JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Mgawanyo wa madaraka ni mgawanyo wa majukumu ya serikali katika matawi tofauti ili kuzuia tawi moja kutekeleza majukumu ya msingi ya lingine.
Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeeleza Mafundisho (Doctrine) ya mgawanyo wa madaraka kwa kugawanya mihimili mitatu kwenye mamlaka na madaraka tofauti mihimili hiyo ni Serikali kuu, Bunge, na Mahakama.
Serikali kuu inatajwa chini ya Sura ya Pili ya Katiba ambapo kazi yake ni kutekeleza sheria ambayo imetungwa na Bunge au na mamlaka nyingine ambazo zimepewa nguvu na bunge kutunga sheria.
Bunge limetolewa ufafanuzi chini ya Sura ya Tatu ya Katiba hiyo ambapo kazi yake ni kutunga sheria.
Na Mahakama imetajwa chini ya Sura ya Tano ambapo kazi yake ni kutafsiri sheria.
Kusudi la mgawanyo wa madaraka ni kuzuia mkusanyiko wa nguvu na kuwezesha muhimili mmoja kuwajibisha muhimili mwengine ikiwa utakosea.
Upvote
1