Habari wanajamvi.
Hakuna gari nazipenda kama za kampuni ya landrover, na kwenye jamii hiyo, Freelander ndio chaguo langu la kwanza likifuatiwa na discovery hasa td5.
Nimeshaendesha sana 110 ya diesel zile za mwanzo, defender tdi, na range rover 4.0 ya mwaka 1998, (ila si freelander na discovery). Hizo zote nilizoendesha hazijawahi kusumbua engine kiasi cha kuitwa pasua kichwa, au niseme hazijasumbua kabisa.
Labda range rover inatesa kidogo system yake ya air suspension (au busta). Wengine hufunga suspension za kawaida ili kuondokana na hilo tatizo. Pia bei ya spare hasa za range rover pengine ni juu kidogo kuliko magari tuliyozoea kama ya Toyota
KUHUSU FREELANDER
Kama nilivyotangulia kusema ni gari ambazo nazipenda sana, kwa sasa nina toyota mark II ila ndoto yangu ni kumiliki freelander au discovery.
ILA SASA, habari nazosikia kuhusu freelander hazinitii moyo kabisa, sijui kama ishu ni mafundi hawazijui au ni kweli hizi gari ni pasua kichwa na zikianza kukutesa tiba ni kubadili engine tu kuweka ya rav 4 (3s).
Kikubwa naomba kwa wajuzi na wazoefu wa magari haya, mnipe mawazo yenu na ushauri. Natanguliza shukrani