Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
NINI MAANA YA DHANA YA NDOA?
Kwa mujibu wa sheria ya Ndoa ya Tanzania, ikidhibitika kuwa mwanaume na mwanamke wameiishi pamoja kwa miaka miwli au zaidi, katika hadhi ya mume na mke, basi kutakuwepo na dhana ya ndoa.
Sheria hii, imedhamiria kukomesha kama si kupunguza ile tabia ya wanaume au wanawake wengi kukaa na kumtumia mwenzi wake kwa jinsi ya mume au mke na baadae kumtelekeza akiwa hana kitu chochote katika maisha yake.
Hata ivyo ili mtu aishawishi mahakama kuhusu dhana ya ndoa inabidi athibitishe vitu vifuatavyo:
1. Ziwe ni jinsia mbili tofauti yaani jinsia ya kiume na ya kike. Hii ni kufuatia msimamo wa Tanzania kutotambua ndoa za jinsia moja.
2. Wawe wameishi chini ya nyumba moja. Hapa, inahitaji kuthibitika kuwa watu hawa huwa wanaishi katika nyumba moja kama mke na mume. Hivyo kutembelewa na mpenzi wako kwa kipindi kifupi kama wikiendi na kukaa pamoja kisha kila mtu anarudi kwake haiwezi kutumika kuthibitisha dhana ya ndoa.
3. Wawe wameishi katika hadhi ya mume na mke. Hapa ni lazima pathibitike kuwa wawili hao wameishi katika hali ya kuwapa hadhi ya mke na mume, mfano kuzaa pamoja.
4. Wawe wameishi pamoja kuanzia miaka miwili au zaidi.
JE MTU ANAWEZAJE KUIBATILISHA NDOA YA NAMNA HII?
Ili kuibatilisha ndoa ya namna hii, mtu anatakiwa athibitishe kutokamilika kwa vigezo vilivyotajwa hapo juu. Mfano kama miaka walioshi ni chini ya miaka miwili.