Jamani hamna Mwenye ushuhuda mzuri atutie moyo
Kilimo sio rahisi kama wengi wanavyofikiria, kwanza, usimamizi katika kilimo ni jambo la kuzingatia sana, mtu unaweka kibarua, unakaa mjini unategemea mambo yaende sawa, kumbuka hata kibarua ana interest zake unampa kazi ukigeuza mgongo hafanyi anatafta kaz nyingine ww anazidi kukuchelewesha, wengine ndio ivo unawaweka kambi unawahudumia haufik mara kwa mara kuwaona, unawalisha wanapiga kazi kidogo kwako wanaenda kwa wengine kupiga parttime.
Lazma uchezee hasara tu, ipo ivo hata katika pembejeo kama dawa, mbegu, mbolea na hata vifaa na nishati, unanunu hivyo vtu unawapa bila usimamiz mzuri wanauza then wanakwambia vimepungua, unanunua tena, lazima mwisho wa siku uchezee hasara.
Kitu kingine unazalisha nini?, na sehemu gan? sehem yeyote palipo na producers wengi na consumer wachache hapafai kufanyia kazi, nakumbuka nliwahi Lima tikiti katavi, mambo hayakuwa mazuri kabisa, nlipata faida kidogo, nliamua kuondoka huko nkafanyia kazi sehem nyingine, mambo yakawa vzuri, kilimo hakitupi ukikifanya kwa umakin hasa cha umwagiliaji, cha kutegemea mvua kina risk japo hata penyew ukiwa makin hautoki patupu.
Kuna changamoto za masoko hapa, cha muhimu hapa ni kuangalia misimu ya mbwago na misimu ambyo unacholima kinahtajika kwa wingi, jarbu kufatilia factors zinazoshusha mazao na zinazopandisha mazao sehemu unayofanyia kazi.
Mfano, wakulima Wa mboga mboga hawalimi kupindi cha masika(mvua nyingi) basi wewe Lima (kama una pesa anzisha greenhouse hata robo/ nusu heka inatosha, especially kwa wakulima wa mboga mboga. misimu ya low season kwa maeneo ya utalii hushusha mazao ya mboga mboga na matunda, na high season mazao hupanda, mambo ya dini mfno mfungo kwa waislam ushusha baadhi ya mazao ya mboga mboga kama bamia, na hupandisha mazao kama maboga, viaz na mihogo.
Kila shughuri yenye pesa ina changamoto kama ilivyo katika biashara yeyote, lakin kilimo dare to say ndio sekta pekee ambayo labour n too cheap. Uwe makini unapoiweka pesa yako hakikisha inafanya kazi uliyoikusudia (narudia tena usimamizi n mhimu sana katika kilimo, pata mazao ya maana soko n matokeo) .