosha hawalagi ubeche?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ntamwachia ntapitia hesabu coz mda mwingi ntakua kibaruani
Nashauri itakuwa vzur uptie faida ya sku yaani baada ya yeye kuuza na kununua tena bidhaa ulizoaanza nazo kipi kinasalia? yaan mkabidhi / wakabithi wakulipe kias kadhaa kwa sku, ambacho kitalipa tena kodi na gharama nyingne na faida ya uwekezaji wako kila la kheri.
 
Cataliyya omba ruhusa ya wiki moja kibaruani kwako usimamie kwanza
Ni kweli itazame biashara mwanzoni (mwanzo mgumu) mzunguko halisi, pia baada ya muda flani kuona unachopata ni stahiki? pia inatakiwa uridhie tu kiwe wastani sio kila sku faida itakuwa hyo hyo
 
Mpendwa,

Mengi yamenenwa na wadau, nawapa big up wadau.

Jambo muhimu ni kwamba hilo wazo ni nzuri tena sana, kwasababu kubwa 2

Moja - biashara ha chakula haina hasara kwasababu watu lazima wale. Lkn pia hali ya maisha asilimia kubwa ya watu wamepunguza bajeti zao sasa hivyo badala ya kula mahoteli makubwa ama manyama choma, mamantilke wamepata wateja sana.

Mbili, kudhubutu. Hakuna atakae fanikiwa bila kudhubutu na kuanguka ndio mwanzo wa kufanikiwa. Wanasema hjashindwa hujafanikiwa.

Kwa msaada zaidi, sio kwako tu bali wadau wengine patahuduma zetu ambazo ziifanikisha zaidi ndoto zako

HUENDA WAHITAJI:

* Kusajili kampuni
* Annual Retur - Brela
* Hesabu za Kodi, Hesabu za Kampuni,
* Kuandaa Memorandum....
* Kuandika Business Plan, Business Profile,
* Kuandaa Tender documents, CRB
* Kutengeneza LOGO, Business Cards, Brochures, Banners
* Printing - All types of Books
* Digital Printing: T-SHIRTS, CAPS, BAGS, PLATES, CUPS, etc.

TUPIGIE/ MESEJI - 0684 205039: WATSUP TU 0652 411402
BEI ZETU HAZINA USHINDANI, MIKOANI PIA TUNAHUDUMIA

Ushauri ni bure


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee, biashara nzuri ukiifanya mwenyewe ujionee changamoto zake na namna ya kuzitatua, kwa ninavyoona umejipanga kurudi jioni na kukusanya mapato huku ukiwapangia cha kufanya jiandae kupoteza hiyo milioni yako

Nakupa mfano miaka mi 4 iliyopita nilifanya hiki unachokifanya tena kwa ukubwa haswa nikitafuta wamama wapishi wazuri (akiwemo shangazi yangu), nikafungua cafeteria chuo kimoja kipo hapo mbezi jogoo, nilitengeneza mfumo mzuri wa uendeshaji huku nikiwuweka shangazi yangu kama manager, mimi mara moja moja mwisho wa wiki ndio ninaenda, kukagua na kuchukua mapato kutenga budget ya wiki i ayofuatia n.k

Walichonifanya baada ya kuona kuwa ninakuj kuchukua hela tuu na kuwapangia cha kufanya wakataka nyongeza ya mshahara, nikawapa, hawakuridhika nilikuwa nimepanga wafanyakazi kila mtu kitengo chake kuna mtu wa kuosha vyombo, wa juice, chips, chai na vitafunwa na wa bites, kila mmoja kwa kitengo chake wakaanza kunipiga taratibu mfano mtu wa bites (karanga, ubuyu n.k)anatengeneza wa kwake anauza ukiisha ndio anauza vyangu,

Mapato yakaanza kuporomoka, nikachukua likizo, na kwenda kusimamia mwenyewe waliacha kazi watatu wenyewe na wengine nilifukuza taratibu akiwemo shangazi yangu ambaye nilimtimua mpaka leo hatuongei

Kuwa makini, usije ukawa umempa mtu mtaji afanye yake

Hukupata watu sahihi na hukuwasoma kwanza utendaji wao wa kazi ulikurupuka ilibidi uwasome kwanza, yeye kua shangazi yako haimaanishi sio mwizi ilibidi umsome kwanza
Hongera kama inaendelea vizuri
 
Aisee, biashara nzuri ukiifanya mwenyewe ujionee changamoto zake na namna ya kuzitatua, kwa ninavyoona umejipanga kurudi jioni na kukusanya mapato huku ukiwapangia cha kufanya jiandae kupoteza hiyo milioni yako

Nakupa mfano miaka mi 4 iliyopita nilifanya hiki unachokifanya tena kwa ukubwa haswa nikitafuta wamama wapishi wazuri (akiwemo shangazi yangu), nikafungua cafeteria chuo kimoja kipo hapo mbezi jogoo, nilitengeneza mfumo mzuri wa uendeshaji huku nikiwuweka shangazi yangu kama manager, mimi mara moja moja mwisho wa wiki ndio ninaenda, kukagua na kuchukua mapato kutenga budget ya wiki i ayofuatia n.k

Walichonifanya baada ya kuona kuwa ninakuj kuchukua hela tuu na kuwapangia cha kufanya wakataka nyongeza ya mshahara, nikawapa...hawakuridhika nilikuwa nimepanga wafanyakazi kila mtu kitengo chake kuna mtu wa kuosha vyombo, wa juice, chips, chai na vitafunwa na wa bites, kila mmoja kwa kitengo chake wakaanza kunipiga taratibu mfano mtu wa bites (karanga, ubuyu n.k)anatengeneza wa kwake anauza ukiisha ndio anauza vyangu,

Mapato yakaanza kuporomoka, nikachukua likizo, na kwenda kusimamia mwenyewe waliacha kazi watatu wenyewe na wengine nilifukuza taratibu akiwemo shangazi yangu ambaye nilimtimua mpaka leo hatuongei

Kuwa makini, usije ukawa umempa mtu mtaji afanye yake

Hukupata watu sahihi na hukuwasoma kwanza utendaji wao wa kazi ulikurupuka ilibidi uwasome kwanza, yeye kua shangazi yako haimaanishi sio mwizi ilibidi umsome kwanza.

Hongera kama inaendelea vizuri.
 
Wabongo tuna upuuzi wa kujifanya mabosi kipindi tunafungua biashara. Kama wafungua biashara, kaa mwenyew maana jua kuwa hapo umewekeza hela na co mawe. Kama una kibarua kwakweli tulia kwanza, ila kama waipenda hyo biashara, anza kwa kukaa wew mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaribu kuchukua ata likizo ya mwezi mmoja ndo uanze biashara ukiwepo ili kuhakikisha kila utakachomwelekeza ata kifanyia kazi kwa mfano usafi,chakula kizuri kiwe full package, namna ya kuhudumia wateja, muda wa kufungua n.k

Usipende kuwaamini sana watu kwenye kuanzisha kitu kwa pesa yako ukiamini atasimamia vizuri kumbuka malengo yatatofautiana utaishia kupoteza pesa na mtu hawezi kujitoa kama utakavyofanya wewe mwenye pesa.

Sawa ntazingatia kama ntakachomwambia atakifuata.
 
Back
Top Bottom