Fahamu kuhusu El Nino na athari zake kwa Binadamu na Mazingira

Fahamu kuhusu El Nino na athari zake kwa Binadamu na Mazingira

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
El Nino ni mfumo wa Hali ya Hewa unaosababishwa ongezeko kubwa la Joto la Bahari katika eneo la kati la Kitropiki kwenye Bahari ya Pasifiki. Hali hii huambatana na Vipindi vya Mvua kubwa vinavyoweza kusababisha mafuriko.

El Niño inaweza kusababisha mabadiliko ya Hali Mbaya ya Hewa, ikiwemo Ukame, Mafuriko, Vimbunga, na Vipindi visivyotabirika vya Joto ambavyo vyote ni Hatari kwa Afya ya Binadamu

Kwa mujibu tafiti mbalimbali za Kijiografia, zimeonesha El Niño inatarajiwa kuathiri maeneo mengi duniani hasa kuelekea mwisho wa mwaka 2023. Athari kubwa zaidi zitaonekana kwenye maeneo ya Nchi zenye hali ya Joto

Athari zaidi za El Niño zinaweza kuwa na madhara makubwa katika maisha ya kila siku, baadhi yake ni kuporomoka kwa Usalama wa Chakula, Ubora wa Hewa na Maji, Miundombinu, Magonjwa yanayoenezwa na Wadudu na Maji.

=============

Akizungungumza kupitia mtandao akiwa jijini Geneva Uswisi Dkt. Maria Neira ambaye ni Mkurugenzi wa Mazingira,mabadiliko ya tabianci na afya wa WHO amesema utabiri wa hivi karibuni unaonesha kuwa hali ya El Niño sasa iko na inatarajiwa kufikia kilele chake kati ya mwezi Septemba 2023 na Februari 2024.

“El Niño inaweza kusababisha matukio mbalimbali ya hali mbaya ya hewa, ikiwa ni pamoja na ukame, mafuriko, vimbunga, na mawimbi ya joto, ambayo yote ni hatari kwa afya ya binadamu.” Amesema Dkt Neira.

El Niño inatarajiwa kuathiri maeneo mengi ulimwenguni lakini athari kubwa zaidi zitaonekana kwenye maeneo yenye hali ya ya joto, ikiwa ni pamoja na nchi na maeneo ya Afrika, Amerika ya Kusin, pamoja na Kusini na Kusini-Mashariki mwa Asia ambako huathirika zaidi na majanga ya asili.

Athari za kiafya ziletwazo na El Niño

Kwa kubadilisha hali ya hewa, El Niño inaweza kuwa na madhara makubwa kwa viashirio muhimu vya afya kupitia, mambo mbalimbali kama vile; athari kwa usalama wa chakula, ubora wa hewa na maji, mifumo ikolojia na usalama wa miundombinu ya afya. Matukio ya magonjwa yanayoenezwa na wadudu na magonjwa yanayoenezwa na maji, kukabiliwa na moshi na moto wa nyikani, na mafuriko na athari za kiafya na lishe zinazohusiana na ukame.

Miradi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yakwamua jamii nchini Ethiopia.

Picha: FAO/Tamiru Legesse
Miradi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yakwamua jamii nchini Ethiopia.

Nchi zijiandae na athari zifuatazo za kiafya:

  1. Uhaba wa chakula na kuongezeka kwa utapiamlo wa wastani na wa hali ya juu hasa miongoni mwa walio hatarini zaidi.
  2. Kuongezeka kwa magonjwa yatokanayo na maji kama vile kipindupindu kutokana na uhaba wa maji au mafuriko na miundombinu ya vyoo.
  3. Ongezeko la milipuko ya magonjwa yanayoenezwa na mbu kama vile malaria katika maeneo ya nyanda za juu ambayo kwa kawaida ni baridi san, na ongezeko la hatari ya Homa ya Bonde la Ufa.
  4. Kuongezeka kwa idadi ya watu walioathiriwa na magonjwa ya kuambukiza kama vile surua na uti wa mgongo.
  5. Kukatizwa kwa huduma za afya kutokana na ukosefu wa maji katika hali ya ukame au uharibifu wa miundombinu ya afya kutokana na mafuriko na vimbunga.
  6. Joto kali na ongezeko la hatari ya moto wa mwituni
Familia ikipata mlo wao wa kila siku nyumbani kwao wilaya ya Balaka nchini Malawi (Juni 2016)

UNICEF/Sebastian Rich
Familia ikipata mlo wao wa kila siku nyumbani kwao wilaya ya Balaka nchini Malawi (Juni 2016)

WHO inafanya nini?

Ingawa athari halisi za matukio ya El Nino haziwezi kutabiriwa kwa usahihi, lakini WHO inatoa msaada kwa nchi ambazo athari ya El Niño zinatarajiwa kutokea.

Wanafanya hivyo kupitia ufuatiliaji endelevu wa utabiri, tathmini za hatari, uimarishaji wa juhudi zinazowezekana za kukabiliana na kujiandaa pamoja na mipango ya dharura na uimarishaji wa magonjwa yaletwayo na El Niño

WHO ni sehemu ya mifumo ya Umoja wa Mataifa ya uratibu na ufuatiliaji wa El Niño na inafanya kazi kwa karibu na mashirika kama vile WMO linalohusika na utabiri wa hali ya hewa duniani.

WHO inaratibu katika ngazi za kimataifa, kikanda na nchi ili kutoa taarifa na usaidizi wa kiufundi kwa Nchi Wanachama na washirika wa afya na kuimarisha utayari wa matukio ya afya yanayohusiana na El Niño.
 
sitasahau 97 ilivyosababisha maji yakaanza kutoka chini,chemchem kila sehemu.

inafika kipindi mnalimisi jua,linawezashinda wiki mbili halijachomoza kabisa,mihogo ikaozea shambani,mahindi yakadumaa,mpunga unapenda maji ila hapa uliyashindwa😅😅 ukafa.
 
Nakumbuka nilikua chalii mdogo,moja ya mvua za elnino ilinyesha kuanzia sa8 mchana hadi sa5 usiku,kabla mvua haijaanza lilitanda wingu kubwa jeusi sijawahi pata kuliona,mvua ilikua kubwa yenye upepo na radi za kutosha. R.I.P bro ulinibeba mabegani ili tuvuke kijito kilichojaa maji.
 
Back
Top Bottom