Fahamu kuhusu Kupooza Uso/mdomo (Facial Paralysis): Mdomo kusogea upande: Visababishi na Matibabu

Fahamu kuhusu Kupooza Uso/mdomo (Facial Paralysis): Mdomo kusogea upande: Visababishi na Matibabu

Dr PL

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2024
Posts
327
Reaction score
537
ENT_2012_09_pp06_01.jpg


Picha kwa hisani ya Google.


Kupooza uso/mdomo ni hali ya mdomo kusogea pembeni au kwenda upande mmoja (kitaalamu huitwa Facial nerve paralysis/Bell's Palsy) ambayo husababishwa na matatizo ya mishipa ya fahamu ya uso/mdomo (facial nerve) ambayo husimamia na kuendesha utendaji kazi wa misuli ya uso/mdomo.

Mishipa ya fahamu ya uso (facial nerve) ziko za aina mbili: ya upande wa kushoto na wa kulia.

facial-nerve-and-muscles-Facial-Nerve-Center-OHNS-Stanford.jpg

Mshipa wa fahamu wa uso (facial nerve) [rangi nyeupe/dhahabu]

Uimara wa mishipa hiyo (kushoto na kulia) ndiyo hufanya uso/mdomo wako kuwa katika nafasi na muonekano wake wa kawaida.

Kutokana na hitilafu, kuharibika, kupooza au maambukizi katika mishipa hiyo ya fahamu ya uso (facial nerve paralysis) misuli inayosimamiwa na kuendeshwa na mishipa hiyo huwa midhaifu/hushindwa kufanya kazi yake hivyo mdomo/uso kusogea pembeni/upande mmoja.

Kukiwa na athari (hitilafu, uharibifu, maambukizi, kupooza) kwenye mshipa wa fahamu wa uso/mdomo (facial nerve) ya upande mfano wa kushoto basi misuli ya upande huo huwa midhaifu au hushindwa kufanya kazi na huvutwa na misuli ya upande wa kulia ambayo iko imara, hivyo mdomo huhamia/husogelea upande wa kulia. Vivyo hivyo kama mshipa wa upande wa kulia ukiwa na hitilafu mdomo huelekea kushoto.
Pia jicho la upande husika haliwezi kufumbwa kisawasawa, yaani mtu akifumba macho jicho moja hubaki wazi.

Visababishi:
Hali hii (facial nerve paralysis/Bell's Palsy) husababishwa na vitu mbalimbali mfano:

-maambukizi ya aina fulani ambayo hushambulia mishipa hiyo ya fahamu: bacteria, virusi kama HSV nk

-Ajali au kuumia au kuvunjika mifupa ya uso ambapo mishipa hiyo huweza kukatika au kugandamizwa

-maambukizi kwenye masikio (otitis media)

-uvimbe kwenye masikio, uso au ubongo ambao hugandamiza mishipa hiyo ya fahamu ya uso

-kiharusi (stroke)

-kisukari nk

Matibabu:
Matibabu ya tatizo la kupooza uso/mdomo (facial nerve paralysis/Bell Palsy) hulenga katika kutibu/kughulikia kisababishi. Kwa hiyo ni muhimu kufika hospitalini kwa uchunguzi na vipimo ili kubaini kisababishi na kukishughulikia.
 
Mimi nilidhani ni kiharusi tu kinaleta hali hiyo - kumbe kuna visababishi vingine!
 
Back
Top Bottom