JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Ripoti ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kitengo cha Afya inaeleza kuwa, Msongo wa Mawazo ni mfadhaiko wa akili anaoupata mtu kutokana na shida, taabu, dhiki, matatizo au changamoto zinazomkabili katika maisha.
Ripoti inabainisha mgawanyiko wa sababu za Msongo wa Mawazo kuwa ni sababu za kibiologia na kisaikolojia. Sababu za kibiologia ni pamoja na mtu kurithi vinasaba kutoka kwa Mzazi na Magonjwa ya muda mrefu.
Sababu za kisaikolojia ni kama vile matukio yasiyofurahisha ikiwemo ubakaji, uvamizi, ajali, kufiwa, kutekwa nyara, kutoelewana na jamii pamoja na changamoto za kila siku kama Ugoni, Talaka, Mimba kuharibika, kufungwa au kukosa kazi pamoja na migogoro sehemu za kazi.