Fahamu kuhusu gari aina ya Land Rover Freelander

Wataalam, naomba kujua kama Land Rover Freelander ni gari nzuri kwa matumizi ya kawaida hapa kwetu Tanzania.

Kwa kifupi, Freelander hazifai kwa mazingira ya Tanzania. Kama unataka compact SUV nunua toleo la kwanza la Toyota RAV4.
 
Wataalam, naomba kujua kama Land Rover Freelander ni gari nzuri kwa matumizi ya kawaida hapa kwetu Tanzania.

nunua ya kuanzia 2005 onwards....toleo la mwanzo walichemsha sana zinaua cylinder head sana.
 
Kwa ufupi nimeanza kupata majibu labda nitoe consideration kwa zile za kuanzia 2005, ila tayari nimeshapata woga na hizi Freelander.
 
Mie pia sikushauri ununue Freelander. Mbali na spea na mafundi kushindwa kuzimudu.
Pia ujue ukinunua huna wa kumuuzia tena,labda ukubali kuuza kwa bei ya bodaboda.

Na ndio maana hata kwenye Yard nyingi Gari hizi huzikuti.

Ila kama unataka Kujaribu,huku ipo inauzwa 7m old model,zile zilizotolewa serikalini.
Ina miaka 8 haijapata wa kununua
 
Hizi gari wengi wamefunga Engine ya Rav 4
 
Mie pia nina miliki freelander ya mwaka 1998, gari ni kichefuchefu hicho spare muhimu hazipatikani hata kama ukieenda autorover au morogoro stores ngumu sana wanazo chache na sio zote muhimu, option yako kubwa ni kwenye used Tabata dampo na Sinza darajani kwa mbele. Tena bei zipo juu iwe mpya ama used.

Ukipata Manual Diesel atleast machine inakaa lakini itakusumbua within three years.
 
Jamani ahsanteni. mkataa pema pabaya pana mwita.

SINUNUI TENA
 
jaman kwa anayefahamu mazuri na mabaya ya toyota alphad
, toyota alphad g na toyota alphad v, naomba anisaidie nimezipenda nataka niaagize.
 
Habari wanajamvi.

Hakuna gari nazipenda kama za kampuni ya landrover, na kwenye jamii hiyo, Freelander ndio chaguo langu la kwanza likifuatiwa na discovery hasa td5.

Nimeshaendesha sana 110 ya diesel zile za mwanzo, defender tdi, na range rover 4.0 ya mwaka 1998, (ila si freelander na discovery). Hizo zote nilizoendesha hazijawahi kusumbua engine kiasi cha kuitwa pasua kichwa, au niseme hazijasumbua kabisa.

Labda range rover inatesa kidogo system yake ya air suspension (au busta). Wengine hufunga suspension za kawaida ili kuondokana na hilo tatizo. Pia bei ya spare hasa za range rover pengine ni juu kidogo kuliko magari tuliyozoea kama ya Toyota

KUHUSU FREELANDER
Kama nilivyotangulia kusema ni gari ambazo nazipenda sana, kwa sasa nina toyota mark II ila ndoto yangu ni kumiliki freelander au discovery.

ILA SASA, habari nazosikia kuhusu freelander hazinitii moyo kabisa, sijui kama ishu ni mafundi hawazijui au ni kweli hizi gari ni pasua kichwa na zikianza kukutesa tiba ni kubadili engine tu kuweka ya rav 4 (3s).

Kikubwa naomba kwa wajuzi na wazoefu wa magari haya, mnipe mawazo yenu na ushauri. Natanguliza shukrani
 
Daah..hata mimi nimeskia hizi gari ni hovyo sana hasa kwenye engine.. Mkuu kuna uzi humu ndani umebandikwa na Mshana jr unahusu magari na ushauri..hebu ufuatilie unaokota kitu..
 
Engine ya FreeLander haivumilii shida ikiwa wewe ni mtu wa safari ndefu, pia consumption ya mafuta ni shida, huyu mnyama anakunywa hasa!
 
Wakuu kwa aliyetumia hii gari naomba anijuze ubora wake au hata kama mtu anahamu na gari hii nimetokea kutamani kuitumia. please
 
Shosti limbia ufe. hiyo sio gari don't touch the dial.Its so comfortable but not good for human consumption myfried.
matatizo
 
kuna mzee kalipaki ataki hata kuliona. kwa ufupi ni kimeo
 
Wakuu habari!

Naombeni msaada wa kujua machache kuhusu hii gari LandRover Freelander.

1. Kwa kulinganisha na Suzuki Escudo na Rav 4. Ni ipi inafaa kwa kuhimili mikiki ya barabara zetu?

2. Vipi upatikanaji wa spare zake kwa hapa bongo? Na je spare zake ni gharama au bei ni za kawaida?

3. Ipi ni bora? Inayotumia Diesel au Petrol?

Naomba ushauri na mengine ambayo sijauliza kuhusu hii gari.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Tunaiita chembe cha moyo. Kuna msela alitoka PhD UK karudi nayo bongo ikazingua engine tukapeleka ilala jamaa wakafunga engine ya Rav4 haikufit jamaa akauza chuma chakavu 3m
 
Tunaiita chembe cha moyo. Kuna msela alitoka PhD UK karudi nayo bongo ikazingua engine tukapeleka ilala jamaa wakafunga engine ya Rav4 haikufit jamaa akauza chuma chakavu 3m
Duuuu aisee. Asante kwa maelezo yako. Naona nirudi kwenye Suzuki Escudo labda. Vipi kuhusu suzuki escudo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…