Fahamu kuhusu kuanzisha biashara ya Mobile Money (M-Pesa, Tigopesa)

Kwa maana hiyo viwango havipo katika interval kwa kila hela utakayomuwekea mteja si ndio...?

Yaani natamani niendelee kukuuliza ila nahisi kama nitakuwa nakukwaza mkuu kutokana na ulivyonijibu hapo awali.
Mkuu hii biashara nilishawahi ifanya kidogo.....ni hivi kwa kila muamala kuna % unapata kama commision yako na hiyo ndio faida yako....mtu akitoa milioni moja kwa wakati mmoja kile kiasi anachokatwa mteja na ww unapata % yako....so wapo wanaotoa buku tano wanaoweka pia kuna % unapata so kwa mchanganyiko wa watej na wanavyokuwa wengi ndio unamake faida nzuri mkuu....hivyo tu
 

Nafkiri kama bado sijaeleweka vizuri au labda mie ndio nashindwa kuwaelewa vizuri.
 
safi mkuu, bahati mbaya sms huwa nazifuta , maana simu huwa inajaa sana.. ila naahidi, nitakupm sms mwez ujao

thanks to god the almighty
Ebo…kwani ungekuwa hajazifuta ungerusha kweli hizo sms!? Yy aamini kama anaamini vinginevyo apotezee!
 
Commission ni 0.15% ya kiasi kiasi unacho toa cash.
Hapa unamaanisha kuwa mteja amekuja amerusha balance kwenye simu yangu kama wakala then nikampa cash, right.

Na 0.1% ya kiasi unacho pokea kama float.
Na hapa sijaelewa kwa sababu mteja alipokuja mwanzo akataka kutoa si amenirushia float nikampa cash, sasa hiyo ya pili iweje tena nipokee float kwa nini isiwe mteja kaja na hela cash halaf nikamuwekea balance kwenye simu yake...?

Anyway, labda niweke hivi, zoezi langu kubwa litakuwa kwenye kuweka float kwenye simu yangu na kuwarushia watu waliopo site, it means ofisini huwa tunapata tabu ya kwenda mbali kuwarushia hela watu waliopo site, kama mwezi huu uliopita mimi binafsi nilituma zaidi ya milioni 18,yaani napewa hela naenda kwa wakala nawatumia hao wafanyakazi.

Sasa hiyo ni mimi tu, lakini kuna wengine huwa wanapewa pia kwenda kuwatumia wengine kwa hiyo kazi itakuwa ni kwenye kuweka float na kuwarushia watu wa site, that's why kwa kila 1mil nikimtumia mteja kwenye simu yake mimi kamisheni yangu inakuwa kiasi gani, hilo ndio swali langu wakuu.

Nisameheni sana kwa usumbufu aisee ila yote ni katika kutaka kujifunza zaidi kuliko kujifanya nimeelewa then nikakaa kimya halaf kumbe sijaelewa chochote it doesn't make sense.
 
Kuna kupokea na kutoa kwenye biashara hiyo
Ukitoa cash ukampa customer = 0.15%
Mteja akikupa cash= 0.1
 
Sawa lkn kwa nilivyomuelewa alimaanisha in total. Ukiadd up gawio kutoa M PESA, TIGO PESA NK ndio anafikisha 1.7M per month kitu ambacho kwa maelezo yake kinaweza tokea tu
 
Hapo sasa nimekuelewa vyema kabisa kiongozi wangu. Thanks a lot mkuu.
Mkuu mimi nahisi nimekuelewa zaidi unachotaka...nimeelewa kuwa kutokana na kazi unayofanya mmekuwa mkiwatumia hela watu walio site na ni hela nyingi so umeona uitumie iyo kama fursa badala ya kwenda kwa wakala uwe na line yako ya uwakala ili iyo miamala uwe unafanya mwenyewe na kupata faida...mimi sio mtaalamu wa mambo hayo but nilivyomwelewa jamaa hapo juu ukiwa na iyo line ya uwakala utakuwa kila ukimwingizia milioni moja mtu aliye site wewe faida yako ni 0.1 ambayo ni sawasawa na 1000....kwa ushauri wangu mkuu hizi biashara zina faida kama kuna mzunguko mkubwa wa watu wanaoingiza na kutoa pesa...ni vyema kama unabiashara nyingine ongezea na hizi huduma ili hiyo tender ya kuwatumia watu pesa site utakuwa unaipa iyo ofisi yako ya biashara...kama huna biashara unaweza anzisha na kuweka hii huduma...hii itawawezesha na watu wengine kutoa na kuingiza pesa kwenye biashara yako na si kutegemea tu faida ya miamala ya kuwatumia watu pesa site
 

Mkuu kinywa chako kimenena maneno yenye hekima na busara ya hali ya juu kiongozi.

Hilo ni wazo zuri sana umetoa nathamini mawazo yako na nakubali mchango wako kiongozi.

Nitalifanyia kazi hilo suala mkuu. Thanks.
 
Yupo dada ana mtaji wa M2 na faida anapata laki 4. Yupo kwny lango la hospital....
 
zap ndo nn naomba kuijua
 
Habari zenu wapendwa! Nilikuwa Nina wazo la kuanzisha biashara y uwakala w mpes na tho pesa,je nikiwa na mtaji wa ml.1 naweza kuanza?na je vip hii biashara inalipa?na ni taratibu gani nifate ili niwe wakala
 
Nenda Tigo na Vodacom wanawataalam wakukuelewesha procedures zote
 
Wazo kama langu,wadau tujuzeni laini za uwakala kwa tgo na m_pesa ni tsh ngap?
Za kununua mtaani tsh ngapi? Athari zake pia n.k
Biashara mwenza katika vibanda hv vya uwakala ni zp/ipi inafaa kuongezwa n.k
Mtaji kwa uwakala wa tgo na voda,Minimum kianzio kiwe ngapi bila kusahau faida na changamoto za hii biashara.
Natanguliza shukrani na mm,sorry kwa kudandia uzi...
 
Inalipa kama utaifanyia sehemu nzuri, tena kwa mtaji huo unapata laini zote mbili voda na tigo.
.
Ukizipeleka kwenye vimiji vinavyokua kwa kasi utapiga sana vichwa usithubutu kuianzisha sehemu ambako ziko M-pesa kama 20 hivi otherwise uweke na biashara ingine kama saloon n.k
 
Mtaji ni kuanzia laki tano tu unapata laini
 
Vipi na mtu akitaka kutengeneza till zaidi ya moja mfano till za tigo pesa mbili kwa kutumia tin namba moja inawezekana?
 
Vipi pia unaweza ukatambua vipi kuwa kuna mtu anatumia till zenye majina yako kwa sababu kuna mawakala wakuu wengine unapeleka nyaraka unakaa hata miezi mitano anakuja kukuambia nyaraka zako zilipotea kaandae nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…