Jina lake halisi anaitwa N!xau. Inakadiriwa alizaliwa kati ya mwaka 194 au 1944, kwani yeye binafsi hakuwa akijua umri wake. Alikuwa ni mzaliwa w nchini Namibia kijiji cha Tsumkwekatika jangwa la Kalahari.
Hakuwahi kujifunza sanaa ya uigizaji hapo kabla, kwa sababu huyu alikuwa ni mtu pori halisi [yaani kama vile anavyoishi kwenye mu zake basi huo ndio uhalisia wa maisha yake aliyokuwa akiishi hapo kabla] hivy katika maisha ya porini na Jangwani hakukuwa na sanaa ya maigizo. Ila wazungu walimtafuta mtu ambaye alikuwa ni bushman halisi ili wamuwek kwenye muvi zao ndipo wakakutana na huyu bwana.
Hivyo alianza maisha yake mapya ya ucheza filamu mwaka 1980 -1994. Zifuatazo ni filamu maarufu zaidi alizopata kucheza na zikaja kuwa kubw Zaidi ulimwenguni kote hata kufanikiwa kujishindia TUZO mbalimbali: "The God Must Be Crazy II, Crazy Safari, Crazy Hong Kong na The Gods Must Be Funn in China".
Katika movie yake ya kwanza ambayo ni "The Gods Must Be Crazy "alilipwa dollars 300 tu za kimarekani, ambazo kiuhalisia ni kiasi kidogo mno cha pesa, lakini hela hizo zote alizichan sababu hakuwa akijua matumizi ya hela kwa sababu hapo awali hakuwa kutumi hela. Ila baadae baadae alifundishwa umuhimu wa hela, hivyo katika filamu zilizofuata akaanza kudai malipo tena makubwa kweli kweli.
Pia kabla ya kucheza filamu yake ya kwanza alikuwa bado hajawahi kuwaona Wazungu machoni pake, tena hakuwa amewahi kufika mjini. Baada ya kumaliza maisha yake ya uigizaji huko ughaibuni ndipo aliporudi nchini kwao Namibia, ndipo alipoanza maisha mapya alijenga nyumba nzuri ya kifahari kisha akaanza kujihusisha kwa shughuli za kilimo na ufugaji, ambapo katika mifugo aliyokuw akifuga haikuzidi idadi ya 20, na hiyo ni kwa sababu hakuwa akiweza kuhesabu zaidi ya 20.
Lakini bado hakuacha tamaduni yao ya Uwindaji hivyo aliendelea kuwa hivyo licha ya utajiri aliokuwa nao. Nchini kwao Namibia anaheshimika mno kuwa ndiye Msanii mkubwa na mtu maarufu zaidi kuwahi kutokea nchini mwao.