Fahamu kuhusu Bunge Maalum la Katiba

Fahamu kuhusu Bunge Maalum la Katiba

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Ndugu zangu watanzania, baadhi yetu hawana uelewa wa kutosha wa Bunge Maalum la Katiba litakalojadili na kupitisha Rasimu ya pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nikiwa kama mtanzania, msomi wa sheria, nimeona ni bora kudokeza kwa ufupi kuhusu Bunge hili Maalum la Katiba (Constituent Assembly). Nitakuwa, nikisaidiana na mtanzania yeyote mwenye uelewa na jambo hili, ninajibu maswali yatakayojitokeza.

Nafanya hivi nikiamini kuwa ni wakati muafaka kusambaza uelewa juu ya jambo hili kwakuwa nchi yetu inakaribia hatua hiyo muhimu ya kuwa na Bunge Maalum la Katinba katika kuelekea kupata Katiba mpya ya nchi yetu. Napendelea kuleta hoja zangu katika mtindo wa maswali na majibu.

1. Sheria gani inalisimamia Bunge Maalum la Katiba?

Ni Sheria ya Mapitio ya Katiba (Sheria Nambari 8) ya mwaka 2011 ikisomwa pamoja na Marekebisho yake yaliyofanywa kupitia Sheria Nambari 2 ya mwaka 2012.

2. Akina nani watakuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba?

Kulingana na kifungu cha 22 kifungu kidogo cha (1) aya (a), (b) na (c) cha Sheria Nambari 8 ya 2011, Wajumbe wa Bunge la Katiba watakuwa: Kwanza, Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pili, Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.Tatu, wajumbe 166 watakaopatikana kutoka katika Taasisi zisizo za kiserikali, Jumuiya za kidini, vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa, Taasisi za elimu ya juu, shirikisho la wafanyakazi,shirikisho la wakulima,shirikisho la wafugaji, shirikisho la watu wenye mahitaji maalum, na kikundi chochote cha wananchi kinachojulikana kwa jina lolote ambacho kina malengo yanayofanana.

3. Nani anateua/atateua Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba?

Jibu lipo chini ya kifungu cha 22 kifungu kidogo cha (3) cha Sheria Nambari 8. Ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais atachapisha majina ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba katika Gazeti la Serikali. Hatahivyo, uteuzi husika, ifahamike mapema na kwa umakini hapa, utawahusu wajumbe 166 tu ambao si Wabunge wala Wawakilishi. Hii ni kwakuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wataingia Bunge Maalum la Katiba kama walivyo.

4. Bunge Maalum la Katiba litaoongozwa na Nani?

Bunge Maalum la Katiba litaoongozwa na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ambao watachaguliwa kutoka Wajumbe wa Bunge hilo na Wajumbe wenyewe kwa kura za siri. Kama Mwenyekiti atatokea upande mmoja wa Muungano,Makamu wake atatokea upande wa pili. Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, kabla ya kushika ofisi zao, watakula kiapo kitakachoongozwa na Katibu wa Bunge hilo. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 23 cha Sheria Nambari 8 tajwa hapo juu.

Pia, Bunge Maalum la Katiba litakuwa na Katibu na Katibu Msaidizi. Hawa watakuwa ni Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa sasa pamoja na Katibu wa Baraza la Wawakilishi wa sasa. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 24 cha Sheria tajwa hapo juu.Lakini, kama Mwenyekiti anatokea upande mmoja wa Muungano, Katibu atakuwa ni kutoka upande mwingine. Mfano, Mwenyekiti akitoka Zanzibar, Katibu atakuwa ni Katibu wa sasa wa Bunge la Jamhuri. Katibu na Msaidizi wake wataapa mbele ya Rais kabla ya kuanza kazi zao. Hii pia inatamkwa na kifungu cha 24.

5. Mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba yatakuwa/ni yapi?

Mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba yanapatikana chini ya kifungu cha 25 cha Sheria Nambari 8 ya 2011. Yatakuwa ni kuunda Ibara za Katiba mpya, kuboresha na kuweka ibara-mvuko za Katiba Mpya kadiri Bunge husika litakavyoona inapasa. Haya yatazingatia Rasimu ya Katiba itakayowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba na Kupitishwa na Bunge hilo Maalum la Katiba.

Hapa, Bunge la Katiba litajadili, kurekebisha na kuboresha Rasimu ya Katiba na kuipitisha.

Tuanzie hapa kwa leo.....karibuni
 
ibara-mvuko nini..?

naomba ufafanuzi kwenye uboreshaji wa hii rasimu utakavyofanywa na hawa wabunge

asante kwa ufafanuzi.
 
Mkuu Maganga Mkweli, Bunge Maalum la Katiba litakuwa na nguvu ya kurekebisha au kubadili Ibara zilizopo katika Rasimu itakayowasilishwa katika Bunge hilo. Ibara mvuko, ingawa si tafsiri rasmi, ni 'Transitional Provisions'
 
Last edited by a moderator:

Mkuu umesema bunge maalumu linaweza kurekebisha au kubadili ibara zilizopo je lina uwezo wa kubadili Rasmu nzima? au ni baadhi tu ya vifungu? na kama ni baadhi ni vifungu vipi hawaruhusiwi kuvigusa?
 
Rasimu nzima yaweza kubadilishwa kwa kuimarisha Ibara zilizopo.Lakini,kuna Ibara haitakuwa na mijadala mikubwa. Ibara zitakzovuta hisia tayari zimeshaanza kujitokeza.Ni kama ya Serikali tatu na Wabunge kutokuwa Mawaziri. Kimsingi,nguvu ya Bunge Maalum la Katiba ni kujadili na kupitisha Rasimu husika. Lakini,chochote chaweza kutokea
 
Mkuu Kama tume ya katiba ilivunjwa hii maana yake nini? kwamba hawa watu hawataingia kabisa kwenye bunge ka katiba? au pengine wataingia kwa nafasi atazoteua raisi? kama wataingia je wataingia kama wajumbe wa kawaida? au watakuwa na kazi maalumu? ikitokea hawajaingia hakuna athari yoyote?
 
1.Bunge la Katiba litaanza lini?
2.Bunge la Katiba litaisha lini?
3.Je Bunge la Katiba litakapokwisha Je bunge la JMT litarudi au linakufa hapo linapoanza bunge la Katiba?
4.Je Kama litakufa Bunge la JMT je litakapo isha bunge la Katiba hatutakua na bunge mpaka Uchaguzi mkuu 2015
 
Mkuu Adharusi, asante kwa maswali yako manne.Kwanza,kuhusu swali la kwanza na la pili, muda wa kuanza na kuisha kwa Bunge Maalum la Katiba utapangwa na Serikali mara baada ya kutangazwa kwa Wajumbe husika. Inakadiriwa kuwa litakuwa la muda kati ya siku 60-70. Inatarajiwa kuwa hadi kufika mwishoni mwa Februari,Bunge hilo laweza kuanza.

Pili, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litaendelea kuwepo ingawa Wabunge wote watakuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Hii ni kusema kuwa,Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado litakuwepo hadi 2015. Bunge Maalum litaishi kwa muda mfupi sana.

Nadhani nitakuwa nimejibu,kadiri ya uelewa na uwezo wangu, maswali yako ya tatu na nne. Asante Mkuu Adharusi
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kama tume ya katiba ilivunjwa hii maana yake nini? kwamba hawa watu hawataingia kabisa kwenye bunge ka katiba? au pengine wataingia kwa nafasi atazoteua raisi? kama wataingia je wataingia kama wajumbe wa kawaida? au watakuwa na kazi maalumu? ikitokea hawajaingia hakuna athari yoyote?
Mkuu Mkono Luzuba, Tume ya Jaji Warioba ilikoma pale ambapo Tume husika ilikabidhi Ripoti ya Tume kwa Rais wa Jamhuri na Rais wa Zanzibar ple Karimjee. Sheria inayosimamia Bunge Maalum haikatazi waliokuwa Wajumbe wa Tume kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Bunge la Katiba.

Hivyobasi, yeyote aweza kuteuliwa kama Mjumbe kulingana na Sheria. Ikitokea hivyo, Mteule au wateule wataingia kama Wajumbe wa kawaida. Kama hawataingia,hakuakuwa na athari yoyote kwakuwa Sheria husika inatoa taratibu zitakazofuatwa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Adharusi, asante kwa maswali yako manne.Kwanza,kuhusu swali la kwanza na la pili, muda wa kuanza na kuisha kwa Bunge Maalum la Katiba utapangwa na Serikali mara baada ya kutangazwa kwa Wajumbe husika. Inakadiriwa kuwa litakuwa la muda kati ya siku 60-70. Inatarajiwa kuwa hadi kufika mwishoni mwa Februari,Bunge hilo laweza kuanza.

Pili, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litaendelea kuwepo ingawa Wabunge wote watakuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Hii ni kusema kuwa,Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado litakuwepo hadi 2015. Bunge Maalum litaishi kwa muda mfupi sana.

Nadhani nitakuwa nimejibu,kadiri ya uelewa na uwezo wangu, maswali yako ya tatu na nne. Asante Mkuu Adharusi

PETRO E.Mselewa ahsante Mkuu!ila nina swali la Nyongeza
1.Tuliambiwa Katiba inapatikana 2014!Je itaanza kutmika Pale tu siku ambayo imekamilika na kuwa katiba,au mpaka 2015
2.Kama itaanza kutumika 2014(mwaka huu)Je vipi kuhusu uhalali wa wabunge JMT katika maisha ya kibunge,sababu katiba iliowaweka Madarakani imeondoshwa,na baadhi watakuwa hawana vigezo vya kuwa wabunge(rejea kipengere cha Elimu,kama kitabaki hivi hivi rasimu II)
3.Kama itaanza 2015,vp uchaguzi wa serikali za mitaa utatumia Katiba gani ya JMT au Tanganyika(tanzania bara),na ya Zanzibar(Tanzania visiwani)
 
Asante kwa ufafanuzi.
Kweli nasikitika hata nilivyokosa nafasi ya kuwawakilisha wakulima.
 
PETRO E.Mselewa ahsante Mkuu!ila nina swali la Nyongeza
1.Tuliambiwa Katiba inapatikana 2014!Je itaanza kutmika Pale tu siku ambayo imekamilika na kuwa katiba,au mpaka 2015
2.Kama itaanza kutumika 2014(mwaka huu)Je vipi kuhusu uhalali wa wabunge JMT katika maisha ya kibunge,sababu katiba iliowaweka Madarakani imeondoshwa,na baadhi watakuwa hawana vigezo vya kuwa wabunge(rejea kipengere cha Elimu,kama kitabaki hivi hivi rasimu II)
3.Kama itaanza 2015,vp uchaguzi wa serikali za mitaa utatumia Katiba gani ya JMT au Tanganyika(tanzania bara),na ya Zanzibar(Tanzania visiwani)
Mkuu Adharusi,nashukuru kwa maswali yako ya nyongeza. Baada ya Rasimu ya Katiba kupitishwa na Bunge Maalum la Katiba na hatimaye kukubaliwa kwenye Kura ya Maoni na kuwa Katiba mpya,kutapangwa tarehe maalum kwa ajili ya kuanza kutumika kwa Katiba husika. Haiwezi kupangwa tarehe ya kuweza kuleta mkanganyiko.Hatahivyo,kati ya Ibara zitakazokuwepo ni zile zitakazoruhusu kuendelea kuwepo,kwa muda maalum kwa Taasisi au Mamlaka yaliyokuwepo kabla ya Katiba mpya.

Hivyobasi,hakutakuwa a kitu chochote kitakachoathiriwa na Katiba mpya kwa namna unayoisema.
 
Ahsante
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu watanzania, baadhi yetu hawana uelewa wa kutosha wa Bunge Maalum la Katiba litakalojadili na kupitisha Rasimu ya pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nikiwa kama mtanzania, msomi wa sheria, nimeona ni bora kudokeza kwa ufupi kuhusu Bunge hili Maalum la Katiba (Constituent Assembly). Nitakuwa, nikisaidiana na mtanzania yeyote mwenye uelewa na jambo hili, ninajibu maswali yatakayojitokeza.

Nafanya hivi nikiamini kuwa ni wakati muafaka kusambaza uelewa juu ya jambo hili kwakuwa nchi yetu inakaribia hatua hiyo muhimu ya kuwa na Bunge Maalum la Katinba katika kuelekea kupata Katiba mpya ya nchi yetu. Napendelea kuleta hoja zangu katika mtindo wa maswali na majibu.

1. Sheria gani inalisimamia Bunge Maalum la Katiba?

Ni Sheria ya Mapitio ya Katiba (Sheria Nambari 8) ya mwaka 2011 ikisomwa pamoja na Marekebisho yake yaliyofanywa kupitia Sheria Nambari 2 ya mwaka 2012.

2. Akina nani watakuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba?

Kulingana na kifungu cha 22 kifungu kidogo cha (1) aya (a), (b) na (c) cha Sheria Nambari 8 ya 2011, Wajumbe wa Bunge la Katiba watakuwa: Kwanza, Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pili, Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.Tatu, wajumbe 166 watakaopatikana kutoka katika Taasisi zisizo za kiserikali, Jumuiya za kidini, vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa, Taasisi za elimu ya juu, shirikisho la wafanyakazi,shirikisho la wakulima,shirikisho la wafugaji, shirikisho la watu wenye mahitaji maalum, na kikundi chochote cha wananchi kinachojulikana kwa jina lolote ambacho kina malengo yanayofanana.

3. Nani anateua/atateua Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba?

Jibu lipo chini ya kifungu cha 22 kifungu kidogo cha (3) cha Sheria Nambari 8. Ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais atachapisha majina ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba katika Gazeti la Serikali. Hatahivyo, uteuzi husika, ifahamike mapema na kwa umakini hapa, utawahusu wajumbe 166 tu ambao si Wabunge wala Wawakilishi. Hii ni kwakuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wataingia Bunge Maalum la Katiba kama walivyo.

4. Bunge Maalum la Katiba litaoongozwa na Nani?

Bunge Maalum la Katiba litaoongozwa na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ambao watachaguliwa kutoka Wajumbe wa Bunge hilo na Wajumbe wenyewe kwa kura za siri. Kama Mwenyekiti atatokea upande mmoja wa Muungano,Makamu wake atatokea upande wa pili. Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, kabla ya kushika ofisi zao, watakula kiapo kitakachoongozwa na Katibu wa Bunge hilo. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 23 cha Sheria Nambari 8 tajwa hapo juu.

Pia, Bunge Maalum la Katiba litakuwa na Katibu na Katibu Msaidizi. Hawa watakuwa ni Katibu wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa sasa pamoja na Katibu wa Baraza la Wawakilishi wa sasa. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 24 cha Sheria tajwa hapo juu.Lakini, kama Mwenyekiti anatokea upande mmoja wa Muungano, Katibu atakuwa ni kutoka upande mwingine. Mfano, Mwenyekiti akitoka Zanzibar, Katibu atakuwa ni Katibu wa sasa wa Bunge la Jamhuri. Katibu na Msaidizi wake wataapa mbele ya Rais kabla ya kuanza kazi zao. Hii pia inatamkwa na kifungu cha 24.

5. Mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba yatakuwa/ni yapi?

Mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba yanapatikana chini ya kifungu cha 25 cha Sheria Nambari 8 ya 2011. Yatakuwa ni kuunda Ibara za Katiba mpya, kuboresha na kuweka ibara-mvuko za Katiba Mpya kadiri Bunge husika litakavyoona inapasa. Haya yatazingatia Rasimu ya Katiba itakayowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba na Kupitishwa na Bunge hilo Maalum la Katiba.

Hapa, Bunge la Katiba litajadili, kurekebisha na kuboresha Rasimu ya Katiba na kuipitisha.

Tuanzie hapa kwa leo.....karibuni

samahani
ktk kipengele kinachohusu wahusika wa bunge la katiba,je kwa wanafunzi wanaosoma nje ya Tanzania wananafasi ya kuwemo ktk bunge la katiba?
 
Mkuu engmtolera, katika aina za Wajumbe,sioni inayowashirikisha wanafunzi wa ndani wala wa nje ya nchi. Asante
 
Last edited by a moderator:
Mkuu engmtolera, katika aina za Wajumbe,sioni inayowashirikisha wanafunzi wa ndani wala wa nje ya nchi. Asante

kama ni hivyo mkuu Petro E.Mselewa naona kama kutakuwa na kasoro ktk hili,maana ktk vyuo vikuu mfano vya Tanzania tulitegemea tungepata wawakilishi ambao wangeweza kuwakilisha mawazo ya wanafunzi wa vyuo vikuu hadi shule za msingi,hii ingesaidia kupata maoni toka kwa vijana wasomi ambao ndio viongozi wa kesho.
maana naona wafanya kazi na mashirika ya dini wao wana wawakilishi wao
sijui wewe unalionaje hili ukiwa kama ni mtaalamu wa sheria
 
Back
Top Bottom